Ijumaa ya leo ikukumbushe tu Sabato ni Jumamosi

Ijumaa ya leo ikukumbushe tu Sabato ni Jumamosi

MWANZO 2​

1' Hivyo ndivyo mbingu na dunia zilivyokamilika pamoja na vitu vyote vilivyomo. 2' Siku ya saba Mungu alimaliza kazi yake yote aliyofanya; siku hiyo ya saba Mungu akapumzika baada ya kazi yake yote aliyofanya. 3' Mungu akaibariki siku ya saba na kuitakasa, kwa kuwa siku hiyo Mungu alipumzika baada ya kazi yake yote ya kuumba. 4' Hivyo ndivyo mbingu na dunia zilivyoumbwa.

Jumatano kwangu ndio siku yangu ya saba, wewe jumamosi ndio siku yako ya saba, jumapili ni siku ya saba kwa watu wengine na ijumaa pia ni siku ya saba kwa jamii nyingine.

Tatizo lako liko wapi hapo?
Ni wapi kwenye maandiko ya Mungu imeandikwa kuwa siku ya saba iliitwa jumamosi??
Mungu alizipanga siku kwa mpangilio sio shagharabaghara hadi kila mtu ajipangie anavyotaka.

Maelezo aliyoyatoa alikuja kuyarudia kwa Wymayahudi ( sio kuyaanza). Na wayahudi licha ya kumkataa Yesu ila ishu ya sabato inafuatwa siku zote nahawajawahi kubadilisha na nijumamosi.

Ziko tafsiri za kiswahili kiingereza nyingi sana za Biblia ziko wazi kuwa Sabato Jumamosi, siku ya kwanza imewekea ni jumapili.

Huu sio mjadala uko wazi, ndio maana hii mada nimeiweka makusudi ijumaa kuu kbla ya sabato.
 
Hatujadili sabato ya kiyahudi.
Tunajadili Sabato ambayo Mungu aliiweka kwa ajili ya mwanadamu. Na mwanadamu wa kwanza sio myahudi no Adam na Hawa.

Maandiko usipokuwa makini yatageuka kitanzi cha kukunyongea kiroho.

Hayo mafungu yote hayana uhusiano na Sabato ya siku ya Saba ambayo Yesu alimuewekea mwanadamu.
Haya nakubali tufanye Sabato yako wewe umeitoa kwa Mungu, KUPITIA MAANDIKO MATAKATIFU BIBLIA. na kwa adamu na hawa.

Haya hao unaowaita wa sabato ya kiyahudi na kutaka kujitofautisha nao kabisa kana kwamba ni vitu viwili tofauti kabisa mnafanya WAO WALIITOA WAPI ?, WALIITOA KWENYE MAANDIKO YAPI ?
 
Kukopi sura nzima na kukuwekea humu sifikirii kama ni kitu sahihi, ndio maana hata biblia yenyewe imegawanywa katika mistariii na aya.

Hivyo iwapo umegundua makosa au unyofoaji wa vifungu na kuharibu maana ni vizuri ukanionesha nikakuelewesha
Unajua origin ya Sabath inaanzia kwenye uumbaji,angalia Kut 20:8-11,wewe umeacha huu mstari umeona tu kwenye kumb la torati ilipoongelewa na kumbolewa kutoka Misri...umewahi kujifunza kitabu Cha torati kazi yake haswa?
 
Haya nakubali tufanye Sabato yako wewe umeitoa kwa Mungu, KUPITIA MAANDIKO MATAKATIFU BIBLIA. na kwa adamu na hawa.

Haya hao unaowaita wa sabato ya kiyahudi na kutaka kujitofautisha nao kabisa kana kwamba ni vitu viwili tofauti kabisa mnafanya WAO WALIITOA WAPI ?, WALIITOA KWENYE MAANDIKO YAPI ?
Maandiko ni haya haya.
Sabato ni Jumamosi kama jumapili ilivyosiku ya kwanza ya Juma kwa Wayahudi na wakristo sio tu wa sabato.

Tatizo la dini ya kiyahudi wao hawamuamini Yesu. Na sio wayahudi wote. Maana myahudi Paulo alikuwa anasali siku ya sabato huku akimuamini Yesu.

Maisha ni kuchagua. Unaweza kuchagua Jumatano kwa kukerwa na Mungu kuweka Jumamosi ila kila uamuzi utasimama mbele ya kitu cha Hukumu ijulikane nani anapaswa kutiiwa Mungu mweza wa yote au ajili zako mkuu
 
Unajua origin ya Sabath inaanzia kwenye uumbaji,angalia Kut 20:8-11,wewe umeacha huu mstari umeona tu kwenye kumb la torati ilipoongelewa na kumbolewa kutoka Misri...umewahi kujifunza kitabu Cha torati kazi yake haswa?
Origin ya sabato Kwa Mujibu wa Yesu aliyemuumba mwanadamu Ni siku mwanadamu anaumbwa kesho yake.

'Sabato ilifanyika kwa ajili ya Mwanadamu.

Ingekuwa vinginevyo wiki ingeishia ijumaa tu.
 
Mliofungwa kwenye kifungo cha kuabudu siku Fulani tuu Mungu awasaidie, haiitaji PhD kuelewa kwamba Mungu hataki Wala haitaji kuabudiwa kwenye hiyo siku unayoitaka wewe na wenzio ambao mnataka iwe hivyo,,,,,, Mungu anatamani wanaomwabudu wamuabudu katika mienendo Yao yote yaani Kila dakika Kila saa Kila wakati wewe umwabudu na kumuishia Mungu sio usubiri hadi jumamosi au ijumaa ama jumapili ndio ufanye kumuabudu Mungu hapana Bali, Kila siku na Kila saa unapaswa umwabudu Mungu Wala haipaswi ufungwe katika kifungo cha siku, kama umeamua kumuabudu Mungu yafanye yawe maisha yako Kila siku na sio jumamosi tuu.
 
Unajua origin ya Sabath inaanzia kwenye uumbaji,angalia Kut 20:8-11,wewe umeacha huu mstari umeona tu kwenye kumb la torati ilipoongelewa na kumbolewa kutoka Misri...umewahi kujifunza kitabu Cha torati kazi yake haswa?
Naelewa vizuri kabisa.
Lakini nafikiri itakuwa hukunipata pale juu kabisa maelezo ya mwanzoni kabisa kabla sijaelezea vifungu vya MABADILIKO YA SABATO YALIOTABIRIWA NA KUFANYWA NA MUNGU MWENYE KUPITIA YESU KRISTU.

Sijakataa uwepo wa sabato hiyo ya mwanzo kabla ya ufufuko wa Yesu unayoizubgumzia wewe, mbali na hilo fungu ulilonipatia. Zaidi imefafanuliwa na kuelezewa katika mafungu yafuatayo ya Biblia na hasa agano la kale kuna maagizo, maelekezo na amri nyingi tu kuhusu kuiishi na kuifuata sabato (sabato ya kiyahudi). mfano waweza kurejea mafungu yafuatayo: isaya 56:2, isaya 58:13-14, kutoka 20:8-11, kumb 5:11-15, yeremia 17:19-27, Eze 20:20-24, Mwanzo 2:3, Kutoka 13:13, Kut. 16:23, Kut. 16:29, Kut. 35:3, Hes. 15:32 hayo mafungu yote hapo juu ni maagizo ya Mungu kwa wayahudi(taifa teule) kuhusu kuiishi na kuifuata sabato
 
Mliofungwa kwenye kifungo cha kuabudu siku Fulani tuu Mungu awasaidie, haiitaji PhD kuelewa kwamba Mungu hataki Wala haitaji kuabudiwa kwenye hiyo siku unayoitaka wewe na wenzio ambao mnataka iwe hivyo,,,,,, Mungu anatamani wanaomwabudu wamuabudu katika mienendo Yao yote yaani Kila dakika Kila saa Kila wakati wewe umwabudu na kumuishia Mungu sio usubiri hadi jumamosi au ijumaa ama jumapili ndio ufanye kumuabudu Mungu hapana Bali, Kila siku na Kila saa unapaswa umwabudu Mungu Wala haipaswi ufungwe katika kifungo cha siku, kama umeamua kumuabudu Mungu yafanye yawe maisha yako Kila siku na sio jumamosi tuu.
Wala msiache kukusanyika kama ilivyodesturi ya watakatifu.

Asiyefanya kazi na asile

Siku sita Fanya kazi lakini siku ya saba ni SABATO ya Bwana Mungu wako.

Ambao wanapuuza agizo la sabato ndio wako kwenye kifungo.
Maana suala la kumuabudu Mungu linajulikana. Na kwa hekima zake akatenga siku nzima ukae ukitafakari ukuu wake.

Kupinga agizo hili la kifalme ni kumuonyesha dharau Mungu na kuyilia shaka uwezo wake na maamuzi take
 
Mungu alizipanga siku kwa mpangilio sio shagharabaghara hadi kila mtu ajipangie anavyotaka.

Maelezo aliyoyatoa alikuja kuyarudia kwa Wymayahudi ( sio kuyaanza). Na wayahudi licha ya kumkataa Yesu ila ishu ya sabato inafuatwa siku zote nahawajawahi kubadilisha na nijumamosi.

Ziko tafsiri za kiswahili kiingereza nyingi sana za Biblia ziko wazi kuwa Sabato Jumamosi, siku ya kwanza imewekea ni jumapili.

Huu sio mjadala uko wazi, ndio maana hii mada nimeiweka makusudi ijumaa kuu kbla ya sabato.

1. JUMAMOSI
2. JUMAPILI
3. JUMATATU
4. JUMANNE
5. JUMATANO
6. ALHAMISI
7. IJUMAA

Jumamosi inakuwaje siku ya saba ilhali neno lenyewe linamaanisha moja/kwanza?
 
Poleee

Mabadiliko ya sabato kutoka jumamosi kwenda jumapili yalifanywa na Mungu mwenyewe. Kisha hilo kufanyika Yesu aliwatangazia wayahudi kwa maneno na matendo.

Kiufupi kabisa. Mwisho wa sabato ya kiyahudi umetangazwa mara nne katika Biblia Na kukuthibitishia hilo zisome sehemu hizo kama zinavofuata hapa. Hosea 2:11, Ebr 4;4-10, Rum 14;4-10 , kol 2:16-17

Sabato imebailishwa na kutangazwa kuwa ilikuwa ni kivuli tu cha mambo yajayo
(rejea kol 2:16-17)
Nanukuu
“16Kwa hiyo mtu asiwahukumu ninyi kuhusu vyakula au vinywaji, au kuhusu kuadhimisha sikukuu za dini, au Sikukuu za Mwandamo wa mwezi au Siku ya Sabato. 17Hizi zilikuwa kivuli cha mambo ambayo yangekuja, lakini ile iliyo halisi imo ndani ya Kristo.”

na hatimaye siku zote zimetangazwa kuwa sawa mbele ya Mingu (rejea Rum 14:4-10)

kiufupi, kwa sababu ya uzito na woga wa kuachana na siku walioizoea kusudi kifuata siku mpa (SIKU YA BWANA), wafuasi wa yesu walikuwa njia panda na hivyo wakawa wanahuduria sabato pamoja na wayahudi wote na SIKU YA BWANA ilipofika wakawa wanajikusanya peke yao ili kusali, kusoma maandishi yao na kumega mkate (rejea matendo 20:7)

Nanukuu 7Siku ya kwanza ya juma tulikutana pamoja kwa ajili ya kumega mkate. Paulo akaongea na watu, naye kwa kuwa alikuwa amekusudia kuondoka kesho yake, aliendelea kuongea mpaka usiku wa manane”

Hakuna andiko lolote Mungu aliposema Sabato au siku ya Saba ni Jumamosi.
Someni maandiko vizuri.
hakuna muda wowote uliopata kupotea tangu uumbaji ulipotokea mpaka wakati huu. Kwa hiyo mzunguko ule ule wa siku saba za juma ulioanzishwa wakati wa uumbaji ndiyo mzunguko ule ule wa siku saba za juma kwa leo ambao tunaendelea kuufuata hata kama majina ya juma yamebadilishwa kutegemeana na kalenda inayotumika!
Wakati kalenda ilipobadilishwa kutoka katika ile ya Julia kwenda kwa kalenda ya Gregori nyuma katika karne ya kumi na sita, iligundulika kwamba kalenda ya Julia ilikuwa imepungua siku 10 kutoka katika mwaka mmoja halisi. Lakini mzunguko ule ule wa siku za juma la siku saba haukubadilishwa hata kama siku kumi ziliongezwa kwa Kalenda ya Gregori. Alhamisi, Oktoba 4, 1582 katika kalenda ya Julia, ilifuatwa mara moja na Ijumaa, Oktoba 15, 1582 katika kalenda ya Gregori – hivyo, kutunza mwendelezo wa mzunguko wa juma la Jumapili kwenda Jumamosi! Lakini hata kama wengine hawataamini ukweli kwamba hakujakuwepo wakati uliopotea tangu uumbaji, Mungu anataka kabisa kuonyesha watu wake wote ni siku gani ya juma leo iliyo siku ya saba ya juma – ibada ya kweli ya Sabato ya Mungu!
Wakati Kristo alipokuwa katika dunia hii, akiwa Bwana wa Sabato, pasipo shaka alijua kabisa ni siku gani ya juma ilikuwa ni Sabato ya siku ya saba ya zamani ya uumbaji kumwabudu Mungu [siku hiyo]. Lakini kwa sababu tunatumia kalenda tofauti leo kuliko Kristo alizopata kuzitumia, ni siku ipi ya juma katika kalenda yetu ya kisasa ambapo Sabato ya siku hii ya saba huangukia? Biblia kwa wazi na moja kwa moja huwaonyesha wote watakaoona, katika matukio yanayozunguka kusulubishwa na kufufuka kwa Bwana wetu na Mwokozi Yesu kristo, kwa uhalisia ni siku ipi ya juma leo ni Sabato takatifu ya Mungu.
Biblia imeweka kumbukumbu kwamba Kristo alisulubishwa siku ya sita ya juma, au siku ya maandalizi – siku kabla ya Sabato haijatokea (angalia Marko 15:42; Luka 23:54; Yohana 19:31, 42; Mathayo 27:62), Alifufuka siku ya kwanza ya juma, au siku baada ya Sabato kuwa imepita (angalia Mathayo 28:1-8; Marko 16:1-10; Luka 24:1-8; Yohana 20:1), hivyo ikionyesha kwamba Kristo alikuwa amepumzika kaburini wakati wa siku ya saba ya Sabato. Ni maarifa yaliyo wazi kwamba Kristo alifufuka kutoka kaburini siku ya Jumapili asubuhi – ambayo wengi hurejea kama Pasaka (angalia Mdo 12:4). Tukiwa na maarifa haya ya ukweli, basi inakuwa ni rahisi kuamua kiuhalisia ni siku gani za juma katika kalenda yetu ya kisasa huendana pamoja na siku za juma hapo zamani.
Kutokana na kwamba Kristo alifufuka katika siku tunayoiita Jumapili leo, siku hii inaendana na siku ya kwanza ya juma hapo zamani – au siku baada ya Sabato kuwa imepita. Hatimaye, siku tunayoiita Jumamosi katika kalenda yetu ya kisasa, huendana na siku ya saba ya juma hapo zamani, na siku tunayoiita Ijumaa katika kalenda yetu ya kisasa huendana na siku ya sita ya juma hapo zamani – au siku ya maandalizi kabla ya Sabato kuanza! Hivyo, wote wanaotamani kufuata na kumtumikia Mungu kwa mioyo yao yote, mawazo, roho, na nguvu, kutokana na upendo kwa kile alichokwisha kukifanya na anaendelea kukifanya kwa ajili yao, wataona kuwa Sabato ya siku ya saba ya Mungu leo ni Jumamosi – siku baada ya Ijumaa, na siku kabla ya Jumapili! Hii basi inatuonyesha kwa wazi kwamba siku ya Sabato ya Mungu haijabadilishwa sehemu yake ya saba katika mzunguko wa kila juma tangu ilipofanywa takatifu wakati wa uumbaji, na wala haitabadilishwa!
 
1. JUMAMOSI
2. JUMAPILI
3. JUMATATU
4. JUMANNE
5. JUMATANO
6. ALHAMISI
7. IJUMAA

Jumamosi inakuwaje siku ya saba ilhali neno lenyewe linamaanisha moja/kwanza?
Ndio maana nilimuuliza swali juu kuwa mosi maanake nini
 
Mimi ninasali jumapili na ndio siku sahihi kwa wakristo sababu ni siku ya UFUFUKO WA YESU MWENYEWE, ni siku ya USHINDI, NI SIKU KUKOMBOLEWA TOKA UTUMWA DHAMBI NA MAUTI, hiyo ndio sabato ya agano jipya, sio KIVULI TENA CHA SABATO YA KWANZA JUMAMOSI, sabato ya agano la kale.
Ni wapi Mungu amepata kusema hili? Halipatikani popote katika neno la Mungu. Je, kuna haki gani basi, kwa mtu yeyote kufanya sababu kama hiyo na kisha kujenga badiliko la Sabato juu yake? Mungu kamwe hakuwataka watu kutunza siku yoyote kama ukumbusho wa ukombozi. Lakini alituamuru kutunza kitakatifu Sabato ya siku ya saba kama ukumbusho wa uumbaji wake na hivyo kumtambua Mungu kama Mwumbaji wetu.
Hata hivyo kama, ingekuwa wajibu kutunza siku moja ya juma kutokana na sababu hii, zaidi kwa uhakika siku ya kusulibishwa ina madai yenye uzito. Haisemwi kwamba tuna ukombozi kupitia katika ufufuo wa Kristo, lakini inasemwa kwamba tuna ukombozi kwa njia ya kumwagwa kwa damu yake [Kristo] (angalia Ufunuo 5:9; Waefeso 1:7; Wakolosai 1:14; Waebrania 9:12, 15). Maajabu ya tendo la Yehova katika kumtoa Mwanawe mpendwa na wa pekee kufa kwa ajili ya jamii ya waasi ilikuwa ni miwani ya ukombozi wa upendo ambao juu yake ulimwengu ulitakiwa kuangalia kwa mshangao katika kipindi chote cha milele. Nani angeshangaa kwamba jua lilikuwa limefunikwa katika giza na kwamba [vitu vyote vya] asili vilitetemeka kwa mwonekano! Ijumaa, siku ya mateso, kwa hiyo, ina madai makubwa zaidi kuliko siku ya ufufuo; lakini Mungu hajatoa amri ya kutunza mojawapo.
Kama tungeadhimisha ukombozi, hakuna umuhimu wa kuiba utakatifu wa siku ya pumziko la Bwana ili kuiadhimisha. Kwani Mungu ametupatia ukumbusho kwa tukio hili (angalia 1 Wakorintho 11:23-26).
 
1. JUMAMOSI
2. JUMAPILI
3. JUMATATU
4. JUMANNE
5. JUMATANO
6. ALHAMISI
7. IJUMAA

Jumamosi inakuwaje siku ya saba ilhali neno lenyewe linamaanisha moja/kwanza?
Majina hayakuoangiwa kanisani mkuu.
Unapanga tu ila ukifika sehemu ukakuta dhahabu inaitwa tope au mkaa unayeijua huangaiki.

Kuna nchi zaidi ya 20 duniani hii tunayoiita Jumamosi inaitwa moja kwa moja Sabato. Mfano Spain.

Sisi tunayoiita ijumaa kuu waingereza goodfriday. Haimaanishi.imebadilishwa
 
hakuna muda wowote uliopata kupotea tangu uumbaji ulipotokea mpaka wakati huu. Kwa hiyo mzunguko ule ule wa siku saba za juma ulioanzishwa wakati wa uumbaji ndiyo mzunguko ule ule wa siku saba za juma kwa leo ambao tunaendelea kuufuata hata kama majina ya juma yamebadilishwa kutegemeana na kalenda inayotumika!
Wakati kalenda ilipobadilishwa kutoka katika ile ya Julia kwenda kwa kalenda ya Gregori nyuma katika karne ya kumi na sita, iligundulika kwamba kalenda ya Julia ilikuwa imepungua siku 10 kutoka katika mwaka mmoja halisi. Lakini mzunguko ule ule wa siku za juma la siku saba haukubadilishwa hata kama siku kumi ziliongezwa kwa Kalenda ya Gregori. Alhamisi, Oktoba 4, 1582 katika kalenda ya Julia, ilifuatwa mara moja na Ijumaa, Oktoba 15, 1582 katika kalenda ya Gregori – hivyo, kutunza mwendelezo wa mzunguko wa juma la Jumapili kwenda Jumamosi! Lakini hata kama wengine hawataamini ukweli kwamba hakujakuwepo wakati uliopotea tangu uumbaji, Mungu anataka kabisa kuonyesha watu wake wote ni siku gani ya juma leo iliyo siku ya saba ya juma – ibada ya kweli ya Sabato ya Mungu!
Wakati Kristo alipokuwa katika dunia hii, akiwa Bwana wa Sabato, pasipo shaka alijua kabisa ni siku gani ya juma ilikuwa ni Sabato ya siku ya saba ya zamani ya uumbaji kumwabudu Mungu [siku hiyo]. Lakini kwa sababu tunatumia kalenda tofauti leo kuliko Kristo alizopata kuzitumia, ni siku ipi ya juma katika kalenda yetu ya kisasa ambapo Sabato ya siku hii ya saba huangukia? Biblia kwa wazi na moja kwa moja huwaonyesha wote watakaoona, katika matukio yanayozunguka kusulubishwa na kufufuka kwa Bwana wetu na Mwokozi Yesu kristo, kwa uhalisia ni siku ipi ya juma leo ni Sabato takatifu ya Mungu.
Biblia imeweka kumbukumbu kwamba Kristo alisulubishwa siku ya sita ya juma, au siku ya maandalizi – siku kabla ya Sabato haijatokea (angalia Marko 15:42; Luka 23:54; Yohana 19:31, 42; Mathayo 27:62), Alifufuka siku ya kwanza ya juma, au siku baada ya Sabato kuwa imepita (angalia Mathayo 28:1-8; Marko 16:1-10; Luka 24:1-8; Yohana 20:1), hivyo ikionyesha kwamba Kristo alikuwa amepumzika kaburini wakati wa siku ya saba ya Sabato. Ni maarifa yaliyo wazi kwamba Kristo alifufuka kutoka kaburini siku ya Jumapili asubuhi – ambayo wengi hurejea kama Pasaka (angalia Mdo 12:4). Tukiwa na maarifa haya ya ukweli, basi inakuwa ni rahisi kuamua kiuhalisia ni siku gani za juma katika kalenda yetu ya kisasa huendana pamoja na siku za juma hapo zamani.
Kutokana na kwamba Kristo alifufuka katika siku tunayoiita Jumapili leo, siku hii inaendana na siku ya kwanza ya juma hapo zamani – au siku baada ya Sabato kuwa imepita. Hatimaye, siku tunayoiita Jumamosi katika kalenda yetu ya kisasa, huendana na siku ya saba ya juma hapo zamani, na siku tunayoiita Ijumaa katika kalenda yetu ya kisasa huendana na siku ya sita ya juma hapo zamani – au siku ya maandalizi kabla ya Sabato kuanza! Hivyo, wote wanaotamani kufuata na kumtumikia Mungu kwa mioyo yao yote, mawazo, roho, na nguvu, kutokana na upendo kwa kile alichokwisha kukifanya na anaendelea kukifanya kwa ajili yao, wataona kuwa Sabato ya siku ya saba ya Mungu leo ni Jumamosi – siku baada ya Ijumaa, na siku kabla ya Jumapili! Hii basi inatuonyesha kwa wazi kwamba siku ya Sabato ya Mungu haijabadilishwa sehemu yake ya saba katika mzunguko wa kila juma tangu ilipofanywa takatifu wakati wa uumbaji, na wala haitabadilishwa!
Mkuu kwa hiyo wewe katika kupanga jumamosi za sabato ni unafuata utaratibu uliopangwa calenda ipi ?

Ni unafuata kalenda gani kujua kesho ni sabato ?
 
Majina hayakuoangiwa kanisani mkuu.
Unapanga tu ila ukifika sehemu ukakuta dhahabu inaitwa tope au mkaa unayeijua huangaiki.

Kuna nchi zaidi ya 20 duniani hii tunayoiita Jumamosi inaitwa moja kwa moja Sabato. Mfano Spain.

Sisi tunayoiita ijumaa kuu waingereza goodfriday. Haimaanishi.imebadilishwa

spain wanaiita saturday sábado (sabath)

spain hawajui kitu kinaitwa jumamosi mkuu, na kwakuwa wale ni wasomi ukiwaeleza maana ya neno jumamosi watakataa kuwa ni siku ya saba!

na ijumaa ni ijumaa wala sio friday
ijumaa ndio siku ya saba kulingana na lugha yetu ambayo imetoholewa kutoka neno la kiarabu Al-Jumah

Friday inatokana na sayari ya yunus ama Venus

The days were named after the planets of Hellenistic astrology, in the order: Sun, Moon, Mars (Ares), Mercury (Hermes), Jupiter (Zeus), Venus (Aphrodite) and Saturn (Cronos).
 
“Wao [Waprotestanti] huona ni wajibu wao kuitunza Jumapili kitakatifu. Kwa nini? Kwa sababu Kanisa Katoliki huwaambia kufanya hivyo. Hawana sababu nyingine [zaidi]....Utunzaji wa Jumapili hivyo basi huja kuwa sheria ya kikanisa tofauti kabisa kutoka katika sheria ya Mungu ya kutunza Sabato....Mwanzilishi wa sheria ya Jumapili...ni Kanisa Katoliki.” Ecclesiastical Review, Februari, 1914.

“Jumapili...ni uumbaji kabisa wa Kanisa katoliki.” American Catholic Quarterly Review, Januari, 1883.

“Jumapili...ni sheria ya kanisa Katoliki pekee...” American Sentinel (Catholic), Juni, 1893.

““Jumapili ni pando la Kikatoliki na madai yake kuitunza yanaweza kutetewa tu kwa njia ya kanuni za Kikatoliki....Kutoka mwanzo hadi mwisho wa Maandiko hakuna hata fungu moja ambalo linahalalisha kubadilishwa kwa ibada ya hadhara ya kila juma kutoka siku ya mwisho ya juma kwenda siku ya kwanza.” Catholic Press, Sydney, Australia, August, 1990.
 
Back
Top Bottom