IGP Simon Sirro: Magaidi wapatao 300 kutoka Msumbiji walivamia Kijiji cha Kitaya mkoani Mtwara

INSPEKTA Jenerali wa Polisi (IGP) nchini Tanzania, Simon Sirro amesema, magaidi zaidi ya 300 kutoka Msumbiji walivamia Kijiji cha Kitaya Mkoa wa Mtwara na kufanya uhalifu mbalimbali ikiwemo mauaji.

“Magaidi wapatao 300 kutoka Msumbiji, walivamia Kijiji chetu cha Kitaya na kufanya uhalifu mbalimbali ikiwemo mauaji,” amesema IGP Sirro aliyekuwa anazungumzia hali ya usalama kuelekea Uchaguzi Mkuu tarehe 28 Oktoba 2020.

IGP Sirro amesema, “tumefuatilia baadhi ya watu, wamekamatwa na wengine ni wa kwetu hapa tumewakamata tunaendelea kuwahoji.”

IGP Sirro amesema, “tunaendelea kupambana nao ili kuupata mtandao wote ulioanzia kule Kibiti na Rufiji ambao tulipambana nao wakaona wameshindwa.”

Mkuu huyo wa jeshi amesema, watahakikisha wanakamatwa iwe wanakwenda Msumbiji, Kenya au kwingineko ili “mwisho wa siku haki itandendeka na watakamatwa na kupelekwa mahakamani.”

Soma pia > Tetesi: - Kuna jambo baya linaendelea Mtwara...
wapate tab sana
 
Hao watu wakizidisha mashambulizi Tanzania itaingia Msumbiji ipende isipende.
Pamoja na kwamba vita ni gharama kubwa naamini Tanzania inatamani ikawavuruge hao magaidi kulekule Msumbiji. Tatizo ni kuwa huingiizi jeshi lako nchi ingine kiholelaholela tu. Inabidi ukubaliwe na nchi husika. Na hiyo ina mambo yake kwa nchi inayokubali jeshi la nchi ingine liingie kwake japo faida ni kubwa kusaidiwa.

Tatzo ni pale Msumbiji unaweza kukuta kuna wanajeshi na wakubwa serikalini wengi tu hawataki lile tatizo liishe.... Sasa unategemea nini hapo. Au Wanaweza kupendelea majeshi ya kukodi yapambane na magaidi ili wayalipe na wapate kamisheni na nk. JWTZ wakiingia kichwakichwa wanaweza kuuzwa.

Pasipo na rushwa na penye jeshi imara na serikali imara magaidi hayatambi. Hebu angalia yanayotokea Nigeria na boko haram yao
 
Magaidi 300 mbona wengi sana, kwani si muda mrefu habari kuwa huko jirani zetu si sàlama, kwanini wasiweke ulinzi? Ila wakisikia kuna maandamano utasikia tulijajua kutakuwa na vurugu watu wenyewe hata nyembe hawana lakini nguvu kuuuuubwa kuwazuia
 
kwa mujibu wa taarifa magaidi walipita njia za bahari/maji na walipoondoka walichukua simu zote kijijini
Kama walichukua simu zote then Ni rahisi sana ku wa track. Kijana mmoja mzuri kwenye IT anaweza kuwaonyesha polisi hao wahujumu walipo kwa kushirikiana na Telmocambique.
 
INSPEKTA Jenerali wa Polisi (IGP) nchini Tanzania, Simon Sirro amesema, magaidi zaidi ya 300 kutoka Msumbiji walivamia Kijiji cha Kitaya Mkoa wa Mtwara na kufanya uhalifu mbalimbali ikiwemo mauaji.

“Magaidi wapatao 300 kutoka Msumbiji, walivamia Kijiji chetu cha Kitaya na kufanya uhalifu mbalimbali ikiwemo mauaji,” amesema IGP Sirro aliyekuwa anazungumzia hali ya usalama kuelekea Uchaguzi Mkuu tarehe 28 Oktoba 2020.

IGP Sirro amesema, “tumefuatilia baadhi ya watu, wamekamatwa na wengine ni wa kwetu hapa tumewakamata tunaendelea kuwahoji.”

IGP Sirro amesema, “tunaendelea kupambana nao ili kuupata mtandao wote ulioanzia kule Kibiti na Rufiji ambao tulipambana nao wakaona wameshindwa.”

Mkuu huyo wa jeshi amesema, watahakikisha wanakamatwa iwe wanakwenda Msumbiji, Kenya au kwingineko ili “mwisho wa siku haki itandendeka na watakamatwa na kupelekwa mahakamani.”

Soma pia > Tetesi: - Kuna jambo baya linaendelea Mtwara...
NAOMBA KUJUZWA HIVI MIPAKA INALINDWA NA POLISI AU JWTZ?
 
Magaidi 300, WTF!!

Hii ni sinema tu kama sinema zingine, lengo ni kutia hofu watu ili wasikinukishe pale tume ikivurunda... which is most likely.

Amateur scriptwriter!!
 
kwanza tushukru kumekuwa na taarifa maana kulikuwa na romus nyingi bila kukanushwa wala kuthibitishwa.. sasa basi kunakitu cha msingi sana cha kujifunza.... ugaidi si jambo la kufurahia hat kidogo... tunapaswa wote kwa pamoja kulaani na kulisuport. jeshi letu... haijarishi tunatofautiana mitazAmo au itikadi za vyama au siasa.. ila linapokuja swala la amani ya nchi yetu tunapaswa kuilinda kwa ghalama zote...

leo tunajadili tumiwa tupo nyuma ya keyboard za sim au computa bt madhira yakitokea hakutakuwa na hyo fursa... tunaweza tukachukua kama jambo dogo lkn ugaid ni miongoni mwa magonjwa ambayo hayana tiba ila unaweza kuzuia ugaidi...

hvyo tuviunge mkono vyombo vyetu vya usalama tuache lugha za kuudhi kwa majeshi yetu ili kwa pamoja tutashinda vita hii
niwaombe pia wanasiasa hasa wenye majina makubwa waliache jeshi lifanye kazi yao...

idada iliyotolewa na IGP ya magaidi inaukwel maana yy anavyo vyanzo vingi vya taarifa sahihi na alichokisema ni kuonesh tu ukubwa wa tatzo...
tusiache kumuomba Mungu ili aondoe hii ghasia na watu wa mtwala na tz kwa ujumla amani iendelee kudumu..

MUNGU IBARIKI AFRIKA
MUNGU IBARIKI TANZANIA
TUDUMISHE AMANI YETU
KWA PAMOJA TUTASHINDA
 
Kama hivyo sioni umuhimu wa kuweka jeshi huko mipakani,na wanajeshi wakome kujinasibu kwamba wanalinda nchi,kumbe hatupo salama.Huu ni udhaifu mkubwa ktk kazi ya ulinzi,wasipo weka ulinzi ktk hivyo vipenyo watu wata......
mipaka ni kwa uvamizi ila sidhani n ka kulinda kila kipenyo maana kuko wazi na huwezi juwa wapi ni wapi na ikumbukwe ni kms nyingi
 
Wanaogopa aibu kama ya Westgate kenya
Huwezi kufananisha aibu ya Wastegate na lilotokea Mtwara. Kule ni mtu ameingia kwenye mall, na mall ilikuja kuwa surrounded na majeshi ya KDF na private forces, wakaishia kudunguana wenyewe kwa wenyewe kwa bifu zao na majeshi kuondoka na peremende za eclairs.

Cha msingi saivi, Jeshi liingie msumbiji kumalizana nao.
 
Kuingia msumbiji n swala ambalo lazima msumbiji waridhie na lazma watatubana katika ukubwa wa kikos
 
INSPEKTA Jenerali wa Polisi (IGP) nchini Tanzania, Simon Sirro amesema, magaidi zaidi ya 300 kutoka Msumbiji walivamia Kijiji cha Kitaya Mkoa wa Mtwara na kufanya uhalifu mbalimbali ikiwemo mauaji.

“Magaidi wapatao 300 kutoka Msumbiji, walivamia Kijiji chetu cha Kitaya na kufanya uhalifu mbalimbali ikiwemo mauaji,” amesema IGP Sirro aliyekuwa anazungumzia hali ya usalama kuelekea Uchaguzi Mkuu tarehe 28 Oktoba 2020.

IGP Sirro amesema, “tumefuatilia baadhi ya watu, wamekamatwa na wengine ni wa kwetu hapa tumewakamata tunaendelea kuwahoji.”

IGP Sirro amesema, “tunaendelea kupambana nao ili kuupata mtandao wote ulioanzia kule Kibiti na Rufiji ambao tulipambana nao wakaona wameshindwa.”

Mkuu huyo wa jeshi amesema, watahakikisha wanakamatwa iwe wanakwenda Msumbiji, Kenya au kwingineko ili “mwisho wa siku haki itandendeka na watakamatwa na kupelekwa mahakamani.”

Soma pia > Tetesi: - Kuna jambo baya linaendelea Mtwara...
Aache uwongo hao police hawana jeuri ya kupambana nao,ndio mana jwtz wamepelekwa huko
 
Back
Top Bottom