IGP Sirro: CHADEMA wanamuona Mbowe Malaika hawezi kosea, ushahidi tunao

IGP Sirro: CHADEMA wanamuona Mbowe Malaika hawezi kosea, ushahidi tunao

Bila wewe kwenda Dodoma na Bashite Cyprian Musiba Heri kisanduku na wasiojulikana kumpiga risasi angefikaje huko ughaibuni?
Ugonjwa wa Akili ni hatari

naona unapata hallucinations vividly
Grow up son
 
Ugonjwa wa Akili ni hatari

naona unapata hallucinations vividly
Grow up son
Aliyekuambia kuwa una Akili timamu ni nani? Ugonjwa wako wa Akili usikudanganye kujifanya jaji wa Akili, kutetea uonevu unyanyasaji kuwabambikia kesi wapinzani ndiyo Ugonjwa wa Akili Hatari zaidi kupita wote Duniani
 
Jeshi la Polisi limeundwa kwa mujibu wa sheria na moja ya majukumu yake makubwa ni KULINDA RAIA NA MALI ZAO, lkn pia kulinda AMANI na UTULIVU.
haijalishi yeyote atakaye vunja sheria atachukuliwa hatua kali za kisheria bila kujali chama chake awe ccm, chadema au hata kama hana chama atachakazwa vilivyo.
Amani ya nchi yetu ni muhimu zaidi kuliko chama chochote kile.
Amani ya Nchi huduma pindi chama Tawala kisipotumia Polisiccm kuwabambikia kesi wapinzani CCM ndiyo inavuruga Amani ya Nchi kwa kuendekeza vitendo haramu vya kishamba na kishetani
 
Polisi na dini wapi na wapi?
Nchi yetu, serikali na vyombo vya Dola havina dini.
Yapo matukio mengi sana yenye shaka ya haki kwa polisi.
Ni vizuri Bwana Yesu asihusishwe kwa sababu kwake hakuna shaka ya HAKI.
 
Its very risky kumpa kesi ya ugaidi mtu km Mbowe

sijui hili litaishaje
Am somehow convinced Serikali wana ushahidi

na kama ni kweli daah.,
Ngoja tuyaone yajayo mahakamani
 
acheni ugaidi, hii nchi sio ya kwenu peke yenu. kama amefadhili ugaidi mnataka asiguswe? na mnashinikiza aachiwe hamuoni kama mnaingilia mahakama, kesi si ipo mahakamani? DPP si ametoa kibali cha kuanza kusikilizwa (si mmeona ile charge ina consent n a certificate), manake kesi inaanza kusikilizwa haraka, au mnaogopa ushahidi utakaoletwa? tulieni dawa iwaingie.
Kwa kweli kwenye hili watu wawe neutral
Hadi proven beyond reasonable doubt
 
Naomba kueleweshwa kwa mujibu wa sheria ni wapi kuandamana kumepewa jina la uvunjifu wa amani?

Naomba kifungu cha sheria kinachotaja maandamano kama uvunjifu wa sheria.Nijuavyo maandamano ni haki ya raia kueleza masahibu au uungaji mkono jambo fulani.
Polisiccm hawatumii Sheria za Nchi kuwabambikia kesi wapinzani hutumia fikra zisizo sahihi za mtukufu mwenyekiti wa CCM kuwabambikia kesi kuwaonea kuwanyanyasa wapinzani
 
Siro ameshazeeka asituharibie taifa.

Hakuna duniani mtutu wa bunduki ulileta amani.

Haya mambo yake yasijeleta waasi nchini kwetu. Wengine hatuna pa kwenda asee.

Huko pwani ya mtwara wanawasumbua, anajua ni gharama kiasi gani kama nchi tunaitumia?

Asidhani kujaza vikosi na silaha ndiyo ushindi,ajue tunayumbishwa kiuchumi.

Sasa nchi yote ikiwa haina amani anadhani ni kiasi gani cha fedha kitatumika?

Ama ndiyo wanatafuta namna wajitajikwapulie fedha zetu.

Hatupo tayari,wanaondamana wawaache wafanye hivyo ilimradi hawafanyi uharibifu. Polisi wayaongoze tena hayo maandamano.
Hata kama wanatembea hadi hai, acha waende.

Ushahidi mnao tayari,tungepende kuona kesi inasomwa mfululizo tena mkiweza ili TBC ipate umaarufu irushe live kesi.

Tuipende amani,tuipende nchi yetu.

Yote ni kuwa watu wa haki,utu na kuvumiliana.

Nchi yangu Tanzania, naipenda Tanzania.
 
Sijawahi kuwaamini polisi hata kama ni usiku wakaniambia nje giza nitatoka mwenyewe nje kuhakikisha.
Polisi ni ccm, CCM ni polisi
Polisi sio walinzi wa raia na mali zao polisi ni wezi, majambazi
Polisi ndio wanaongoza kwa rushwa
Polisiccm ni Tawi la CCM
 
Wapinzani hawana fujo hawana bunduki wanadai katiba kwa Amani lakini cha ajabu sasa Polisiccm na CCM wanawabambikia kesi za ugaidi, Tanzania kuulizia kudai katiba mpya ni ugaidi ni kioja kilioje Duniani
 
Waheshimiwa habari zenu!

Tangu Mbowe ameshikwa ni wiki mbili sijui tatu zimepita sasa. Wengi tulilalamika kuwa ameonewa na kwamba kashikwa kwasababu za kisiasa tu.

Leo IGP Sirro katoa ufafanuzi juu ya kushikwa kwa Freeman Mbowe. Ingawa IGP Sirro kaenda mbali kaongea utadhani mahakama imeshamtia Mbowe hatiani.

Ok turudi kwenye zima ya uzi wangu huu. Niko hapa napiga magoti kwa mtawala mwenye haki anayehukumu kwa haki. Kama Mbowe kahusika na ugaidi Mungu amuhukumu haraka, kama Mbowe hajahusika na ugaidi Mungu amuhukumu aliyemsingia.

Niliacha wiki moja ya neema, wiki ambayo Mbowe au waliomsingizia kesi kama wapo wamgeukie Mungu. Wiki ambayo imeshaisha na sasa tumeingia wiki ya hukumu. Wiki hii tutapata jibu
 
Hii nchi wanakoipeleka siyo, kutoka kwenye siasa za hoja kwa hoja mpaka kwenye siasa za kuharibiana maisha, wanatengeneza visasi vitakavyokuja kuleta madhara kwa taifa inaweza isiwe leo wala kesho

Mwendazake ametuachia taifa la ovyo sana katuaribia nchi, hatukua na siasa za hivi na hata kama zilikuepo si kwa kiwango hiki.

Naona ule mkwara wa kuachia watu na kufuta kesi ilikua ni kusafishia njia mashekh wa uamusho
Umesahau mauaji ya Morogoro Mwangosi, milipuko ya mabomu Arusha, Kibanda kutobolewa macho, Ulimboka kung'olewa meno(sjui alienda wapi)..

Mbona marais wote wamefanya mamboz sema umesahau
 
Aliyekuambia kuwa una Akili timamu ni nani? Ugonjwa wako wa Akili usikudanganye kujifanya jaji wa Akili, kutetea uonevu unyanyasaji kuwabambikia kesi wapinzani ndiyo Ugonjwa wa Akili Hatari zaidi kupita wote Duniani
Minyoo ni shida
 
View attachment 1877322
IGP Simon Sirro leo Agosti 2, 2021 akizungumza kukamatwa kwa Mwenyekiti wa CHADEMA Freeman Mbowe


IGP Simon Sirro leo Agost 2,2021 amefanya mkutano na Waandishi wa Habari ambapo amezungumza mbalimbali kuhusu kukamatwa na Mwenyekiti wa Chadema pamoja na vuguvugu la kutaka kufanya maandamano. Akiwa katika mkutano huo SIrro alisema yafuatayo:

“CHADEMA wanaona Mwenyekiti wao (Mbowe) ameonewa na wanasema hawezi kuwa hivyo wanamuona ni Malaika hawezi kufanya kosa”

“Kabla ya Uchaguzi nilisema kuna Watu wamepanga kuhakikisha Uchaguzi haufanyiki, nilisema kuna baadhi ya Watu wamepanga kulipua visima vya mafuta na kufanya mauaji ya Viongozi na nilisema tutawakamata kabla hawajafanya hivyo”

“Tuliwakamata kabla, hayo ya Mwenyekiti wao (Mbowe) sitaki kuzungumzia sana lipo Mahakama ila wajue yeye ni Binadamu kama Binadamu wengine na anaweza kufanya kosa tumempeleka Mahakamani tuache Mahakama itimize wajibu wake”

“Kama kweli ni mkweli Mwenyekiti wao (Mbowe) na anamuamini Mungu waende wamuulize habari hiyo, kuna mambo unaweza kuyafanya kwamba ni siri lakini ndio mana Vyombo vya Habari vipo, niwaombe Watanzania wenzangu usilolijua ni kama usiku wa giza usiingie kwenye mtego ambao hujui aliyeutega ana jambo gani”

“Waende wamuulize huyo Mtu tuliyempeleka Mahakamani (Mbowe) kwamba hili jambo unalijua na kama ni ukweli ana Dini yake na anamjua Yesu Kristo aende aaambiwe, tunamuonea kwa lipi ?, tupate nini?, tuna ushahidi wa kutosha tuache Mahakama iamue, kafanya Yes hakufanya Yes lakini habari ya kikundi cha Watu kusema tunataka kuandamana wewe ni nani Bro!? hiyo nafasi hauna”

Awaonya Wanaotaka kuandamana
“Niwaombe Watanzania tuache wale Watu wachache ambao wanataka kupambana na Serikali wapambane nayo labda wana sababu zake lakini Mtu wenye hekima na busara anielewe, lakini kikubwa kama wameandaa kwenda Canada au Marekani wajiandae ila hatuwezi kuruhusu Watu wachache wavuruge Nchi kwasababu wamekosa madaraka”

“Habari ya kusema mnataka kuandamana mnavunja sheria na ukivunja sheria usilaumu Jeshi, ukivunja sheria umeingia kwenye uhalifu, Sirro hatokuacha na Polisi hawatokuacha na ndio maana wanafanya siasa kwa sababu amani na utulivu upo, Sisi hatufanyi Siasa”

“Niwaombe Watanzania ambao wameambiwa mkusanyike kutoka Mara kutoka wapi sijui na muelewe Mahakamana ni kituo nyeti ni kama Kituo cha Polisi ukitaka kuvamia utakung’utwa kwa mujibu wa sheria sababu umetaka sasa kama kuna Mtu maisha yamemshinda aje ila asije kulalamika, hii kesi iko Mahakamani tuiachie Mahakama iamue”
Haya yote yanaonyesha jinsi Katiba Mpya ilivyo muhimu.
 
Back
Top Bottom