Ikiwa Rais ndiye anatoa pesa zake kwa maendeleo ya nchi, Serikali inapeleka wapi kodi zetu?

Mm siju ninashida gan na mchemba. Simuamini amini.

Increments yetu amefanyaje, siioni
 
Kuna shida gani wakisema Rais anatoa?
Shida ipo kisheria na kikatiba.

Shida ni uongo unaozungumzwa kwa sababu hakuna senti inayotoka mfukoni kwa rais kwa sababu hata kodi halipi.

Shida ipo kwa sababu, maneno hayo yanatumika kuficha ukwapuaji na wizi wa fedha za umma unaofanywa na wanasiasa waliomo serikalini

Shida zipo nyingi sana mkuu
 
Mm siju ninashida gan na mchemba. Simuamini amini.

Increments yetu amefanyaje, siioni
Yeye ndo mshauri mkuu wa masuala ya uchumi. Na mkwamo wote wa kiuchumi na kodi ana inputs zake.

He is a joker
 
Shida ipo kisheria na kikatiba.

Shida ni uongo unaozungumzwa kwa sababu hakuna senti inayotoka mfukoni kwa rais kwa sababu hata kodi halipi.

Shida ipo kwa sababu, maneno hayo yanatumika kuficha ukwapuaji na wizi wa fedha za umma unaofanywa na wanasiasa waliomo serikalini

Shida zipo nyingi sana mkuu
Upuuzi
 
Tumesikia kila mdomo wa Waziri na viongozi waandamizi wanaposimama kuhutubia ama kuzungumza wanamshukuru Rais kwa kutoa hela ambazo zimwtekeleza miradi ya maendeleo na miundombinu.

Hivyo wanatuaminisha kuwa fedha zote za miradi na maendeleo zinatolewa na rais. Na anayetoa hela hufanya hivyo kwa hiyari halazimishwi. Ndo maana hata akina Pascal Mayalla wanatuasa kuwa tuwe na shukrani kwa hisani anazotufanyia rais ambapo tafsiri inayojengeka ni kuwa Rais hawajibiki kwa yeyote na lolote bali ni utashi wake kufanya kila analofanya na hakuna wa kumhoji na ni kumkosea heshima kuhoji wajibu wake wa kikatiba.

Sasa, tunajjuliza sisi wadadisi na wakaidi wa mfumo usiozingatia katiba na sheria.

  1. Nini hutokea kwa mtu anayegombea urais akashinda na ghafla anakuwa tajjri mkubwa anayeweza kufadhili miradi ya serikali bila masharti magumu?
  2. Tunapolipa kodi zetu na fedha za wafadhili zinapoingia serikalini huwa zinapelekwa wapi? Kwa sababu hatujawahi kusikia serikali imetoa hela za miradi. Rais anajitolea mnoo hadi tunamhurumia
  3. Wizara ya fedha kwa nini isifutwe ama isiwekwe chini ya ofisi ya Rais kwa sababu inakusanya fedha na haiwezi kuziratibu zinaliwa hovyo hadi rais anaingilia kati kutoa fedha zake kufanikisha miradi ya maendeleo
  4. Ushahidi wa ripoti ya CAG unaonesha wazi kabisa kuwa ofisi ya Rais haijawahi kupata hati chafu.
  5. Lakini hakuna wizara wala idara ya serikali iliyokwepa tuhuma za matumizi mabaya ya kodi zetu, hivyo inawezekana kodi zetu zinaliwa na serikali hadi kufikia Rais kutoa fedha zake
  6. Wabunge wana kazi gani kama siyo ulaji wa fedha za umma? Nasema hivyo kwa sababu wakifika Bungeni hugeuka kuwa wabunge wa chama na siyo wa wananchi tena. Tumeona viongozi waandamizi wa vyama wakikutana na wabunge na kuwapa maelekezo hususan Bunge la Bajeti, lazima chama kikuu kiwape maelekezo wabunge na hakuna mahala ambapo wwnanchi wamewahi kusikilizwa na wabunge. Mifano ni mingi sana...

All in all, kama rais anatoa fedha zake kwa maendelo ya nchi, serikali inangoja nini kujiuzulu kwa kushindwa kufanya hivyo kwa jamii? Na kodi zetu zinaenda wapi?

CC: Retired Depal MshanaJR raraa reree imhotep FaizaFoxy dronedrake zitto junior Dkt Mohamed Attia Samia gang johnthebaptist
Rais bdiye mwenye maamuzi ya mwisho, pesa zitumike vipi na wapi.
 
Communist culture ya kutukuza viongozi. Legacy ya awamu ya 5 iliyokumbatiwa kikamilifu na awamu ya 6. Zote ni kodi za Wananchi; pesa za umma. Lakini kwa vile wanaotawaliwa wameshaonekana mazuzu, wanasemewa chochote na kuimbishwa mapambio ya kila modeli.

Enzi za Mao Zedong (Mao Tse Tung), huko China madaktari walikuwa wakimshukuru Mao kwa kuweza kukamilisha operesheni ya ubongo baada ya kusoma muongozo wake wa papo kwa hapo. Wahandisi, wanasayansi, n.k. wote walikuwa wakidai hadharani kuwa bila “instant guidance” ya Mao wasingeweza kufanikisha chochote! Waulize Wachina wa leo kama hata wanakumbuka ujinga ule.

Tumerudi nyuma kweli kweli!
 
Basi tuseme kuwa Rais ndiye KATIBA ya nchi. Ndiye SHERIA na mshikilia pumzi zetu.

Bunge ni kupoteza hela za umma. Kinachotakiwa ni wizara kuandaa bajeti na kumpelekea Rais aidhinkshe au kukataa kutoa hela
 
Halafu wanaosema hayo ya rais katoa hela, wengi ni wasomi na maprofesa.

Rais analipa kodi kwani?
 
Ndivyo katiba ya Nyerere aliyotuwachia ilivyo.
.rais wa Tanzania ana mamlaka ya kifalme ndani ya Tanzania.
 
Tupe kipengele cha sheria ama ibara ya katiba inayosapoti hayo unayoyasimamia kuhusu rais kumiliki fedha zote za umma....

Kama hauna ni vyema.ukatukiza akili na kulinda heshima yako
 
Isome katiba yote.

Unafikiri kwanini watu wanashikilia kutaka katiba mpya?
 
Halafu wanaosema hayo ya rais katoa hela, wengi ni wasomi na maprofesa.

Rais analipa kodi kwani?
Inashangaza sana. Uongozi wa CCM sasa unategemea kikamilifu propaganda za enzi zile za mwaka 1947! Hawashtuki kabisa kuwa hii ni 2023 - karne nyingine. Wanaamini watanzania “wa asili” wengi bado sifuri kichwani. Kwamba wachache wanaohoji basi hao uraia wao lazima una mashaka au wameshanunuliwa na “mabeberu” na kuwa wasaliti!

Kwamba ukitamka “Rais wetu anashindwa kulala; anahangaika sana kutafuta hela; anamwaga mabilioni ili kuboresha maisha yetu”, basi Watanzania (sijui katika uzuzu wao) watamuona kama malaika fulani hivi au masihi, au “mungu” kabisa ambaye anatakiwa kuheshimiwa sana. Ili akitokea mtu kumpinga, au kumkosoa au hata kutaka kugombea ile nafasi basi mtu huyo aonekane mbaya sana mithili ya shetani!

Btw, ni wazi kabisa kuwa hii yote ni mjumuiko wa “campaign mode” ya kudumu. Tangu awamu iliyopita hawa viongozi siku zote wako kwenye kampeni za uchaguzi wakitumia rasilimali na majukwaa ya shughuli za kiserikali kujinasibu kama wao ndio wahisani wa Watanzania “wanyonge”. Kwamba wao pekee ndio “wanaoweza kuleta maendeleo” katika nchi hii. Ndio wanaoweza kutafuta na kugawa mabilioni ya miradi, ruzuku na fadhila mbalimbali!
 
Kwa hakika kuanzia wanachi wa Tanzania [emoji1241], na viongozi wameharibiwa sana na CCM.

Yani najaribu ku imagine! Pale marekani mbunge asimame aseme tunamshukuru Biden kwa kutoa pesa kwaajili ya miundo mbinu au namna yoyote ile, aiseee haiwezi tokea

Rais hana pesa za kufadhili miradi bali ni ujinga mkubwa sana kwa viongozi wetu wenye, PhD za kupewa udom( serious kidding [emoji38]). Lakini pia kutokujitambua kwa wanachi wenyewe ambao ndio walipa kodi.
Huko kwa Biden mbali hata hapo pa majirani tu waseme Ruto ametoa pesa .Wakenya wako vizuri kwenye elimu ya uraia kuliko sisi ambao mtu na akili zake anakiri hadharani kwamba eti ni chawa wa mtu fulani !Idiot
 
Mi nimechoka kujibu mambo ya kijinga labda wana JF wanaweza kutueleza.
Yani wageni wananiuliza ili
Naibu waziri wa afya ametia aibu kabisa kwa kusema Samia anajua kutafuta pesa,... Samia ametoa bilioni.....Ni hela za Samia hizi.....! Huu ni upuuzi mkubwa unaofanywa na mazuzu huko CCM.
 
Back
Top Bottom