Kifurukutu
JF-Expert Member
- Aug 29, 2013
- 4,641
- 6,694
Wacheni kulalamaMarafiki wa Dar mara nyingi wanapoongea na washkaji zao wa mikoani waliosoma nao vyuoni au labda walikua udogoni pamoja mikoani hujinasibu wana maisha bora sana huko Dar.
Na pia wana michongo ya kufa mtu si wanawake wala wanaume..
Sasa wanapokuja mikoani washkaji zao huwakaribisha kwa ukarimu sana,huwakuta jamaa zao wanamaisha bora,makazi bora na hata familia bora.
Ila kwa kuwa wengi wao si wazungumzaji wa maisha yao wanayoishi huko mikoani basi huwa ni SURPRISE kubwa sana kwa hawa jamaa zao wa Dar..
Sasa kimbembe kinakujaga pale hawa jamaa wa mikoani wanapokuja Dar labda kuna inshu fulani zimewaleta na kuwapigia simu washkaji zao wenyeji ambao hujitapa wazee wa mishe nyingi za hela kuja kuwapokea ...!!!!
Hapo wasela lazma walale mbele na visingizio kibao ili mradi jamaa yao asijue wanapoishi tokana na zile tambo zao za kila siku kwenye kupiga mastori nao kwenye simu
Jamaa huwaza huwaza watamlaza mgeni wapi ikiwa wanajua mgeni anavyoishi alipotoka
Jamaa huwaza watarudisha vipi lile bata mwenyeji wao alilowapa walipokuja mkoani kwa gharama zake peke yake siku zote walizokuwepo huko..na wao wakijitapa hayo ndio maisha yao ya kila siku huku Dar
Na mambo kibao..HIVYO HUONA KULIKO KUAIBIKA NA KUJULIKANA MAISHA HALISI BORA KULALA MBELE NA KUSINGIZIA AMEPATA SAFARI YA GHAFLA KIKAZI MTWARA HIVYO KACHOMOKA ASUBUHI SANA😅😅😅😅😅😅😅😅
Zama za kufikia kwa ndugu zimepitwa na wakati otherwise uwe ni mtegemezi
Unajua unasafari jipange kipesa, naulu chakula na malazi