Ikitokea Rais Samia akakemea kufungwa kanisa la Gwajima na kutengua uteuzi wa Bashungwa CCM hawatamsifia?

Mwandishi ameshtuka saa 10 alfajiri katikati ya dimbwi la mandoto ya kukimbizwa vichakani....
 
Kuna yule jamaa anajigamba kwamba kile kikosi cha chinjachinja alikuwa anakiongoza yeye.
 
Shetani akizeeka anakuwa malaika ila chama dola shetani akizeeka anabaki hivyo hivyo shetani!!.
 
Wewe mbona hujatekwa ?!
Au watekaji ni wajomba zako ndio maana wanawateka na kuwaua watu wengine wewe wanakuacha?!
Na mbona mimi hapa sijatekwa ?
Watekaji wananiogopa ?!
Kwanini watekaji wanateka watu wengine mimi wananiacha?!
KWANINI MIMI NA WEWE HATIJATEKWA?!
 
Hii hadithi inatufundisha nini?
 
Tatizo Taifa kwa sasa lina watu wengi wanajali zaidi maslahi binafsi kuliko maslahi ya Taifa.
Watu wameweka pembeni taaluma zao,waneweka pembeni imani zao za kiroho na wameweka pembeni ubinadamu wao na kutanguliza mbele maslahi yao binafsi.
Ni bahati mbaya pia kuwa mfumo wa utawala umeweka maslahi mazuri mno upande mmoja tu, SIASA.
Kila mtu anataka kuwa mwanasiasa kwa namna na mbinu yoyote ile ili kupata hayo maslahi.Uliyoyaandika hapa ni vigumu kufanyika japo ni sahihi.
Ni swala la kusubiri na kuona yakitokea.
 
Bashungwa kadandia Gari la ibirisi kawa shetani kuliko waliopita na kibaya zaidi kwa Bashungwa ni kuomba bilion 15 kazi maalum ya kudidimiza demokrasia na vitendo haramu vya kishetani
Ameziomba wapi hizo bilion 15 una document? Shetani mkuu ni bibi yenu tunahitaji kumkataa bibi yenu na mambo yake yote na kazi zake zote tuache kupambana na vijimatawi.
 
Kumbe ni mawazo tu....
 
Swali gumu ni je, Askofu ndie kanisa?.

Nafikiri ilitakiwa iende barua ya onyo kabla ya yote sababu ukiangalia Askofu ni mtumishi tu wa kanisa wala kanisa sio mali yake. Kuna bodi ya wadhamini na kuna waanzilishi pia.

Tumeenda haraka sana.
 
Wakati mwingine unatakiwa kuwalinda uliowapa majukumu kukusaidia kuongoza ili wazidishe loyalty! Wakati mwingine unalazimika kuwashughulikia ili kulinda legality yako ya kuongoza.
===
Sasa mleta mada fafanua mada yako kwa kuzingatia mitazamo hii miwili ya loyalty and legality.
 
Swali gumu ni je, Askofu ndie kanisa?.

Nafikiri ilitakiwa iende barua ya onyo kabla ya yote sababu ukiangalia Askofu ni mtumishi tu wa kanisa wala kanisa sio mali yake. Kuna bodi ya wadhamini na kuna waanzilishi pia.

Tumeenda haraka sana.
Labda ilionekana udharura...! Lakini, mara ya Mwisho ilisemekana Muhusika hakupokea barua....halafu yupo wapi Sasa hivi huyu Muhusika? Kaenda mlimani kufungwa zile siku saba?Yupo wapi?
 
Labda ilionekana udharura...! Lakini, mara ya Mwisho ilisemekana Muhusika hakupokea barua....halafu yupo wapi Sasa hivi huyu Muhusika? Kaenda mlimani kufungwa zile siku saba?Yupo wapi?
Ila hili litazidi kuvuruga mambo maana askofu ana aina ya waumini sio watu wa kutumia maarifa ya kawaida. Wao watatfsiri kama vita vya kiroho. Kitu mbaya sana hiyo.
 
Endelea kuota hadi 2030.
Chadema imekula kwao.
Wewe unaiota CHADEMA, mimi naiamini Tanzania.
Sina la zaidi la kukueleza mtu kama wewe unayejulikana kuwa bwege tu kutokana na michango iliyomo humu JF
 
Sasa haioni kuwa matope yote yanaenda kwake!!!?
Inaona.
Lakini na yenyewe, kama tulivyo wote waTanzania kwa wakati huu, ni mateka tu wa hilo genge. Wao (waliomo ccm) wanatishiwa maslahi yao; kama ulivyosikia "Magwajima wote wasipewe nafasi ndani ya chama) Hadi wapatikane "Magwajima" wa kutosha huko CCM, hapo ndipo utaona cheche zikitimka; kama hawatawahiwa na hili joto lililopo nje ya chama litakalowafyeka wote.
 
Kikwete tu ndiye angeweza kufanya hivyo. Samiah hajui siasa na inaelekea kila kitu anashauriwa naye anatekeleza bila kuchanganya na zake.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…