IGP Sirro: Polisi hatuna taarifa kuwa Tundu Lissu ametishiwa kuuawa

IGP Sirro: Polisi hatuna taarifa kuwa Tundu Lissu ametishiwa kuuawa

Sky Eclat

JF-Expert Member
Joined
Oct 17, 2012
Posts
58,636
Reaction score
220,438
POLISI HATUNA TAARIFA KUWA LISSU AMETISHIWA KUUAWA​

Jeshi la Polisi limesema halina taarifa ya madai yaliyotolewa na Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA, Tundu Lissu, kuwa ametishiwa kuuawa na watu ambao hawajajitambulisha.

Akizungumza na Gazeti ya Mwananchi, Mkuu wa Jeshi la Polisi, IGP Simon Sirro amesema kuwa mwanasiasa huyo hajatoa taarifa hiyo kwenye chombo cha usalama na wala hawana taarifa za yeye kukimbilia kwenye Ubalozi wa Ujerumani jijini Dar es Salaaam.

"Mimi nasikia kama ulivyosikia wewe. Muulize mwenyewe kama ameshawasiliana na chombo chochote cha usalama kama kuna shida hiyo," IGP Sirro ameliambia gazeti hilo.

Sirro ameongeza kuwa wamesikia kwamba mwanasiasa huyo aliyegombea Urais wa Tanzania anahojiwa na Ubalozi wa Ujerumani, lakini hajasema chochote.

"Yeye anajua nipo, haji kunijulisha. Tunakutana naye katika magazeti. Si anatafuta hifadhi, sisi tutasemaje?"

Akizungumza na vyombo vya habari kwa nyakati tofauti Lissu amesema aliomba hifadhi ubalozini hapo tangu Jumatatu na kwamba ataendelea kukaa humo hadi hapo usalama wake utakapoimarika.

Usipitwe na habari na matukio like page yetu
 
Duhhhhh!
Basi sawa, ngoja tusubiri kusikia pia ubalozi wa Ujerumani pia watasema nini.
 
Mwana wa Adam, kaka yako yuko wapi? Hili swali Mungu alimuuliza Kaini baada ya kumuua kaka yake Habili.

Kaini akajibu kama ambavyo hawa washenzi kwa jeuri wanajibu leo hii. Kaini alimjibu Mungu, "Sijui, mimi ni mlinzi wa ndugu yangu?"
 
Awape nani taarifa, na nyie POLICCM ndio mliomuua kwa risasi nyingi dodoma, ikashindikana,. na sasa mama SAMIA amewambia zisizidi risasi tatu kummaliza vinginevyo mtafutwa kazi.

Tuueni tu ili Magufuli afurahi haina shida.
 
Awaambie nini wakati tukkio la kushambuliwa kwake hawajawahi kulichuunguza hadi leo any way ninikitabadilika akisha waambia just nonsense.
 
Mimi hainiingii akilini kuwa lissu anatishiwa kuuawa,hao wauaji wakulikuwa wapi kumtishia au hata kumuua kabisa wakati wa kampeni hadi wasubiri muda huu ambapo mtu mwenyewe ana mawazo na stress nyingi.

Mimi naamini ni wafuasi wa chama cha CHADEMA ambao aliwaaminisha kuwa anao uwezo wa kuchukua nchi na kukipatia chama wabunge wengi matokeo yake kakididimiza chama, sasa hawa wafuasi kindaki ndaki wanahasira juu yake na ndo hao wanataka roho yake.
 
Awape nani taarifa, na nyie POLICCM ndio mliomuua kwa risasi nyingi dodoma, ikashindikana,. na sasa mama SAMIA amewambia zisizidi risasi tatu kummaliza vinginevyo mtafutwa kazi.

Tuueni tu ili Magufuli afurahi haina shida.
Halafu unakuta mtu aliyetoa maagizo ya kufanya huo uovu,anaingia kanisani like a saint na kushiriki sacrament kabisa!
 
Ana kesi kaambiwa aripoti mahakamani tarehe 30 mwezi huu Sasa kaona Amsterdam hataki hizi kesi anataka kesi kuhusu kuibiwa kura kaona aingie mitini.

Hata siku anaenda ubelgiji apelekwe na gari la balozi.
 
Mwana wa Adam, kaka yako yuko wapi? Hili swali Mungu alimuuliza Kaini baada ya kumuua kaka yake Habili.

Kaini akajibu kama ambavyo hawa washenzi kwa jeuri wanajibu leo hii. Kaini alimjibu Mungu, "Sijui, mimi ni mlinzi wa ndugu yangu?".
Mkuu Jeshi letu la Polisi linasikitisha mno ukilitafakari kwa makini. Wamekuwa wakitumika na Wanasiasa wa Upande wa Watawala kama Walinzi wao Binafsi. Na kuwatendea unyama wowote ule wale wote wasiowafirahisha Watawala. Wamesahau kuwa kila Binadamu ana Haki ya Kuishi.
 
Mimi hainiingii akilini kuwa lissu anatishiwa kuuawa,hao wauaji wakulikuwa wapi kumtishia au hata kumuua kabisa wakati wa kampeni hadi wasubiri muda huu ambapo mtu mwenyewe ana mawazo na stress nyingi,

Mimi naamini ni wafuasi wa chama cha CHADEMA ambao aliwaaminisha kuwa anao uwezo wa kuchukua nchi na kukipatia chama wabunge wengi matokeo yake kakididimiza chama,sasa hawa wafuasi kindaki ndaki wanahasira juu yake na ndo hao wanataka roho yake.
Huo ndio ukweli, pia Mbowe nae hamtaki kasikia anataka uenyekiti hivyo lazima afukuzwe kama Zitto chadema au akimbie kama sumaye, Mwambe, au afe Kama Wangwe. Hai wote waliutaka uenyekiti.
 
Back
Top Bottom