Watu weusi tuna taabu!! Tusipojiegesha kwa Wayahudi utasikia Misri ya Kale tulikuwa sisi!!
Tulivyo maboya, upande mwingine tunaamini sisi ni watoto wa Ibrahim! Na kuhitimisha uboya kama sio ukila.za wetu hapo hapo tunakubali, Ishmael ni mtoto wa Ibrahim na huyu Ishmael mama ake alitokea Misri! Na kutokana na unduze huo huo tulionao tunakubali Ishmael ndie chimbuko la Waarabu-- kwamba mtoto wa mama Mmisri ndie chimbuko la Waarabu na hivyo kuwa na uwezekano mkubwa kwamba mama ake Ishmael nae alikuwa Mwarabu wa Misri!
Sasa hao Waarabu walienda wapi hadi Misri ikageuka kuwa ya Wamatumbi akina Firauni?! Mbona hawa Wamatumbi hatusikii kwamba ndio wanadamu wa kale nchi jirani na Misri?!
Miafrika bhana... kusikia Wayahudi eti ma-genius na yenyewe inataka kujinasibisha na Wayahudi! Kusikia Mzungu na jeuri yake yote hadi leo hafahamu mapiramidi yalijengwaje... Wamatumbi hao; kama mkojo wa asubuhi kwamba eti mapiramidi yalijengwa na mababu zao!!
Ajabu ni kwamba, hawafananii na chochote na hao kimaarifa! Japo miaka elfu kadhaa ishapita, ndo kwanza wengine tunajiita Tanzania ya Viwanda lakini viwanda vyenyewe ni vile ambavyo Ulaya vilikuwepo miaka 500 iliyopita!
Waarabu huwaita wamisri Wajomba na mama wadogo kwani Mama yake Ishmael "Hajri" alikuwa mmisri yaan Mtu kutoka Afrika. Ndio maana Baada ya Hajri kufukuzwa na Mke mkubwa Sarah aliamua kurudi kwao misri lakini akiwa njian akarudishwa na Malaika, stori iishie hapo.
Ishamael pia alizaa watoto kumi na mbili tofauti na ndugu yake Isaka aliyechelewa kupata watoto na kupata watoto mapacha uzeeni(Yakobo ambaye ndiye Israel na Esau ambaye ndiye Baba wa Waedomu.
Waafrika ni race muhimu katika ulimwengu huu kwani ilianza zamani Sana kabla ya uwepo wa wazungu.
Ikumbukwe kuwa Waafrika ni kizazi cha pili cha Nuhu yaani watoto wa Hamu ambaye inasemekana alikuwa na ngozi nyeusi.
Hamu ndiye aliyewazaa kina Kanaani, Misri na Kushi n.k.
Kutokana na Laana aliyoitoa Nuhu kwa Hamu baada ya Hamu kumchungulia.
Kilembwe cha Nuhu yaan mjukuu wa Hamu aitwaye Nimrodi akajenga ufalme katika nchi ya Shinari, Ninawi na bonde la ashuri(nchi ya uzuri) kwa sasa ni Iran na Iraq. Akajaribu kuvunja ile laana ya Babu yake kwa kuwatumikisha watoto wa Shemu na Yafeth ambao ni ndugu zake Hamu aliyebabu yake.
Jambo lile lilipelekea watu kukimbia utawala wa Nimrodi. Walikimbia Magharibi ambayo kwa sasa ni Ulaya na Mashariki ambayo ni Nchi za China, Japani kwa aina zao.
Nimrod aliwaneemesha ukoo wake yaani watoto wa Hamu ambao ni Wamisri, Wakushi, wakanaani kwa jamii zao jambo lililoleta chuki kwa koo zilizokimbia ambazo ndio mataifa ya Leo yanayoichukia Afrika.
Historia ni ndefu Sana na yaliyofichwa ni mengi