IGP Sirro: Kipindi cha kampeni nilimtafuta Tundu Lissu aje kuhojiwa lakini hakuja

IGP Sirro: Kipindi cha kampeni nilimtafuta Tundu Lissu aje kuhojiwa lakini hakuja

Kwa nini Lissu hataki kwenda kuhojiwa?
Warejeshe kwanza zile cctv ziangaliwe,waliowaamrisha walinzi wasiwepo kazini mida hiyo,ujio wa Makonda Dodoma jioni ile kabla ya tukio,na vielelezo vingine kadha wa kadha wahusika waweze kukamatwa na kuhojiwa.

Ni suala la Muda tu,watatajana wenyewe sijui watafichia sura zao wapi hawa wazee wetu. "Vyeti vya mirembe" tungeyajua wapi?
Ni swala la muda tu.

Mungu hadhihakiwi
 
Huyu kamanda Sirro asitufanye watanzania ni wajinga. Zama za kudanganyana zimepitwa na wakati.

Ni mara kadhaa sasa huyu IGP Sirro amekuwa akijibu kifedhuli anapoulizwa juu ya uchunguzi wa shambulio la risasi la mtanzania mwenzetu Tundu Lisu. Amekuwa akidai kuwa wamekosa ushirikiano tokakwa Lisu mwenyewe. Na Jana akiwa StarTV amerudia majibu kama haya.

Lisu angekuwa amekufa? Kule Hiati mbona rais kafa lkn bado uchunguzi inafanywa na watuhumiwa wanakamatwa?

Jeshi la polisi lisione aibu, liseme ukweli tu. Nani aliondoa walinzi kwenye makazi ya serikali alipokuwa anakaa Lisu? Na nani aliondoa CCTV cameras? Na kwa nn jeshi halijwahi hata kumhoji mshukiwa yeyote?

Siasa zisitugawe watanzania. IGP Sirro na wenzako siku nikiwa rais mtapata tabu!!
 
Huyu hajui anachokisema
Kwa hio tuseme lissu angekufa siku hio na uchunguzi ndio ungeishia siku hio!?...
Hivi kinachokwepwa haswa ni nini? Kwaiyo mnataka ufanyike uchunguzi pasi kuwahoji wenyewe walikawa eneo la tukio? Dereva mmemkimbiza kwa kisingizio atauawa hamtaki ahojiwe kweli?
 
Hahahaha akwambie nini wakati CCTV camera [emoji327] mlizing'oa [emoji23][emoji23][emoji23] angeanza na walinzi wa mageti kwanza
 
Hahahaha akwambie nini wakati CCTV camera [emoji327] mlizing'oa [emoji23][emoji23][emoji23] angeanza na walinzi wa mageti kwanza
Camera za nyumbani kwa Kalemani zilitolewa punde baada ya tukio.
Kumbuka nyumba ya Mbunge huyo wa Chato inatazamana na nyumba ya Lissu, ni majirani.
 
Risasi kwa lissu ni mtaji anatamani hata apigwe tena
 
IGP angestaafu tu abakie na heshima yake ya kuwa IGP
Kila kukicha Siro ana haribu. Yaani intelijensia yake naonekana ilikuwa ya mabavu. Kuua, kupoteza watu na kesi za kubambikizia.

Naona ni muda muafaka Mh. Rais amstaafishe kwa heshima ya Watanzania.

Hivi Lissu ana takiwa akatoe maelezo au polisi ndio wana takiwa watoe maelezo ya upelelezi wao? Ni nani asie jua kwamba Lissu alishambuliwa?

Ni maelezo gani wana yataka kwa Lissu kama sio wana potezea hii issue na wanajua ABC za hili shambulizi?

Shame shame, shame to Siro.
 
Wakikujibu hili naomba unitag.
Utaratibu wa kufuata mshambuliwa akiwa amefariki ni tofauti na akiwa hai ...maiti unaweza chukua simu yake ... unaweza ukaomba taarifa zake binafsi...unaweza uifanyie postmortem lakin akiwa hai huwezi pata hii access ... Lissu kama anataka kesi yake itatuliwe inabidi ashikiane na polisi la sivyo aendelee kuitumia kama mtaji
 
Safi Sana,IGP ameupiga msumari kichwani, lissu ni tapeli saana
 
Utaratibu wa kufuata mshambuliwa akiwa amefariki ni tofauti na akiwa hai ...maiti unaweza chukua simu yake ... unaweza ukaomba taarifa zake binafsi...unaweza uifanyie postmortem lakin akiwa hai huwezi pata hii access ... Lissu kama anataka kesi yake itatuliwe inabidi ashikiane na polisi la sivyo aendelee kuitumia kama mtaji
Yani ndiyo sirro anamuita Lissu kituoni umuhoji katikati ya ratiba za mikutano ya kampeni za urais??

Siku zote hizo Lissu alizoomba kuhojiwa hata kwa video call mlikua wapi???
 
Sirro tunza heshima yako
Uchunguzi wa Jinai haukomi kwa kumpigia simu shahidi halafu asitokee. Jeshi la Polisi lina taratibu za kisheria za kufuata mpaka shahidi ajitokeze la sivyo ni kosa la jinai
 
Back
Top Bottom