IGP Sirro: Hatujafikia hatua ya kufunga mipaka ya nchi kutokana na ugonjwa wa Corona

IGP Sirro: Hatujafikia hatua ya kufunga mipaka ya nchi kutokana na ugonjwa wa Corona

Polepole ameshaeleza hilo kwamba hatuwezi kuzuia utalii sababu ya Corona maana kiuchumi tutaumia ila tumeshatenga vituo vya kuhudumia wagonjwa.
 
Wenzetu wamepiga marufuku kutoka nje jimbo la Califonia Bongo ndio bado mnaruhusu watalii waje ili watumalize duh! Argentina nayo imepiga marufuku watu kutoka nje Bongo ndio kwanza leo watu walikuwa wamejazana misikitini hii imekaaje?

Tunisia pia ni ya karibuni zaidi kulazimisha raia kubakia nyumbani:

Tunisia orders lockdown

Bila lockdown hakuna haja ya kujindanganya hali yetu itakuwa pevu kweli kweli.
 
Sijui ni mtalii gani atakayekuja kwa sasa sioni ila hili janga limetuonyesha kuwa Watanzania ni Nguvu za muumba ndio zinazotulinda sio hawa viongozi ghafla na makatibu wao waenezi wa maradhi
 
Wewe umeshasema California, kwani tuwaige wao tunauhusiano nao?

xi xhua tumzgunch
 
Wenzetu wamepiga marufuku kutoka nje jimbo la Califonia Bongo ndio bado mnaruhusu watalii waje ili watumalize duh! Argentina nayo imepiga marufuku watu kutoka nje Bongo ndio kwanza leo watu walikuwa wamejazana misikitini hii imekaaje?
Na kiongozi mmoja mkubwa tu katangaza ataendesha mikutano. Akivunjwavunjwa mifupa anajua kabisa hakuna tena kwenda Ubelgiji.
 
Hili janga likiendelea huko kwenye nchi zinatoa watalii, utalii utatetereka.
Yaani hata wakiendelea kuruhusu watalii kuingia, hao watalii hawatakuwapo kwa sababu nchi zao zinakwenda kwenye total lockdown.

Muda sio mrefu kuna watu watajua hawajui.
 
Na kiongozi mmoja mkubwa tu katangaza ataendesha mikutano. Akivunjwavunjwa mifupa anajua kabisa hakuna tena kwenda Ubelgiji.
Umechagua upumbav kuwa sehemu ya maisha yako!
 
Shida wanadhani Corona inawaathiri watu wa tabaka la chini tu.
Wanasahau Corona haimjui IGP wala Waziri,wala Polepole.
 
Uzuri ni kuwa wanavyoendelea kufanya mzaha, watagundua na wao wanajiweka kwenye risk ya kupata hivyo virusi. Wamekosa maarifa hawa watu, waache tu.

Mimi binafsi nilipata symptoms za corona December mwaka jana. Nilikaa navyo weee ila bado nikaona vinaendelea kunisumbua, hasa kikohozi na kujihisi dhaifu muda wote. Nikasema hii siyo issue ya kawaida nikaamua kwenda hospitali wakachukua damu baadae wakanipa dozi moja kali sana ila hata hawakuniambia nasumbuliwa na nini. Na ilichukua zaidi ya wiki kupata nafuu. Sikuconnect dots ila nilishangaa dawa zilivyokuwa nyingi walizonipa.

Nilipoanza kupata nafuu, mshkaji wangu naye baada ya muda mfupi akaanza naye kuumwa kama nilivyoumwa mimi.

Huu ugonjwa upo na nadhani tumekuwa nao kwa muda. Sijui wangapi watakuwa wamepoteza maisha.
 
Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini Tanzania (IGP) Simon Sirro amesema jeshi hilo limejipanga imara kwenye mipaka ili kuhakikisha kwamba watu wanaoingia nchini wanafuata utaratibu na endapo wakibainika kuwa na viashiria vya virusi vya Corona basi hatua zinachukuliwa kwa mujibu wa taratibu zilizowekwa.

Akizungumza na ITV Online IGP Sirro amesema kwa sasa hakuna haja ya kufungwa kwa mipaka lakini kama kutakuwa na sababu ya moja kwa moja vyombo vya usalama vilivyopo katika mipaka vitashauri lakini kutokana na Intelijensia walizozipata hakuna tishio kubwa kiasi hicho mpaka kufikia kufungwa mipaka.

"Sasa elimu tumeshaipata kilichobaki ni sisi watanzania kutekeleza hiyo elimu ambayo tumeipata, manaake ukiipata hiyo elimu, usipoitumia hiyo elimu ukabaki kufanya mambo yako ya zamani mwisho wa siku utaangamiza jamii ya Watanzania" Alisema.


Credit: ITV

Tangu lini jukumu la kufunga mipaka likawa chini ya polisi.
 
Back
Top Bottom