Ijue sababu ya marafiki wa DSM kuwakimbia na kuanzisha visingizio pale inapofika mda wa kupokea washkaji zao wa mikoani

Ijue sababu ya marafiki wa DSM kuwakimbia na kuanzisha visingizio pale inapofika mda wa kupokea washkaji zao wa mikoani

Marafiki wa Dar mara nyingi wanapoongea na washkaji zao wa mikoani waliosoma nao vyuoni au labda walikua udogoni pamoja mikoani hujinasibu wana maisha bora sana huko Dar.

Na pia wana michongo ya kufa mtu si wanawake wala wanaume..

Sasa wanapokuja mikoani washkaji zao huwakaribisha kwa ukarimu sana,huwakuta jamaa zao wanamaisha bora,makazi bora na hata familia bora.

Ila kwa kuwa wengi wao si wazungumzaji wa maisha yao wanayoishi huko mikoani basi huwa ni SURPRISE kubwa sana kwa hawa jamaa zao wa Dar..
Sasa kimbembe kinakujaga pale hawa jamaa wa mikoani wanapokuja Dar labda kuna inshu fulani zimewaleta na kuwapigia simu washkaji zao wenyeji ambao hujitapa wazee wa mishe nyingi za hela kuja kuwapokea ...!!!!

Hapo wasela lazma walale mbele na visingizio kibao ili mradi jamaa yao asijue wanapoishi tokana na zile tambo zao za kila siku kwenye kupiga mastori nao kwenye simu

Jamaa huwaza huwaza watamlaza mgeni wapi ikiwa wanajua mgeni anavyoishi alipotoka

Jamaa huwaza watarudisha vipi lile bata mwenyeji wao alilowapa walipokuja mkoani kwa gharama zake peke yake siku zote walizokuwepo huko..na wao wakijitapa hayo ndio maisha yao ya kila siku huku Dar

Na mambo kibao..HIVYO HUONA KULIKO KUAIBIKA NA KUJULIKANA MAISHA HALISI BORA KULALA MBELE NA KUSINGIZIA AMEPATA SAFARI YA GHAFLA KIKAZI MTWARA HIVYO KACHOMOKA ASUBUHI SANA😅😅😅😅😅😅😅😅
Wacheni kulalama
Zama za kufikia kwa ndugu zimepitwa na wakati otherwise uwe ni mtegemezi
Unajua unasafari jipange kipesa, naulu chakula na malazi
 
Wacheni kulalama
Zama za kufikia kwa ndugu zimepitwa na wakati otherwise uwe ni mtegemezi
Unajua unasafari jipange kipesa, naulu chakula
Bro hizo ni inshu ndogo sn..kwa watu wenye kazi..
Nakupa kisa ya kwa nini nimeleta huu hii thread maana kuna tukio limetokea kwa jamaa yetu na kuna group letu marafiki tuliokuwa karibu huko vyuoni na kwenye yale mambo yetu..

Kimsingi tunapigana sana kampani kuanzia kwenye majanga mpaka kuchangiana harusi n.k

Sasa kuna mwamba mmoja wa hapo mjini kwenye mambo yetu alipigwa na presha ghafla kukimbizwa hsptl..watu wanatafuta watu wanaokaa nae au anapoishi jamaa marafik wote hakuna anaepajua na mara kibao watu kwenye mishe wanakutana nae kwenye kupiga gambe na inshu zingine..
Sasa akawa ni kusubir tu simu itakayopigwa ndio watu watoe taarifa kwamba huyu mtu yuko hsptl,simu yake ina pasword

Ndio watu kwenye group kuanza kuelezea visa km hivyo nao walivyokutana navyo kwa washkaji kibao wa huko..
Maana jamaa alimpeleka hsptl alipata shida sana na aliomba sana jamaa asije kata moto..

Hakuna mtu asie jua mazingira ya hapo Mjini,usipoenda kikazi ,utaenda kibiashara mji unapokea watu kibao,the ishu ni kwamba sehemu yenye mwenyeji rafik ni nzur sn coz kuna zile ABCD mnapeana hata unataka kuwekeza huko...km unavyokuwaga mnajadili kwenye group lenu mambo kibao ya uwekezaji kwenye maeneo husika na changamoto zake..

Lkn ishu ya na maelezo ya wachangiaji ikaja onekana washkaji wa DSM maneno mengi sana kwenye mambo ya biashara ila watu wanapotaka kujua makazi yao hutokea mazingaombwe kibao

Na sababu kubwa pia wengi wenu hujiweka kwenye high profile ya maisha..

Huwezi mtu wa dizaini ukamuamini kibwege.
 
Siku naenda New York kwa mara ya kwanza rafiki yangu alinitelekeza Queens bridge
Kwa sababu we mjinga mjinga. Kwa sisi tulioishi NY, ungeenda ubalozi mdogo wa NY ukaongea na Balozi Kenedi akupe zile floor za juu hazitumiki uwe unaishi humo wakati unajipanga. Tena ungekua unakaa Downtown NY.

Otherwise ungetafuta Mbangladesh mmoja akupe mchongo uwe Cab Driver.
 
Nilisolve hiyo ishu kibave ila jasho lilinitoka,unakuwaje Cab drivee kwenye jiji lile barabara zina lane 8 na ni mgeni haiwezekani
 
Ishu sio sehemu ya kulala..ishu ni unafanya kupafahamu kwa mshkaji na pia na kampani tokana na urafiki ulioishi utotoni au vyuoni..Kumwambia mtu nlikuwepo hapo wiki kikaz mwez uliopta lazma atakulaumu ndugu yangu kwanini hujanitafuta upajue home na nini..hata nikupe kampani na nini mida ya jion..

Kwa hiyo ndugu kulala ni ishu ndogo sana na ndio maana nimekwambia mtu umeanda labda kwa shughuli flan hivi mara moja..unamcheck mwanao ambaye mara kibao mnamawasiliano.
Ila mkiambiwa mwanangu niko lodge flan hapa kwenye hii shughuli natoka saa 11 tafuta eneo tulivu tuwe tunapata mojambilitatu..daah yaan mchiz lazma daily unitafute jion upate offer [emoji16][emoji16][emoji16][emoji16][emoji16]
ila kwa nini mfiche maeneo mnayoishi..?
Wako hivyo wapuuzi sana. Ukimwambia niko hotel fulani njoo. Faster huyo anakuja
 
Mimi nadhani Dar maisha yako juu sana tu, huenda ndio sababu mioyo yetu ina kutu flani hivi. Imagine uko na watoto wawili, unaishi chumba na sebule, plus dada wa kukusaidia. Akija mgeni unamlaza wapi.

Sawa kaja, utasema alale lodge, zote ni gharama tu, ataomba umtembeze, wewe unatoka home 12asubuhi unarudi 3usiku, huo mda unaupata wapi.
😄😄 Tatizo mkija mkoani hamsemi mnakaa kwny chumba kimoja na sebule 😄😄
 
Machalii zangu walioenda dar wameharibika sana wakipata smartphone , earphone, viatu pea mbili, suruali fupi zile wanavaa bila soksi, shati 3 na kuvaa miwan nyeusi wanakuja kunivimbia.

Kuna mmoja alirud nikampeleka sehem tukachoma nyama kilo na ugali mbili kwenye stori zake akaanza kukosoa eti dar wanajua kuchoma nyama kuliko huku, eti mara nyingi wachoma nyama wanamjua wakimuona tu huwa hatoi order wanamletea kama kawaida yake.

Alivyomaliza kula nikajisachi nikamwambia aise nimesahau hela hebu lipia alafu nakurudishia maana Nina card tu mfukon, jamaa akaanza kutoka jasho tu.
 
Marafiki wa Dar mara nyingi wanapoongea na washkaji zao wa mikoani waliosoma nao vyuoni au labda walikua udogoni pamoja mikoani hujinasibu wana maisha bora sana huko Dar.

Na pia wana michongo ya kufa mtu si wanawake wala wanaume..

Sasa wanapokuja mikoani washkaji zao huwakaribisha kwa ukarimu sana,huwakuta jamaa zao wanamaisha bora,makazi bora na hata familia bora.

Ila kwa kuwa wengi wao si wazungumzaji wa maisha yao wanayoishi huko mikoani basi huwa ni SURPRISE kubwa sana kwa hawa jamaa zao wa Dar..
Sasa kimbembe kinakujaga pale hawa jamaa wa mikoani wanapokuja Dar labda kuna inshu fulani zimewaleta na kuwapigia simu washkaji zao wenyeji ambao hujitapa wazee wa mishe nyingi za hela kuja kuwapokea ...!!!!

Hapo wasela lazma walale mbele na visingizio kibao ili mradi jamaa yao asijue wanapoishi tokana na zile tambo zao za kila siku kwenye kupiga mastori nao kwenye simu

Jamaa huwaza huwaza watamlaza mgeni wapi ikiwa wanajua mgeni anavyoishi alipotoka

Jamaa huwaza watarudisha vipi lile bata mwenyeji wao alilowapa walipokuja mkoani kwa gharama zake peke yake siku zote walizokuwepo huko..na wao wakijitapa hayo ndio maisha yao ya kila siku huku Dar

Na mambo kibao..HIVYO HUONA KULIKO KUAIBIKA NA KUJULIKANA MAISHA HALISI BORA KULALA MBELE NA KUSINGIZIA AMEPATA SAFARI YA GHAFLA KIKAZI MTWARA HIVYO KACHOMOKA ASUBUHI SANA😅😅😅😅😅😅😅😅
Jamaa umeamua kutuchana live bila chenga🤣🤣
 
Umefanya conclusion ya kijinga sana, usichokijua dar watu wako busy. Kupotezeana muda hakuna anayetaka.
Alafu wengine mnakuja kufanya umbea, lengo ujue tu mtu anaishi vipi uanze kusambaza maneno, kama mimi kwangu sileti mtu kienyeji enyeji tutakutana bar na mabarabarani, hata nikienda mkoani huwa sihangaiki na nyumba za watu

Dunia ya kibepari hii, sasa ww bado unataka kuishi kijamaa.

Sent from my CPH2219 using JamiiForums mobile app
😄😄 Watu wa Dar kila mtu hua anasema yuko bize na michongo mingi, unaweza kudhani kila mtu huku Ni bakhresa/Mo huku Ila njoo ujionee maisha Yao Sasa.
 
Back
Top Bottom