Ijue Jamhuri ya Watu wa SOGODO, Kinondoni

Ijue Jamhuri ya Watu wa SOGODO, Kinondoni

Chaukucha waliwafanyia watu umafia sana...
Walikuwa kama wameshindikana
Tukio moja wililifanya walimpora dem mmja hadi wakambaka..ilibdi viongz wa ilala wakae kikao
Cha chinichini wapange nmna ya kuwatuliza

Alikuja tafutwa mafia mmja wa zamani(rtd)
Smbdy m--nyga.....alipewa baraka zote
Jamaa aliwafagia wote,kmya kmya
Ndipo kipande kile kikaja kutulia

Unajua kuna watu wanajifanya wahuni,wakabaji
Kumbe kuna raia wapo wanawacheki wanawaona kama mafala,siku raia wakiamua
Ohooo ni nomaa

Ova
Walikuja toleo jipya sema uhuni wao ukawa wa chini chini na mbunge zungu akawasaidia kuanzisha timu ya mpira hapo ndo alicheza kama pele,
 
Si unajua watemi,anaweza chukulia sim
Cheni,pesa 😂😂😂

Utemi mambo ya kizamani,sahv kila raia ana fascination zake unaweza muingia akakufanyia
Ndivyo sivyo

Ova
Dah masela walimuua kwa tuhuma za wizi aisee.
 
Madawa yamewalostisha vijana wengi sana
Kuna mwana mmoja alikuwa anaitwa lusekelo
Alikuwa mbavu sana sema alikuwa anatumia madawa,ila anamiguvu akikupa loba hutoki
Sasa mm lusekelo namjua mpaka familia yake
Yote alafu unafikiri familia yake ilikuwa nashida
Mzee wake alikuwa na miradi,mashamba sema yeye sasa
Sasa kuna bar moja pale kota manyanya,kino shule inaitwa kwa ligu akipita alikuwa na style kama za dibo yule😂😂😂😂
Akiona mtu kavaa cheni saa anakuambia vua
Sema naye mabaharia alikuwa anawajua hawavusi
Jamaa madawa yalimpelekesha sana
Kuna wakati akapelekwaga China huko
Akaishia kupigwa nyundo

Ova
 
Dah masela walimuua kwa tuhuma za wizi aisee.
Raia hawafai mzee
Zamani kulikuwa na bonding mmja anaitwa Paul siza,wakati huo vijanq tunasafirisafiri ukirudi unangaa cheni shingoni,chini raba kali
Yeye siza alikuwa analinda langata pale
Ukienda chooni anakuja nyuma yako
Anakugusa Bega ukiegeuka kitasa anakupa
😂😂😂
Sema uzuri wengine ule alwatan ulikuwepo
Kuna siku nko mtungi nko chooni kuchek nyuma siza..ahh nkamwambia mjomba vepe hata mm tena😂😂😂akacheka sana
Siza alipoona kukaba hakumfai akaingia robbery
Kna siku walienda iba mahali raia waliwagumia
Walipiga hadi kuuaaa
Ila naye alishaonywaaa

Siku zote nasema usicheze na raia au kuwachukulia mafala siku wakikuamulia hutoki

Ova
 
Kwanza wengi wanatumia madawa ya kulevya, kula kwao shida, hawawezi show bila kutumia visilaha uchwara kama viwembe n.k., ukimtaitisha mmoja au wawili unawakalisha fresh tu ujanja wao wawe mtu mob.
Wahuni wengi hutumia silaha
Visu nk hawana muda wa kutumia mikono
Ushawahi ona mtu kabla ya kukabwa anaoneshwa visu vilivyokuwa ndani ya jacket

Ova
 
Kwa wakongwe kama Mshana Jr, mitaa ya Dizonga anainyaka vyema, kwani kakaa huko hadi pale alipohahamishwa na jini lililo mnasa vibao akitaka kulinanilihiiii kwenye nyumba ya wageni, akaona isiwe taabu, akahamia Masaki.

Sogodo ni eneo linalopatikana Mwananyamala Bwawani, nyuma ya mahakama ya Kinondoni, kanisa la KKKT Kinondoni, linasambaa hadi jirani na kwa Pawa, baba yake Jaki, alikuwa baunsa wa Billicanas Club Zama zile za kale.

Sogodo Empire, ilikuwa na watu wa hatari, watu wa Shari, wagomvi, watemi, waliojikataa, ambao wako tayari kwa lolote.

Watu wa jamhuri hiii walikuwa ni tishio kiasi kwamba walikuwa na mahakama yao, polisi wao na mamlaka yao wenyewe.

Ukiiba unapelekwa kwa Pawa, Pawa anakusikiliza mhalifu na washitaka wako, baada ya hapo anatoa hukumu.

Hukumu ikitekelezwa hamna kupelekana Polisi wala Nini. Kesi imeisha hiyo.

Sogodo Empire waliishi hivyo kwa miaka mingi.
Sisi watoto waMwananyamala Msisiri B kwa mudi machips tuliwaogopa sana vijana wa sogodo, kwa diwani Songoro mnyonge, ilikuwa balaa na hatujawahi kumkubali mwanaume yeyote wa pale.
 
Back
Top Bottom