Ijue Historia ya Firauni na uongo aliozushiwa

Poa ndugu, nimekucheki. Sasa, ukilielewa kindakindaki hilo swali; utaweza kwenda sambamba na hoja za hapa. Ila usijibu kirahisi, liwazie hilo swali ktk nyanja zote? Mfano, ungejenga daraja pasipo na mto wala maporomoko, kivuko nk. Jibu hiyo kazi, kisayansi, kijiografia, kiuchumi, kijamii, kisiasa, kiukweli, na kivyovyote vile. Jibu.
 
kumbe Yesu alikuaa msukuma kwa asili? Ngwadila
 
Yaani nilitegemea utapinga hizo point! Kumbe dawa imeanza kukuingia.
 
Yaani nilitegemea utapinga hizo point! Kumbe dawa imeanza kukuingia.
Dawa ipi hiyo ndugu?!?!? Wenzako tuliuachia ubongo ukawa huru toka vifungo tulolazimishwa kuvibeba tu vile tumezaliwa na wazazi hawa. Tukawa huru kuzitafuta kweli kokote, tumepitia mengi..... Na bado tunaendelea.. dawa ipi hiyo?

Ungejibu hilo swali ungepata concept yangu, najua umeshalijibu moyoni hivyo umeshaipata. Hongera, hautaniuliza tena kwanini Morogoro mjini halijengwi daraja kubwa kama la kigamboni.
 
Katika yote niliyoyataja kama maendeleo umeona Daraja tu?
 
Katika yote niliyoyataja kama maendeleo umeona Daraja tu?
Nawe macho yako yamekuonesha daraja hapo, sasa mm hata sijataja neno daraja, we ndo umesoma hivyo tu. Tofauti zetu za kuelewa inaanzia hapo. Ukishaanza kuwa na uelewa utanifatilia.
 
Je hao uliwataja miili yao ipo hadi Leo
 
Waarabu huwaita wamisri Wajomba na mama wadogo kwani Mama yake Ishmael "Hajri" alikuwa mmisri yaan Mtu kutoka Afrika. Ndio maana Baada ya Hajri kufukuzwa na Mke mkubwa Sarah aliamua kurudi kwao misri lakini akiwa njian akarudishwa na Malaika, stori iishie hapo.

Ishamael pia alizaa watoto kumi na mbili tofauti na ndugu yake Isaka aliyechelewa kupata watoto na kupata watoto mapacha uzeeni(Yakobo ambaye ndiye Israel na Esau ambaye ndiye Baba wa Waedomu.

Waafrika ni race muhimu katika ulimwengu huu kwani ilianza zamani Sana kabla ya uwepo wa wazungu.

Ikumbukwe kuwa Waafrika ni kizazi cha pili cha Nuhu yaani watoto wa Hamu ambaye inasemekana alikuwa na ngozi nyeusi.
Hamu ndiye aliyewazaa kina Kanaani, Misri na Kushi n.k.

Kutokana na Laana aliyoitoa Nuhu kwa Hamu baada ya Hamu kumchungulia.
Kilembwe cha Nuhu yaan mjukuu wa Hamu aitwaye Nimrodi akajenga ufalme katika nchi ya Shinari, Ninawi na bonde la ashuri(nchi ya uzuri) kwa sasa ni Iran na Iraq. Akajaribu kuvunja ile laana ya Babu yake kwa kuwatumikisha watoto wa Shemu na Yafeth ambao ni ndugu zake Hamu aliyebabu yake.

Jambo lile lilipelekea watu kukimbia utawala wa Nimrodi. Walikimbia Magharibi ambayo kwa sasa ni Ulaya na Mashariki ambayo ni Nchi za China, Japani kwa aina zao.

Nimrod aliwaneemesha ukoo wake yaani watoto wa Hamu ambao ni Wamisri, Wakushi, wakanaani kwa jamii zao jambo lililoleta chuki kwa koo zilizokimbia ambazo ndio mataifa ya Leo yanayoichukia Afrika.

Historia ni ndefu Sana na yaliyofichwa ni mengi
 
Kama tunapinga na habari za farao zilizo katika quran tukufu Mimi naomba majibu ya maswali yafuatayo.
1 Kama mwili wake ulionekana miaka ya 1899,je mtume Mohammad(saw)alizifahamu vipi habari za farao?
2Ni kiashiria gani kilimjulisha kuwa kuna mtu ambaye ni faraho aliishi misri na mwili haujaharibika hadi wakati wake na pia mwili huo hautahalibika hata baada ya kufa kwake?
3Je tukiacha Quran ni kitabu gani ambacho kimeandika habari za faraho kuhusiana na kufa kwake na mwili kuhufadhiwa hadi Leo(weka link tusome).
4Wakati Quran inasema mwili wake hautahalibika hadi siku ya mwisho.mwandishi alijua kuwa hadi miaka hii ungekuwa haujaoza?.Naomba majibu ya maswali yangu
 
Hii ni zaidi ya elimu mkuu.
 
Hii ni zaidi ya elimu mkuu.
Ni kweli mkuu.

Mambo ni mengi Sana.
Elimu yote duniani imeanzia Afrika.

Hapo zaman Misri ilikuwa ndio kitovu cha Mafundisho ya aina mbalimbali.

Nimrodi ndiye mtu wa Mwanzoni kuleta mabadiliko katika ulimwengu huu baada ya gharika.
 
Mtume amezaliwa na kukuta elimu zote zipo, na hata ktk utawala wake ukristo na uyahudi ulikuwepo. Halafu si nguvu za kiungu tu ziwawezeshao wanadamu kujua yaliyo juu ya uwezo wao. Huku kuna kibibi kikipandisha mash......huwa kanaongea lugha zote za kigeni haswa kiarabu. Hajawahi pita skuli hata chembe.
Nilikuwa napita tu.
 
Sasa kama mtume alizaliwa akazikuta hizo elimu.ni kitabu gani kiliandika habari za faraho kabla ya Quran (ni mingi hadi mtume kazaliwa)
 
Ni kweli mkuu.

Mambo ni mengi Sana.
Elimu yote duniani imeanzia Afrika.

Hapo zaman Misri ilikuwa ndio kitovu cha Mafundisho ya aina mbalimbali.

Nimrodi ndiye mtu wa Mwanzoni kuleta mabadiliko katika ulimwengu huu baada ya gharika.
Wa dogon wenyewe wanakubali walitoka misri, hadi leo wako na dini zao, elimu zao na teknolojia zao za ujenzi kama misri ya kale,,, sijui hata wanaolipinga hili wanapingaje?
 
Unajua historia lakini hata ya huyo Mtume Mkuu.
Isiwe ni wale wakuhadithiwa tuu bila kusoma mwwnyewe
 
Wewe kweli tutusa loo
 
Sasa kama mtume alizaliwa akazikuta hizo elimu.ni kitabu gani kiliandika habari za faraho kabla ya Quran (ni mingi hadi mtume kazaliwa)
Vichwani mwa wamisri wenyewe habari hizo zilishawatoka au? Hata kisipokuwepo, fasihi na historia huifadhiwa hata kichwani.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…