IGP Sirro: Hatuna barua ya kumkamata Askofu Gwajima, utaratibu ufuatwe

IGP Sirro: Hatuna barua ya kumkamata Askofu Gwajima, utaratibu ufuatwe

kosa la Gwajima ni lipi mpaka akamatwe?

Makosa ya Askofu Gwajima ni wazi:

1. Hadharani amewatuhumu Rais na wasaidizi wake kwa rushwa.
2. Hadharani amehamasisha watu dhidi ya serikali.
3. Kwenye #2 hapo amekuwa akitumia maneno ya dharau, kejeli, kuudhi, dhidi ya Mh. Rais na serikali.

Haya yote ni makosa kisheria kwani kwa kila moja upo ushahidi wa watu waliokwisha kukamatwa, kushitakiwa na hata kuhukumiwa.

Gwajima, Sirro japo mmoja Ang'oke
 
Kwahiyo wanapo kamatwa wale wanaombambikiwa kuna maandishi rasmi ya maelekezo sio,basi tuonyeshwe maelekezo hayo ya Kamata Kamata yanayoelekezwa kwao tasafali.au ndio mwendo ya maigizo ya sang.
Uoneshwe wewe kama nani?
 
Mama samia nchi ishamshinda kila mtu kambale mpaka madiwani. Kazi ipo
 
20210818_06392422129.jpg


Nakumbuka Makonda amewahi kuwaagiza polisi kumkamata Mbowe baada ya kumtaja kwenye orodha ya madawa ya kulevya. Sirro hakusubiri maandishi. Makonda huyohuyo akaagiza Aabdul Nondo akamatwe kwa tuhuma za kujiteka. Sirro hakusubiri maandishi, licha ya kwamba yalikua maelekezo ya Mkuu wa mkoa tu. Leo Waziri katoa maelekezo anasema anasubiri maandishi?

Anyway ni barua gani Sirro alipewa kuwakamata vijana wa Chadema waliokua ibadani huko Mwanza juzi jumapili? Je Sirro alipewa barua na nani kumkamata Askofu Mwamakula na Prof.Azavel Lwaitama usiku wa manane hotelini kama majambazi na kuwaweka rumande bila hatia? Sirro alipewa barua na nani kuwakamata vijana wanaokwenda mahakamani kufuatilia kesi ya Mwenyekiti Mbowe? Why these double standards?

Credit: Malisa GJ
 
Mbona kwenye hili IGP kajibu na sio kamanda kanda maalum kama kawaida yake? Nahisi kuna kosa mahali.
 
Baada ya Waziri wa Afya Dkt.Doroth Gwajima kuagiza Jeshi la Polisi na TAKUKURU kumkamata Askofu Josephat Gwajima na kumuhoji kwa tuhuma za kupotosha juu ya Chanjo ya UVIKO-19, hatimaye Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Simon Sirro amesema wanachokisubiri sasa ni maelekezo ya maandishi kutoka kwa Waziri huyo.

"Tumeyasikia hayo maelekezo, jambo la msingi unajua maelekezo ya kiserikali mara nyingi yanakwenda kwa maandishi, tunasubiri maandishi ya kuonyesha kuna kosa gani, maanake sisi tunashughulika na makosa ya jinai, kwahiyo nasubiri maelekezo kutoka kwake alafu tutaangalia kama ni makosa ya jinai tutachukua hatua na kama tutaona ni vinginevyo tutashauri njia nyingine itumike badala ya kutumia Jeshi la Polisi"-IGP-Sirro."

Hii hakika ni double standard, kama waziri (Serikali) angeagiza akamatwe kiongozi yeyote wa upinzani kwamba amegomesha watu kupata chanjo kama anavyotuhumiwa Gwajima ni kweli Sirro na jeshi lake wangesubiri taarifa ya maandishi? Au Gwajima ni kwa sababu ni mbunge wa ccm ndiyo maana Sirro anasitasita kumkamata? Sipati picha.
View attachment 1896467
 
Wacha weeeeeh, kwa maccm wenzake Aigipi anakuwa reasonable sana, kwa upinzani angeshaonesha mihemko yake
 
Makosa ya Askofu Gwajima ni wazi:

1. Hadharani amewatuhumu Rais na wasaidizi wake kwa rushwa.
Wapi aliposema Rais amepokea rushwa?
2. Hadharani amehamasisha watu dhidi ya serikali.
Amehamashisha vile serikali ilivyopendekeza, hiari ya kuchanja ama kutokuchanja.
3. Kwenye #2 hapo amekuwa akitumia maneno ya dharau, kejeli, kuudhi, dhidi ya Mh. Rais na serikali.
Sana sana anachofanya ni kusisitiza mapendekezo ya Rais kuwa watu wanahiari ya kutochanja.
Haya yote ni makosa kisheria kwani kwa kila moja upo ushahidi wa watu waliokwisha kukamatwa, kushitakiwa na hata kuhukumiwa.

Gwajima, Sirro japo mmoja Ang'oke
Mbona wanaohamashisha kuchanja hawatuhumiwi kufanya makosa?
 
Gwajima hakamatiki, wakizubaa Jumapili ataendeleza zoezi la kupambana na chanjo ya corona, safari hii atamshughulikia Dorothy [emoji1787]
Acha waumane kisawasawa,nafurahi mimi.Kile Kimwanamke kimemuanika mwenzake lkn chenyewe kusemwa kidogo tu kinakimbilia polisi, pumbavu zake ndio maana sio kizuri.Kikomae kujibu hoja za Askofu Gwajima .
 
Back
Top Bottom