My Son drink water
JF-Expert Member
- Nov 30, 2016
- 4,932
- 13,306
IGP Sirro anadhani Watanzania wamesahau kutekwa kwa MO? Kwa makusudi mjadala wa nani alimteka MO na kukaa naye ndani ya siku 9 umeamka tena baada ya IGP Sirro kujigeuza mahakama na kumhukumu Mbowe kuwa anao ushahidi kuwa Mbowe ni gaidi.
IGP Sirro nataka ujue kuwa, jinai huwa haizeeki, unachokifanya kuna siku utasimama mbele ya Mahakama. Usidhani ilivyo leo ndivyo na kesho itakuwa hivyo.
Kwa sababu ugaidi wa Mbowe unaujua, tunataka kujua ni nani alimteka MO? Na ile picha ya gari la watekaji wa MO uliitoa wapi?
Na ulijuaje kama walikuwa ni wazungu,na waliwezaje kutoroka mipaka ya Tanzania?
Siyo hivyo tu, tunataka utuambie Ben Saanane yuko wapi?
Na Tuambie pia Azory Gwanda yuko wapi?
Na ni kina nani walimpiga risasi Tundu Lissu?
Na tuambie pia yuko wapi Police aliyefyatua risasi iliyomuua Aquilina? Kwa sababu risasi ya kutuliza ghasia hufyatuliwa juu,sasa ilikuwaje Police kufyatua risasi kuelekea kwenye Daladala?
IGP Sirro, hujui gharama ya kukabiliana na Dhambi,siku ukianza kulipa maovu yako na wenzako, usije sema umeonewa.
MUNGU si wa mchezo,walikuwepo kina Samuel Doe,yaliyowakuta ni majonzi na vilio siku walipolipa matendo yao.
MUNGU hawahi wala hachelewi.
Siku inakuja mtalipa tu sawa sawa na matendo yenu.
Amina...!