Ijue sababu ya marafiki wa DSM kuwakimbia na kuanzisha visingizio pale inapofika mda wa kupokea washkaji zao wa mikoani

Ijue sababu ya marafiki wa DSM kuwakimbia na kuanzisha visingizio pale inapofika mda wa kupokea washkaji zao wa mikoani

Mkuuu Fanya ufikie hata kwa mjomba wako maana sisi huku tunapanga chumba kimoja bei 200k then wewe anaforce kuja kuishi hapo usilazimishe mambo
 
Hivi mwanaume unapata wapi ujasiri wa kutembelea mkoa fulani na kutaka ufikie/ulale kwa mwanaume mwenzio?
Hebu acheni unafiki kuna thread nyingi humu wengine mnasema hamruhusu hata ndugu zenu wafikie kwemye nyumba zenu kwasababu hamuamini mtu na watoto wenu,leo tena mnalialia mmekataliwa kufikia kwa wanaume wenzenu.
 
Marafiki wa Dar mara nyingi wanapoongea na washkaji zao wa mikoani waliosoma nao vyuoni au labda walikua udogoni pamoja mikoani hujinasibu wana maisha bora sana huko Dar.

Na pia wana michongo ya kufa mtu si wanawake wala wanaume..

Sasa wanapokuja mikoani washkaji zao huwakaribisha kwa ukarimu sana,huwakuta jamaa zao wanamaisha bora,makazi bora na hata familia bora.

Ila kwa kuwa wengi wao si wazungumzaji wa maisha yao wanayoishi huko mikoani basi huwa ni SURPRISE kubwa sana kwa hawa jamaa zao wa Dar..
Sasa kimbembe kinakujaga pale hawa jamaa wa mikoani wanapokuja Dar labda kuna inshu fulani zimewaleta na kuwapigia simu washkaji zao wenyeji ambao hujitapa wazee wa mishe nyingi za hela kuja kuwapokea ...!!!!

Hapo wasela lazma walale mbele na visingizio kibao ili mradi jamaa yao asijue wanapoishi tokana na zile tambo zao za kila siku kwenye kupiga mastori nao kwenye simu

Jamaa huwaza huwaza watamlaza mgeni wapi ikiwa wanajua mgeni anavyoishi alipotoka

Jamaa huwaza watarudisha vipi lile bata mwenyeji wao alilowapa walipokuja mkoani kwa gharama zake peke yake siku zote walizokuwepo huko..na wao wakijitapa hayo ndio maisha yao ya kila siku huku Dar

Na mambo kibao..HIVYO HUONA KULIKO KUAIBIKA NA KUJULIKANA MAISHA HALISI BORA KULALA MBELE NA KUSINGIZIA AMEPATA SAFARI YA GHAFLA KIKAZI MTWARA HIVYO KACHOMOKA ASUBUHI SANA😅😅😅😅😅😅😅😅
Mim nmekaa na mtu hanisaidii chchte ndani hata kufua nguoz ake hawezi alikua analala sebuleni me naondoka namuacha anaamka sa tano. Bills ni kubwa kinyama maji nilipe 25 umeme elf 15.

Muda huo bado nikipika nyama kg moja nyingine nikiweka kweny kafrije kangu nakuta imedokolewa muda mwingine nampakulia mtoto chakula nakuta ety anaonja tena kwa mikono yake imekaa kama spanner.

Mungu anisamehe nlimtimua tu maan alinichosha kabisa nikinunua ety li jitu linakunywa maziwa ya mtoto ety anasema anapenda sana maziwa ya baridi.

Ndugu zangu usikaribishe watu ni bora wakae huko huko kwa ndugu zao sijui wapi mim nmejifunza kabisa. Sitak aiseh.

Mim saa hivi sikwepeshi kabisa Bora nikae nadg angu akikosea namuelekeza basi maishae mengine yanasonga.
 
Mimi nadhani Dar maisha yako juu sana tu, huenda ndio sababu mioyo yetu ina kutu fulani hivi. Imagine uko na watoto wawili, unaishi chumba na sebule, plus dada wa kukusaidia. Akija mgeni unamlaza wapi.

Sawa kaja, utasema alale lodge, zote ni gharama tu, ataomba umtembeze, wewe unatoka home 12 asubuhi unarudi 3usiku, huo mda unaupata wapi.
 
Hivi mwanaume unapata wapi ujasiri wa kutembelea mkoa fulani na kutaka ufikie/ulale kwa mwanaume mwenzio?
Hebu acheni unafiki kuna thread nyingi humu wengine mnasema hamruhusu hata ndugu zenu wafikie kwemye nyumba zenu kwasababu hamuamini mtu na watoto wenu,leo tena mnalialia mmekataliwa kufikia kwa wanaume wenzenu.
Ishu sio sehemu ya kulala, ishu ni unafanya kupafahamu kwa mshkaji na pia na kampani tokana na urafiki ulioishi utotoni au vyuoni. Kumwambia mtu nlikuwepo hapo wiki kikaz mwez uliopta lazma atakulaumu ndugu yangu kwanini hujanitafuta upajue home na nini..hata nikupe kampani na nini mida ya jioni

Kwa hiyo ndugu kulala ni ishu ndogo sana na ndio maana nimekwambia mtu umeanda labda kwa shughuli flan hivi mara moja, unamcheck mwanao ambaye mara kibao mnamawasiliano.

Ila mkiambiwa mwanangu niko lodge fulani hapa kwenye hii shughuli natoka saa 11 tafuta eneo tulivu tuwe tunapata mojambilitatu, daah yaani mchizi lazima daily unitafute jioni upate offer 😁😁😁😁😁 ila kwa nini mfiche maeneo mnayoishi..?
 
Umefanya conclusion ya kijinga sana, usichokijua dar watu wako busy. Kupotezeana muda hakuna anayetaka.
Alafu wengine mnakuja kufanya umbea, lengo ujue tu mtu anaishi vipi uanze kusambaza maneno, kama mimi kwangu sileti mtu kienyeji enyeji tutakutana bar na mabarabarani, hata nikienda mkoani huwa sihangaiki na nyumba za watu

Dunia ya kibepari hii, sasa ww bado unataka kuishi kijamaa.

Sent from my CPH2219 using JamiiForums mobile app
 
Ishu sio sehemu ya kulala..ishu ni unafanya kupafahamu kwa mshkaji na pia na kampani tokana na urafiki ulioishi utotoni au vyuoni..Kumwambia mtu nlikuwepo hapo wiki kikaz mwez uliopta lazma atakulaumu ndugu yangu kwanini hujanitafuta upajue home na nini..hata nikupe kampani na nini mida ya jion..

Kwa hiyo ndugu kulala ni ishu ndogo sana na ndio maana nimekwambia mtu umeanda labda kwa shughuli flan hivi mara moja..unamcheck mwanao ambaye mara kibao mnamawasiliano.
Ila mkiambiwa mwanangu niko lodge flan hapa kwenye hii shughuli natoka saa 11 tafuta eneo tulivu tuwe tunapata mojambilitatu..daah yaan mchiz lazma daily unitafute jion upate offer 😁😁😁😁😁
ila kwa nini mfiche maeneo mnayoishi..?
Kwani lazima ujue huyo mchizi wako anapoishi? Hamna mtu mwenye muda wa kuchezea mji huu. Wewe umefikia guest house Sinza, mimi nafanyakazi vingunguti nakaa Mbagala, jioni nianze kuhangaika na madaladala nije sinza tunywe bia au nikakuoneshe ninapoishi ili iweje? Halafu wengine tunafahamiana tu sio marafiki hayo yaliishia chuo/makazini tuendelee kuonana bar tu.
 
Umefanya conclusion ya kijinga sana, usichokijua dar watu wako busy. Kupotezeana muda hakuna anayetaka.
Alafu wengine mnakuja kufanya umbea, lengo ujue tu mtu anaishi vipi uanze kusambaza maneno, kama mimi kwangu sileti mtu kienyeji enyeji tutakutana bar na mabarabarani, hata nikienda mkoani huwa sihangaiki na nyumba za watu

Dunia ya kibepari hii, sasa ww bado unataka kuishi kijamaa.

Sent from my CPH2219 using JamiiForums mobile app
Asichokijua yeye ni kwamba sio kila mtu utampeleka ajue kwako.
 
Back
Top Bottom