IGP Wambura ameteuliwa ili Viongozi waishi vizuri?

!!
 
Hayo maneno naona kaongea kama hakujiandaa, course aliongea kwa kutafuta maneno yanayofuata ndg IJP.
 
Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini (IGP) Camillus Wambura, ameahidi kushughulika na yeyote ambaye atakuwa na vitendo vyovyote ambavyo ni kinyume na maadili na kinyume na matendo mema ya Watanzania
Huyo IGP mbona mwepesi tu sidhani kama niya yake ni kupambana na wazalendo wa tz dhidi ya wahuni ...kama ni hivyo basi kazi anayo tena kubwa sana
 
Duuh sidhani kama kuwa kiongozi ni kuishi vizuri.

Kiongozi ni mtumishi wa wananchi.

Hii mindset ndio inaharibu mambo mengi sana hapa nchini.

Ww ndio umesema. Ingekuwa uongozi hapa kwetu ni kutumikia watu na sio kuishi vizuri, usingeona wizi, mauji, ukatali na uhayawani wakati wa uchaguzi. Lakini kwakuwa uongozi ni sehemu ya kula πŸ¦† ndio maana unaona ule uhayawani wakati wa chaguzi zetu.
 
Nanukuu mstari mmoja unasema ,"Tuache viongozi wetu waishi vizuri" swali je kuna tatizo kwa viongozi nyuma ya pazia? Au viongozi na wananchi wa kawaida?
Namnukuu tena
#HABARI Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini (IGP) Camillus Wambura, ameahidi kushughulika na yeyote ambaye atakuwa na vitendo vyovyote ambavyo ni kinyume na maadili na kinyume na matendo mema ya Watanzania.

β€œNitoe rai kwa mtu yeyote ambaye anadhani anaweza akaleta aina yeyote ya vitendo vya uvunjifu wa amani asijaribu atulie tuache viongozi wetu waishi vizuri lakini tutashughulika na yeyote ambaye atakuwa na vitendo vyovyote vitakavyokwenda kinyume na maadili” amesema IGP Camillus Wambura.
 
Naona wanaharakati uchwara, kila mtu kaishapata njia ya kuanzisha uzi kupitia kauli ya IGP mpya. Neno viongozi lina maana pana, hata wewe na mimi na wengine ni viongozi pia kwa wale wa chini yetu tunaowaongoza. Lisu nae ni kiongozi maana ana watu wanaowaongoza ndani ya chama chake.

@Moderators njooni muunganishe huu uzi kule zilipo nyuzi zingine zinazo hoji kauli ya IGP mpya.
 
CCM ina laana,badala ya kuteua watu wenye weledi kama hawa, wanateua Mapaka!πŸ’πŸ’πŸ’
Your browser is not able to display this video.
 
Mbona umepanic mapema na ndo kwanza mechi imeanza dkt ya 1 usimlishe maneno IGP.
Upuuzi mtupu, nyie ndio mnaofanya hili jukwaa lionekane ni la vilaza. Ukiingia upande wa JF kwa upande wa wakenya hauwezi kukuta thread za kijinga jinga hivi.
 
Upuuzi mtupu, nyie ndio mnaofanya hili jukwaa lionekane ni la vilaza. Ukiingia upande wa JF kwa upande wa wakenya hauwezi kukuta thread za kijinga jinga hivi.
Kilichokuuma nini bando yangu simu yangu wazo langu na wewe anzisha uzi wako tatizo mnataka tuishi katika akili zenuπŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€ yaani mwenye akili hutoa hoja siyo matusi na kashfa heri yako wewe usiwe kilaza kama jambo dogo kama hili pia unashindwa kung'amua ngoja nikae kimya.
 
Ilo ni onyo kwa Mbowe na wafuasi wake,rejea kesi yake ya ugaidi kuwa alipanga kuwadhuru viongozi wa kitaifa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…