Ikiwa Rais ndiye anatoa pesa zake kwa maendeleo ya nchi, Serikali inapeleka wapi kodi zetu?

Mm siju ninashida gan na mchemba. Simuamini amini.

Increments yetu amefanyaje, siioni
 
Kuna shida gani wakisema Rais anatoa?
Shida ipo kisheria na kikatiba.

Shida ni uongo unaozungumzwa kwa sababu hakuna senti inayotoka mfukoni kwa rais kwa sababu hata kodi halipi.

Shida ipo kwa sababu, maneno hayo yanatumika kuficha ukwapuaji na wizi wa fedha za umma unaofanywa na wanasiasa waliomo serikalini

Shida zipo nyingi sana mkuu
 
Mm siju ninashida gan na mchemba. Simuamini amini.

Increments yetu amefanyaje, siioni
Yeye ndo mshauri mkuu wa masuala ya uchumi. Na mkwamo wote wa kiuchumi na kodi ana inputs zake.

He is a joker
 
Upuuzi
 
Rais bdiye mwenye maamuzi ya mwisho, pesa zitumike vipi na wapi.
 
Communist culture ya kutukuza viongozi. Legacy ya awamu ya 5 iliyokumbatiwa kikamilifu na awamu ya 6. Zote ni kodi za Wananchi; pesa za umma. Lakini kwa vile wanaotawaliwa wameshaonekana mazuzu, wanasemewa chochote na kuimbishwa mapambio ya kila modeli.

Enzi za Mao Zedong (Mao Tse Tung), huko China madaktari walikuwa wakimshukuru Mao kwa kuweza kukamilisha operesheni ya ubongo baada ya kusoma muongozo wake wa papo kwa hapo. Wahandisi, wanasayansi, n.k. wote walikuwa wakidai hadharani kuwa bila “instant guidance” ya Mao wasingeweza kufanikisha chochote! Waulize Wachina wa leo kama hata wanakumbuka ujinga ule.

Tumerudi nyuma kweli kweli!
 
Rais bdiye mwenye maamuzi ya mwisho, pesa zitumike vipi na wapi.
Basi tuseme kuwa Rais ndiye KATIBA ya nchi. Ndiye SHERIA na mshikilia pumzi zetu.

Bunge ni kupoteza hela za umma. Kinachotakiwa ni wizara kuandaa bajeti na kumpelekea Rais aidhinkshe au kukataa kutoa hela
 
Halafu wanaosema hayo ya rais katoa hela, wengi ni wasomi na maprofesa.

Rais analipa kodi kwani?
 
Basi tuseme kuwa Rais ndiye KATIBA ya nchi. Ndiye SHERIA na mshikilia pumzi zetu.

Bunge ni kupoteza hela za umma. Kinachotakiwa ni wizara kuandaa bajeti na kumpelekea Rais aidhinkshe au kukataa kutoa hela
Ndivyo katiba ya Nyerere aliyotuwachia ilivyo.
.rais wa Tanzania ana mamlaka ya kifalme ndani ya Tanzania.
 
Ndivyo katiba ya Nyerere aliyotuwachia ilivyo.
.rais wa Tanzania ana mamlaka ya kifalme ndani ya Tanzania.
Tupe kipengele cha sheria ama ibara ya katiba inayosapoti hayo unayoyasimamia kuhusu rais kumiliki fedha zote za umma....


Kama hauna ni vyema.ukatukiza akili na kulinda heshima yako
 
Tupe kipengele cha sheria ama ibara ya katiba inayosapoti hayo unayoyasimamia kuhusu rais kumiliki fedha zote za umma....


Kama hauna ni vyema.ukatukiza akili na kulinda heshima yako
Isome katiba yote.

Unafikiri kwanini watu wanashikilia kutaka katiba mpya?
 
Halafu wanaosema hayo ya rais katoa hela, wengi ni wasomi na maprofesa.

Rais analipa kodi kwani?
Inashangaza sana. Uongozi wa CCM sasa unategemea kikamilifu propaganda za enzi zile za mwaka 1947! Hawashtuki kabisa kuwa hii ni 2023 - karne nyingine. Wanaamini watanzania “wa asili” wengi bado sifuri kichwani. Kwamba wachache wanaohoji basi hao uraia wao lazima una mashaka au wameshanunuliwa na “mabeberu” na kuwa wasaliti!

Kwamba ukitamka “Rais wetu anashindwa kulala; anahangaika sana kutafuta hela; anamwaga mabilioni ili kuboresha maisha yetu”, basi Watanzania (sijui katika uzuzu wao) watamuona kama malaika fulani hivi au masihi, au “mungu” kabisa ambaye anatakiwa kuheshimiwa sana. Ili akitokea mtu kumpinga, au kumkosoa au hata kutaka kugombea ile nafasi basi mtu huyo aonekane mbaya sana mithili ya shetani!

Btw, ni wazi kabisa kuwa hii yote ni mjumuiko wa “campaign mode” ya kudumu. Tangu awamu iliyopita hawa viongozi siku zote wako kwenye kampeni za uchaguzi wakitumia rasilimali na majukwaa ya shughuli za kiserikali kujinasibu kama wao ndio wahisani wa Watanzania “wanyonge”. Kwamba wao pekee ndio “wanaoweza kuleta maendeleo” katika nchi hii. Ndio wanaoweza kutafuta na kugawa mabilioni ya miradi, ruzuku na fadhila mbalimbali!
 
Huko kwa Biden mbali hata hapo pa majirani tu waseme Ruto ametoa pesa .Wakenya wako vizuri kwenye elimu ya uraia kuliko sisi ambao mtu na akili zake anakiri hadharani kwamba eti ni chawa wa mtu fulani !Idiot
 
Mi nimechoka kujibu mambo ya kijinga labda wana JF wanaweza kutueleza.
Yani wageni wananiuliza ili
Naibu waziri wa afya ametia aibu kabisa kwa kusema Samia anajua kutafuta pesa,... Samia ametoa bilioni.....Ni hela za Samia hizi.....! Huu ni upuuzi mkubwa unaofanywa na mazuzu huko CCM.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…