IGP Sirro, huyo ni mtoto wa nani?

Katika kikundi cha wazazi sita, wanne wameshaijadili hii kauli ya Sirro, na ni ukweli kuwa wengi hawajaipenda na imewasikitisha.

Isipokuwa kwa akina Mr and mrs privilege's kama Akilinjema na mama D ndio waliomuunga mkono afande Sirro.

Mnamlaumu sirro kwa kukumbusha wazazi umuhimu wa kulea watoto katika njia sahihi!?
Kwa akili zako hamza alijifunza kutumia silaha lini labda na familia yake ikimjua ilifanya nini???

Vitu vingine mkubali kuambiwa buana, hadi sirro kaongea ana taarifa za kutosha za makuzi ya hamza
 
Ohhoo even yule mtangulizi ana kijana sampuli hiyo hiyo even the top top lady wana kijana sampuli hiyo hiyo.

Mwambieni afute hiyo kauli aende kwa gwajima akarudishwe kwenye line
Karma is real.
Hii kitu nimeiona sana.
Unafunga watoto wakiume wa wenzio wasio na hatia magerezani, wakwako wakiume wanageuzwa nje ya magereza Tena kwa Raha zao.
 
Hajaongelea Kulea kaongelea KUZAA elewa concern ya watt

KUZAA kila mtu anazaa na anajitahidi Kulea ila mtoto nae ni binadamu kuna kipindi anashindikana. Kumlaumu ALIYEMZAA ndo alipochemka....usichanganye taarifa
 
Unajua kuwa mkopo unakuwa mkubwa kulingana na ukubwa wa mshahara?
Nakuuliza tena unaujua mshahara wa polisi?
Watu hawajui hayo mahesabu.
Kwa mshahara wa polisi mwenye cheo akichukua mkopo mkubwa sana ataishia milioni 25.
Baada ya hapo ataanza kupokea nusu mshahara kwa miaka 6.
Sasa milioni 25 unaweza kujenga lodge hadi ikamilike kweli
 
Hao watoto ni washamba wana mambo ya kizamani ya miaka 90 huko waliyokuwa wanafanya wakina kinje.
 
Yale yale aliyoyasema IGP ili kutusaidia si umtaje huyo mtoto wa kibosile ili usaidie usalama wa raia au unasubiri yatokee kama ya Hamza?
 
Sio kweli,ameua watu mara ngapi tangu azaliwe?unapomsema mzazi mwenzako inabidi utupe mifano ya watoto wako uliowalea vizuri wamefanya nini cha maana
 
Iliyoko Pasiansi? Kumbe ni hotel ya Sirro? Basi kuna ufisadi mahali, huwezi kujenga kwa mshahara wa u IGP!
Mkuu unamkumbuka Ngunguri,unamkumbuka Mkarimu, unamkumbuka Mrangi hao wote wana ukwasi wa kutisha mbona hao huwasemi, tusiwe na hasira za kumnyoshea kidole IGP kisa Hamza ndio yote hayo yatoke,hebu niambie ni kiongozi gani hapa nchini asiye na ukwasi usioeleweka ?
 
Halafu itabidi aueleze umma wa Watanzania fedha ya kujengea hiyo hotel huyo baba (mtumishi wa umma) ameipataje-pataje?

 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…