Uchaguzi 2020 Ikiwa Dkt. Magufuli atafanikiwa kushinda, aachane na agenda za kuminya Upinzani

Kura tunapiga lakini zinaibiwa. Sasa kwakuwa imezoeleka hivyo tunataka kinuke ili watu wafukuze nzi wa kijani ikulu. Damu ikimwagika ndio ukombozi bila hilo hatutaweza.
 
Kwa akili za hivyo vichwa viwili inawezekana.
Ndio hao hao maana mmoja alikuwa mambo ya ndani, mwingine alikuwa na ushawishi mkubwa kwa rais. Kumbuka kauli za nchemba bungeni huitaji kujua nini anamaanisha.
 
Kura tunapiga lakini zinaibiwa. Sasa kwakuwa imezoeleka hivyo tunataka kinuke ili watu wafukuze nzi wa kijani ikulu. Damu ikimwagika ndio ukombozi bila hilo hatutaweza.
Kupiga kura siyo tatizo, loss ni vyama vya upinzani kukosa umoja ( Rejea nilichoandika ) Ni vigumu sana kukiondoa chama tawala madarakani kwa aina ya upinzani tulionao. Vyama vipo zaidi ya 13, km kweli vingeungana na kudai kuwepo Kwa Tume Huru ya Uchaguzi ama kugoma kuingia kwenye uchaguzi mkuu kwa kukosa tume huru. Hapo mabadiliko ni lazima kwa sababu pamoja na chama tawala kuwa mbuyu, kingesalimu amri tu. Sasa shuhudia sarakasi za hivyo vyama, utashangaa kwanini vinaitwa vyama vya upinzani na siyo CCM B!

Kukinukisha siyo suluhisho. Wananchi wenyewe tuna nafasi ya kuvikataa vyama vya upinzani visivyotambua lengo lao ni nini na vyama vinavyojitambua vijipange na kuwa na mikakati ya pamoja ya kuchukua dola kwa uchaguzi unaofuata na siyo kuwa na mikakati ya zimamoto.
 
Huwezi ukawaacha wapinzani waishi watakavyo sababu hawa ni zaidi ya wapinzani..ni watu wanaopenda chokochoko, fitina, uongo na matusi.. muulize kikwete.
 

Ni vizuri kuangalia kila hatua inayosemekana ni unyanyasaji wa upinzani kwa kina, na kufanya hivyo tutaona michango ya upinzani ina manufaa au laa na wapi.

Hatua yeyote ile lazima tujenge uwezo wa kuangalia kwa muono na utafakarishi wa Hypothesis na synthesis analysis.

Kwa kufuata hali hiyo ndio kila kisemwacho au kifanywacho na pande zote ama upinzani au uongozi wa Magufuli utaweza kupata picha halisi kuwa yafanywayo ni sawa au hapana.

Wakosefu au wauwaji wanapo hukumiwa au kifungo kirefu au kifo haipendezi, lakini kufanyika huko kunaweza kuwa ku- deter kurudiwa rudiwa kwa makosa yasio pendeza.

Mkuu Joka kuu, tupo ambao telikuwa waumini wa upinzani wa kweli kwa miaka kadhaa na tukawa viongozi katika ngazi zetu mbali mbali kichama.

Tukitaka kutapika tuna weza ikaonekana kama tunahalalisha matendo ya Magufuli- lakini sisi pia upinzani lazima tujitahidi kutengeneza matendo ya heshima na tabia ambazo CCM wanaweza kutuona katika sura ya utuu. Ikitiliwa maanani demokrasia yetu bado changa.

kWA MFANO: Nakiri bila kushawishiwa serikali ya awamu ya tano kuna vitu vingi vizuri na vya kimaendeleo wamefanya kwa taifa hili.

Tunaposema hawafanya kitu chochote au tunabadilisha maneno kuonyesha kila wafanyayo hayana thamani kwa watu wetu, jee unategemea Magufuli akushangilie kwa kubalisha ukweli wakati umesema uongo?

Kwa maamuzi ya haraka haraka kwa kubadilisha au kudhihaki kila afanyalo Magufuli anaona bora atunyanyase kwa kuwa analipa tunacho mfanyia. Kumdhihaki hata anapofanya kizuri.

Lazima tuabadilike pia ili nao tuwashawishi wabadilike. CROSS CUTTING.
 

..imepita miaka 4+ tangu Jpm aingie madarakani.

..nadhani tunaweza ku-conclude kwamba Jpm si kiongozi anayeweza ku-co-exist na vyama vya upinzani.

..nimeeleza kwamba binafsi nilianza kuona viashiria vya Jpm kutokukubaliana na demokrasia ya vyama vingi tangu alipokuwa waziri ktk serikali ya Jpm.

..Yapo matamko yake ktk nyakati mbalimbali ambayo yalikuwa yana viashiria vya mambo mabaya ambayo tunayashuhudia leo hii yakiwatokea wapinzani.

..jambo lingine unalopaswa kuangalia ni aina ya kampeni za uchaguzi ambazo Jpm alifanya mwaka 2015. kampeni zile zilijaa MATUSI makubwa-makubwa dhidi ya mpinzani wake, na kwa msingi huo ziliacha MADONDA/MAJERAHA kwa wadau wa uchaguzi ule.

..mshindi mwenye busara, na ukomavu wa kisiasa, alipaswa kuhakikisha kwamba anatibu madonda/majeraha ya kipindi cha kampeni za uchaguzi. Jpm hakushughulika na jambo hilo badala yake alitangaza VITA dhidi ya vyama vya upinzani nchini.

Kuhusu Wapinzani kumsifia / kutomsifia Jpm:

..mimi nadhani wapinzani wakitoa kasoro na mapungufu ya kila aina ndipo tutakapopata nafasi ya kum-appreciate Jpm genuinely.

..wapinzani wasipokuwa "gado" au vigilant, au wakaingia ktk mkumbo wa kusifia na kuabudu, mambo yakiharibika wataingia ktk lawama, kwasababu ni wajibu wao kuikagua na kuikosoa serikali wakati wote.

..Kukosoa maana yake kuna mambo yamefanyika. Jpm angekuwa hajafanya jambo lolote hakuna ambaye angemkosoa.
 
Akifanikiwa kupewa urais awasikilize wananchi wanataka nini asilazimishe wananchi kukubali na kusifia anavyotaka yeye.
Mwalimu Nyerere alisema ukiisha onja nyama ya mtu hutaacha. Hata JPM hataacha. Hiyo iko kwa DNA yake!
 
Tabia ni kama ngozi mkuu ni ngumu sana jamaa kubadilika
 
Mkuu hivi umewahi kuona mwalimu incompetent akiingia darasani bila fimbo au akampa nafasi mwanafunzi kuuliza swali?
 
Ukiwa mpinzani Tanzania inaonekana Kama allien [emoji15]
 
Shida sio Magufuli, ila ni wshauri wake. Hivi leo una weza kuzuia redio na tv kweli? Zisitangaze habari fulani? Su wao Ccm ndio wana jidanganya hizo habari hazionekani?? Mambo ya utopolo kabisa

Kama mshauri wangu akifanya mambo yasiyonipendezea namuonya au kumfuta kazi. Kama anakubaliana na washauri wake maana yake anayapenda yale wanayomwambia.
 
Shida sio Magufuli, ila ni wshauri wake. Hivi leo una weza kuzuia redio na tv kweli? Zisitangaze habari fulani? Su wao Ccm ndio wana jidanganya hizo habari hazionekani?? Mambo ya utopolo kabisa
Shida sio washauri shida ni yeye mwenyewe, tusifiche. Huyu jamaa ni hovyo na hafai kabisa.
 
Shida sio Magufuli, ila ni wshauri wake. Hivi leo una weza kuzuia redio na tv kweli? Zisitangaze habari fulani? Su wao Ccm ndio wana jidanganya hizo habari hazionekani?? Mambo ya utopolo kabisa

Akifanya kazi nzuri sifa zinaenda kwake ila akiharibu lawama zinakua ni za wasaidizi wake,tuacheni unafiki.
 
Tukio la kupigwa risasi Lissu, hila za kununua viongozi wa upinzani, vitabaki kama doa lisilofutika kwa utawala wa kwanza wa Magufuli. Ni moja wapo ya mbinu chafu za kisiasa karne hii ya utandawazi.


Jr[emoji769]
Hali inaweza kuwa mbaya zaidi 2020. He has nothing to lose.
 
Magufuli akishinda urais utafanya nini?
 
Namaanisha upinzani bado sana kishinda Urais wa Tanzania huo ndo ukweli mchungu japo hamtaki kuusikia ! Bado upinzani haujajipanga kimkakati kushinda Urais ndugu!
nkutoe wasi wasi toka 1995 upinzani unashinda
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…