Benaya-
JF-Expert Member
- Jul 31, 2019
- 4,415
- 7,631
Nimeanza kwa swali: Hivi mzee wetu Simoni Sirro ambaye kwa asili ni mtu makini, anajisikiaje kwa jeshi la polisi analiongoza kutumika kisiasa?
Miezi iliyopita tumeshuhudia baadhi ya watu waliokuwa wanasiasa kuachiwa huru na mahakama kutoa hukumu kuwa hao watu walishitakiwa kimakosa ambayo kimsingi polisi ndio iliwatuhumu mfano Mdude nk.
Je, mzee wetu Sirro haoni kuwa si kila agizo analopewa au watu wake wanapoagizwa kuwafanyia raia ni wakati sasa wajiepushe nayo?
Haoni kuwa CV yake inachafuliwa?
Mzee wetu Sirro, kuna wakati ninakuhurumia sana.
USHAURI WANGU
1. Nashauri ajaribu kutumia hekima na busara. Anapopewa maagizo yanayovunja haki za msingi za wananchi kwa mujibu wa katiba
2. Njia bora ya kuwanyamazisha watu kama hawa wanaokusanyika kwa kudai katiba, ni kuwaita viongozi na kutumia diplomasia badala ya nguvu na kubambikia kesi.
3. Kumbuka huna miaka mingi kuwa ofisini na muda sio mrefu unarudi uraiani au kufanya kazi tofauti na hii kazi ya damu na laana hivyo jijengee mazingira ya kukumbukwa na historia.
Mwisho, mnayoyapanda yataota, yatakuwa, yatazaa na yatakomaa na kuiva; mwishowe mtavuna na kula matunda yake.