Sio kweli.
Mimi ninasali jumapili na ndio siku sahihi kwa wakristo sababu ni siku ya UFUFUKO WA YESU MWENYEWE, ni siku ya USHINDI, NI SIKU KUKOMBOLEWA TOKA UTUMWA DHAMBI NA MAUTI, hiyo ndio sabato ya agano jipya, sio KIVULI TENA CHA SABATO YA KWANZA JUMAMOSI, sabato ya agano la kale.
Ni kweli sabato ni jumamosi kama siku ya saba ya juma. Lakini kwa sasa tangu ufufuko wa Yesu ni kivuli cha mambo ya kale agano la kale. Kwa lugha ingine ni Unasali jumapili kama kumbukunbu ya kukombolewa toka katika utumwa wa dhambi kwa tendo la ufufuko wa Yesu siku ya kwanza ya juma jumapili, sabato ya jumamosi kama siku ya saba ya juma ilikuwa ni siku ya kumbukumbuu ya wana wa israeli kukombolewa toka utumwani misri, sasa wewe
Joann na wakristo wengine wote ni lini ulikombolewa toka utumwani misri ?, kilichofanyika ni wewe na wakristo wengine wote mlikombolewa toka katika UTUMWA WA DHAMBI NA KRISTO MWENYEWE SIKU YA KWANZA YA JUMA JUMAPILI, na hiyo ndio siku ya wewe kufanya kumbukumbu na sio jumamosi sabato ya kiyahudi kumbukumbu ya kukombolewa toka utumwani MISRI.
Ndio maana hata wayahudi haters wa yesu walipomletea habari za sabato yao aliwaambia "MIMI NDIYE HUYO BWANA WA SABATO", na mbele huko aliwaambia wanafunzi wake nisikilizeni MIMI (refer tukio la kutokewa na mabii wa kale musa na eliya kule mlimani). Na baadae baada ya yesu kupaa mbinguni wanafunzi wake walifafanua zaidi juu ya hilo na kuwaambia wayahudi na wengine waliokywa wakingangania sabato ya kale kuwa HIYO ILIKUWA NI KIVULI CHA MAMBO YAJAYO YAANI KRISTO MWENYEWE ALIYE KUFA NA KUFUFUKA KAMA ALAMA YA UKOMBOZI NA KUISHINDA MAUTI.