Zulu man
JF-Expert Member
- Nov 28, 2020
- 6,084
- 15,998
Unataka kusema wameachwa kwenye mataa wamepanick?Nimegundua huu uzi wa wakuja
Mkorofi sana aiseeh
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Unataka kusema wameachwa kwenye mataa wamepanick?Nimegundua huu uzi wa wakuja
Ukitoa hilo hamna lingineUnataka kusema wameachwa kwenye mataa wamepanick?
Mkorofi sana aiseeh
Lazima tuwakwepe huku sio mbeya mchele kilo ukimsalimia mtu vizuri anakubless tuBwana ni kweli kwanza najua unanilenga mm shida moja WA mikoani wanakaa Sana mtu anamaliza wiki 3,yupo tu,jamaa ku husu msosi hata sikumoja hajiongezi mm huwa nawakwepa
Amtafute mjomba wake wa chanika aendeMkuuu Fanya ufikie hata kwa mjomba wako maana sisi huku tunapanga chumba kimoja bei 200k then wewe anaforce kuja kuishi hapo usilazimishe mambo
Mim nmekaa na mtu hanisaidii chchte ndani hata kufua nguoz ake hawezi alikua analala sebuleni me naondoka namuacha anaamka sa tano. Bills ni kubwa kinyama maji nilipe 25 umeme elf 15.Marafiki wa Dar mara nyingi wanapoongea na washkaji zao wa mikoani waliosoma nao vyuoni au labda walikua udogoni pamoja mikoani hujinasibu wana maisha bora sana huko Dar.
Na pia wana michongo ya kufa mtu si wanawake wala wanaume..
Sasa wanapokuja mikoani washkaji zao huwakaribisha kwa ukarimu sana,huwakuta jamaa zao wanamaisha bora,makazi bora na hata familia bora.
Ila kwa kuwa wengi wao si wazungumzaji wa maisha yao wanayoishi huko mikoani basi huwa ni SURPRISE kubwa sana kwa hawa jamaa zao wa Dar..
Sasa kimbembe kinakujaga pale hawa jamaa wa mikoani wanapokuja Dar labda kuna inshu fulani zimewaleta na kuwapigia simu washkaji zao wenyeji ambao hujitapa wazee wa mishe nyingi za hela kuja kuwapokea ...!!!!
Hapo wasela lazma walale mbele na visingizio kibao ili mradi jamaa yao asijue wanapoishi tokana na zile tambo zao za kila siku kwenye kupiga mastori nao kwenye simu
Jamaa huwaza huwaza watamlaza mgeni wapi ikiwa wanajua mgeni anavyoishi alipotoka
Jamaa huwaza watarudisha vipi lile bata mwenyeji wao alilowapa walipokuja mkoani kwa gharama zake peke yake siku zote walizokuwepo huko..na wao wakijitapa hayo ndio maisha yao ya kila siku huku Dar
Na mambo kibao..HIVYO HUONA KULIKO KUAIBIKA NA KUJULIKANA MAISHA HALISI BORA KULALA MBELE NA KUSINGIZIA AMEPATA SAFARI YA GHAFLA KIKAZI MTWARA HIVYO KACHOMOKA ASUBUHI SANA😅😅😅😅😅😅😅😅
Hamna lolote mmepigika tu na maishaKushinda siku nzima kuangalia TV,.......hapohapo unaforce ukatembezwe kariakoo, posta, ukaone daraja la ubungo na Tanzanite, hawa watu wa Dar hawawezi kuwa na huo muda, utawalaumu bure.....
Ishu sio sehemu ya kulala, ishu ni unafanya kupafahamu kwa mshkaji na pia na kampani tokana na urafiki ulioishi utotoni au vyuoni. Kumwambia mtu nlikuwepo hapo wiki kikaz mwez uliopta lazma atakulaumu ndugu yangu kwanini hujanitafuta upajue home na nini..hata nikupe kampani na nini mida ya jioniHivi mwanaume unapata wapi ujasiri wa kutembelea mkoa fulani na kutaka ufikie/ulale kwa mwanaume mwenzio?
Hebu acheni unafiki kuna thread nyingi humu wengine mnasema hamruhusu hata ndugu zenu wafikie kwemye nyumba zenu kwasababu hamuamini mtu na watoto wenu,leo tena mnalialia mmekataliwa kufikia kwa wanaume wenzenu.
[emoji23][emoji23][emoji2]Siku naenda New York kwa mara ya kwanza rafiki yangu alinitelekeza Queens bridge
Kwani lazima ujue huyo mchizi wako anapoishi? Hamna mtu mwenye muda wa kuchezea mji huu. Wewe umefikia guest house Sinza, mimi nafanyakazi vingunguti nakaa Mbagala, jioni nianze kuhangaika na madaladala nije sinza tunywe bia au nikakuoneshe ninapoishi ili iweje? Halafu wengine tunafahamiana tu sio marafiki hayo yaliishia chuo/makazini tuendelee kuonana bar tu.Ishu sio sehemu ya kulala..ishu ni unafanya kupafahamu kwa mshkaji na pia na kampani tokana na urafiki ulioishi utotoni au vyuoni..Kumwambia mtu nlikuwepo hapo wiki kikaz mwez uliopta lazma atakulaumu ndugu yangu kwanini hujanitafuta upajue home na nini..hata nikupe kampani na nini mida ya jion..
Kwa hiyo ndugu kulala ni ishu ndogo sana na ndio maana nimekwambia mtu umeanda labda kwa shughuli flan hivi mara moja..unamcheck mwanao ambaye mara kibao mnamawasiliano.
Ila mkiambiwa mwanangu niko lodge flan hapa kwenye hii shughuli natoka saa 11 tafuta eneo tulivu tuwe tunapata mojambilitatu..daah yaan mchiz lazma daily unitafute jion upate offer 😁😁😁😁😁
ila kwa nini mfiche maeneo mnayoishi..?
Asichokijua yeye ni kwamba sio kila mtu utampeleka ajue kwako.Umefanya conclusion ya kijinga sana, usichokijua dar watu wako busy. Kupotezeana muda hakuna anayetaka.
Alafu wengine mnakuja kufanya umbea, lengo ujue tu mtu anaishi vipi uanze kusambaza maneno, kama mimi kwangu sileti mtu kienyeji enyeji tutakutana bar na mabarabarani, hata nikienda mkoani huwa sihangaiki na nyumba za watu
Dunia ya kibepari hii, sasa ww bado unataka kuishi kijamaa.
Sent from my CPH2219 using JamiiForums mobile app