hakuna muda wowote uliopata kupotea tangu uumbaji ulipotokea mpaka wakati huu. Kwa hiyo mzunguko ule ule wa siku saba za juma ulioanzishwa wakati wa uumbaji ndiyo mzunguko ule ule wa siku saba za juma kwa leo ambao tunaendelea kuufuata hata kama majina ya juma yamebadilishwa kutegemeana na kalenda inayotumika!
Wakati kalenda ilipobadilishwa kutoka katika ile ya Julia kwenda kwa kalenda ya Gregori nyuma katika karne ya kumi na sita, iligundulika kwamba kalenda ya Julia ilikuwa imepungua siku 10 kutoka katika mwaka mmoja halisi. Lakini mzunguko ule ule wa siku za juma la siku saba haukubadilishwa hata kama siku kumi ziliongezwa kwa Kalenda ya Gregori. Alhamisi, Oktoba 4, 1582 katika kalenda ya Julia, ilifuatwa mara moja na Ijumaa, Oktoba 15, 1582 katika kalenda ya Gregori – hivyo, kutunza mwendelezo wa mzunguko wa juma la Jumapili kwenda Jumamosi! Lakini hata kama wengine hawataamini ukweli kwamba hakujakuwepo wakati uliopotea tangu uumbaji, Mungu anataka kabisa kuonyesha watu wake wote ni siku gani ya juma leo iliyo siku ya saba ya juma – ibada ya kweli ya Sabato ya Mungu!
Wakati Kristo alipokuwa katika dunia hii, akiwa Bwana wa Sabato, pasipo shaka alijua kabisa ni siku gani ya juma ilikuwa ni Sabato ya siku ya saba ya zamani ya uumbaji kumwabudu Mungu [siku hiyo]. Lakini kwa sababu tunatumia kalenda tofauti leo kuliko Kristo alizopata kuzitumia, ni siku ipi ya juma katika kalenda yetu ya kisasa ambapo Sabato ya siku hii ya saba huangukia? Biblia kwa wazi na moja kwa moja huwaonyesha wote watakaoona, katika matukio yanayozunguka kusulubishwa na kufufuka kwa Bwana wetu na Mwokozi Yesu kristo, kwa uhalisia ni siku ipi ya juma leo ni Sabato takatifu ya Mungu.
Biblia imeweka kumbukumbu kwamba Kristo alisulubishwa siku ya sita ya juma, au siku ya maandalizi – siku kabla ya Sabato haijatokea (angalia Marko 15:42; Luka 23:54; Yohana 19:31, 42; Mathayo 27:62), Alifufuka siku ya kwanza ya juma, au siku baada ya Sabato kuwa imepita (angalia Mathayo 28:1-8; Marko 16:1-10; Luka 24:1-8; Yohana 20:1), hivyo ikionyesha kwamba Kristo alikuwa amepumzika kaburini wakati wa siku ya saba ya Sabato. Ni maarifa yaliyo wazi kwamba Kristo alifufuka kutoka kaburini siku ya Jumapili asubuhi – ambayo wengi hurejea kama Pasaka (angalia Mdo 12:4). Tukiwa na maarifa haya ya ukweli, basi inakuwa ni rahisi kuamua kiuhalisia ni siku gani za juma katika kalenda yetu ya kisasa huendana pamoja na siku za juma hapo zamani.
Kutokana na kwamba Kristo alifufuka katika siku tunayoiita Jumapili leo, siku hii inaendana na siku ya kwanza ya juma hapo zamani – au siku baada ya Sabato kuwa imepita. Hatimaye, siku tunayoiita Jumamosi katika kalenda yetu ya kisasa, huendana na siku ya saba ya juma hapo zamani, na siku tunayoiita Ijumaa katika kalenda yetu ya kisasa huendana na siku ya sita ya juma hapo zamani – au siku ya maandalizi kabla ya Sabato kuanza! Hivyo, wote wanaotamani kufuata na kumtumikia Mungu kwa mioyo yao yote, mawazo, roho, na nguvu, kutokana na upendo kwa kile alichokwisha kukifanya na anaendelea kukifanya kwa ajili yao, wataona kuwa Sabato ya siku ya saba ya Mungu leo ni Jumamosi – siku baada ya Ijumaa, na siku kabla ya Jumapili! Hii basi inatuonyesha kwa wazi kwamba siku ya Sabato ya Mungu haijabadilishwa sehemu yake ya saba katika mzunguko wa kila juma tangu ilipofanywa takatifu wakati wa uumbaji, na wala haitabadilishwa!