IGP Wambura ameteuliwa ili Viongozi waishi vizuri?

IGP Wambura ameteuliwa ili Viongozi waishi vizuri?

mirindimo

JF-Expert Member
Joined
Nov 2, 2009
Posts
901
Reaction score
1,742
Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini (IGP) Camillus Wambura, ameahidi kushughulika na yeyote ambaye atakuwa na vitendo vyovyote ambavyo ni kinyume na maadili na kinyume na matendo mema ya Watanzania.

“Nitoe rai kwa mtu yeyote ambaye anadhani anaweza akaleta aina yeyote ya vitendo vya uvunjifu wa amani asijaribu atulie tuache viongozi wetu waishi vizuri lakini tutashughulika na yeyote ambaye atakuwa na vitendo vyovyote vitakavyokwenda kinyume na maadili”

- Amesema IGP Camillus Wambura.

========

Mama SSH hata kama ulikua na hasira hapa ungetufikiria watoto wako aisee maisha yatakua very magumu

 
Vibaka na mateja mshaanza kujam..ba jam.ba kabla kazi haijaanza.

Huku kamanda Murilo, kule IGP Wambura big combination.
 
Polisi wa nchi za wenzetu wapo kwa ajili ya kulinda raia na mali zao. Sisi wa kwetu jukumu lao kubwa ni kuwalinda viongozi wa ccm waliopo madarakani na pia kukilinda chama chao ili kibakie madarakani kizazi na kizazi.

Wala haishangaizi kuona wakiitwa na baadhi ya watu; policcm.
 
Bora huyo amekiri ukweli hadharani, viongozi wa jeshi la polisi kipaombele chao ni viongozi maana ndio wanawachagua wawe na hizo nafasi.

Yaani hata wasipofanya kazi kwa mujibu wa majukumu yao ya kisheria, ili mradi waliowachagua wanaishi kwa raha kwao sio tatizo.
 
Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini (IGP) Camillus Wambura, ameahidi kushughulika na yeyote ambaye atakuwa na vitendo vyovyote ambavyo ni kinyume na maadili na kinyume na matendo mema ya Watanzania...
Viongozi wa mtumishi wa umma yeyote yule anayefanya kazi ndani ya JMT ni Watanzania wote ambao Katiba ya JMT imempa mtumishi huyo mamlaka na majukumu ya kuwatumikia
 
Sasa mnaopinga onyo la IGP mna ajenda ya kuumiza viongozi kwani? Ni sahihi viongozi wetu wanahitaji utulivu ili watumikie taifa na sisi raia wao! Ni nini shida hapo? 🤷‍♂️🤷‍♂️🤷‍♂️
 
Sasa mnaopinga onyo la IGP mna ajenda ya kuumiza viongozi kwani? Ni sahihi viongozi wetu wanahitaji utulivu ili watumikie taifa na sisi raia wao! Ni nini shida hapo? [emoji2369][emoji2369][emoji2369]
Mbowe tuliii, hakuna cha ukuta hapo.
 
Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini (IGP) Camillus Wambura, ameahidi kushughulika na yeyote ambaye atakuwa na vitendo vyovyote ambavyo ni kinyume na maadili na kinyume na matendo mema ya Watanzania...
Hawa ndio SSH anataka kulindwa ili awauzie wajomba wa arabuni nchi! Ahsante Wambura kwa kukubali cheo hicho kikubwa.

Kuanzia leo OBC ruksa kupakia twiga kwenye madege yenu. Kateni mgao kwa viongozi tu hakuna wa kuwasumbua
 
Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini (IGP) Camillus Wambura, ameahidi kushughulika na yeyote ambaye atakuwa na vitendo vyovyote ambavyo ni kinyume na maadili na kinyume na matendo mema ya Watanzania...
Yeye jukumu lake kuu ni kumlinda aliyemteua na si vinginevyo.

Hivi kazi ya jeshi la polisi ni kuwatisha wananchi? Ninaamini Tanzania si nchi ya wahalifu, je, huu ni ulevi wa madaraka?
 
Back
Top Bottom