Ikitokea Askari MP wa JWTZ na wa Magereza 'wamekubananisha' katika '18' zao utachagua nani ndiyo wakupe Adhabu?

Ikitokea Askari MP wa JWTZ na wa Magereza 'wamekubananisha' katika '18' zao utachagua nani ndiyo wakupe Adhabu?

Magereza ni shida utakula virungu kufa hufi ila kilema utakipata. Jwtz maisha yako yapo hatarini maana wale mafunzo yao ni kuondoa uhai wa adui magereza mafunzo yao ni kumtuliza mfungwa
 
Nasisitiza cheza kote ila usiingie kwenye 18 za MAGEREZA, chezeni mchezavyo, MAGEREZA wanapiga acheni utani kabisa.
Mimi sijawahi pigwa na MAGEREZA ila nimeshuhudia watu kibao sambamba na Askari kadhaa walioingia kwenye 18 za hao Mamwela.

MaMP wa JWTZ wamenipiga sana 833 KJ ila unaona ni kawaida, na zaidi ni Adhabu ambazo karibu kila siku unakutana nazo kambini, sema tu wao wanaongeza mikazo kidogo.

JAMANI MAGEREZA WANAPIGA ACHENI HUO UTANI KABISA.

Mtafuteni yule KOMANDOO wa MBOWE akusimulieni vizuri.
 
Hawa wote wanashughulika nakurekebisha nidhamu kwa njia ya adhabu. MP wa magereza anashughulikia nidhamu za wafungwa wakorofi(raia).
MP wa Jwtz anashughulikia nidhamu za askari wakorofi... narudia,ASKARI wakorofi!Nawote huwa wanaogopwa katika maeneo yao. Sasa fikiria Kam MP wa JW anaogopwa na askari watukutu,vipi umlinganishe nahuyu anayeogopwa na raia(wafungwa).
Kinachofanya magereza waonekane hatar nikwasababu wale wafungwa wanapopata adhabu huwa wanazisimulia mtaani..hii nitofauti na askari ambao Mambo yakambini huishia humohumo.Huwez kuwasikia wakilalamikia adhabu wanazopata pale wanapokosea.
Kwa maoni yangu MP wa JW ni wabaya kuliko wa magereza
Magereza ndio mwisho wa matatizo hata Mjeda atatubu akiingia kwenye 18 za magrwza, inshort Askari Magrza ndio askari anaeweza kukutana na askari wa jeshi lolote na kumsurubu.
 
Magereza wanapiga,wakina h.mdee si waliwabip wakapigiwa si unaona kna watu walivaa hogo,wengine viuno wamevunjwa

Ova
 
Jwtz hawana njaa ila Wana vibali vya kumkamata Askari yeyote wa jeshi lolote na kumtuliza.
 
Hujawahi kuona Magereza wanavotembeza kichapo.

Kuwa Mwanajeshi haimaanishi wewe ni mkomavu kuliko Raia wote, kumbuka kuna majambazi wanazichapa kuliko makomandoo wa JWTZ. Sasa hao majambazi wanatunzwa na hao MAGEREZA.

NI RAHISI KUMPA ADHABU ASKARI KWA KUWA KULE NI UTII TU, LKN KUMPA ADHABU RAIA AMBAYE ANAWEZA KUKUCHENJIA MKAZICHAPA NI HATARI SANA.

KWANGU NI BORA NIKUTANE NA JWTZ naweza toka natambaa (JKT imenikuta sana hii)
Lkn MAGEREZA unatoka umezimia
Unamjua komandoo au unaropoka tu?
 
C rahisi mwanajeshi au magereza kumpiga raia wa kawaida bila sababu ila hawa police wengine form four failure ni bure kabisa akili hawana kabisa unaweza kuta upo kituoni ukapigwa bonge kofi bila sababu ya msingi.sheenzy sana

Respect kwa jwtz hawa jamaa hawana mambo ya kishamba kabisa, kwa bahati mbaya nilishwahi gonga basi lao nikapusua taa yao ila walikuwa calm waliniambia niwe makini wakaondoka zao,sipati picha kama ningepasua taa za hawa Polisi tahira
 
Askari jela ni habari nyingine.. Nenda Segerea kuna 'Sero moja ya watu nunda :itokee wanaitaji choo halafu usumbue we ndo utawajua hao. Anakuvua nguo uwe uchi. Usawa wa makalio na kiuno kwa nyuma.. Mbata moja lazima uharo utoke tu[emoji4][emoji4][emoji4]
 
C rahisi mwanajeshi au magereza kumpiga raia wa kawaida bila sababu ila hawa police wengine form four failure ni bure kabisa akili hawana kabisa unaweza kuta upo kituoni ukapigwa bonge kofi bila sababu ya msingi.sheenzy sana

Respect kwa jwtz hawa jamaa hawana mambo ya kishamba kabisa, kwa bahati mbaya nilishwahi gonga basi lao nikapusua taa yao ila walikuwa calm waliniambia niwe makini wakaondoka zao,sipati picha kama ningepasua taa za hawa Polisi tahira
Usijisifie kuwa hao JWTZ uliwagonga na wakakuacha tu ukweli ni kwamba hiyo Siku huenda uliwakuta ndiyo wametoka Kupokea Mishahara yao ama iko mbioni kutoka.

Ili uamini hili nakuomba kwa Makusudi Kawagonge tena kati ya tarehe zao Dume za 9 hadi 22 ya kila Mwezi ndipo utawajua walivyo na Usununu ( Hasira ) na kwanini Nyoka hana Ugoko.
 
Back
Top Bottom