Ikiwa wewe ndiye Masikini zaidi kati ya ndugu zako, epuka mikusanyiko ya Kifamilia

Sio pesa tu mim nimekulia familia ambayo watoto wa kiume wana thaman sana sisi wa kike takataka ,vitu vizuri vyote wanatunziwa wa kiume ,wajukuu wanapendwa wa kiume kama kuku imepikwa ni kidogo inatunzwa ya wanaume nyie wa kike mle maharage
β€’ Hizo zitakuwa mila zenu mkuu, Maana hata sisi kabila letu, Mwanamke hata awe mkubwa kiasi gani, Siwezi kumuachia kiti/kigoda akae, ( labda awe mama angu wa kinizaa)

β€’ Kwa maneno uliyo Sema hapi juu, Alafu uwe maskini, πŸ€”, sijui itakuwaje??
 

Sana yaan ndugu majina tu kiukweli ukikaa mbali nao unapata amani ya moyo kabisa,mim kuna ndugu siwasilian nao kabisa na wala sikanyagi makwao
Kuna ndugu zetu zaman walikuwa wana uwezo yaan wakija bib mzaa mama anasema hawa ndio wajukuu zangu sasa [emoji23][emoji23][emoji23],pesa zimewaishia wanaishi maisha mabaya mpaka huruma wamekuwa wapoleee kama sio wao mpaka wamerudi kuish nyumba ya bib alipofariki wameuza nyumba zote
 

Nishajitegemea nna amani mno kuliko nilivyokuwa naishi na ndugu sitamani hata kwenda kuishi huko
 
Wanakuona umepoteza network kabisaπŸ€£πŸ€£πŸ˜…πŸ˜…
😁😁, Unaweza kuwa umesoma fresh, ila ukikaa zaidi ya miaka 6-7 home bila ajira , tayari unawekwa level ya umaskini na ni mtu ambaye ulienda kupoteza mda shuleni. ( kwa hiyo huna faida yeyote ile)
 
Popote unapoishi hapa duniani ndugu yako ni yule wakuzaliwa hawa wajinga wa kuitwa sijui watoto wa mama mdogo , sijui wa aunt , sijui binamu ni takataka kama watu baki fanya uwezavyo watupe nje ya mizunguko yako .

Hawanaga shukrani hata uwasaidie vipi , hawana amani na mafanikio yako zaidi wanatamani wao ndiyo wawe na mafanikio .

Oooh my God ndugu sio watu ni wabaya hawafai , usiwaweke karibu hata kwa kidogo wakimbie kama ukoma Dejane bado haunielewi ila nasisitiza nielewe mimi ndugu baki ni takakata ila hata wa kuzaliwa akileta pigo sizo tupa kule .

Ndugu wabaya wao .

Sent from my SM-J410F using JamiiForums mobile app
 
Hii nadhani inategemea na koo au familia na mtazamo wa familia au ukoo katika masuala mbalimbali ya maisha, familia yetu au ukoo wetu sisi hukutana Kila ikikaribia nusu ya mwaka, familia zote za ukoo popote zilipo pale huenda kijijini kule kwenye makutano na huandaliwa tafrija yoyote tu Ili kuchangamsha na watu hukaa vizuri na kusalimiana na kuheshimiana, tena wenye nacho Huwa wanyenyekevu sana very humble, kwetu sisi hakuna hicho kitu hivyo inategemea kama nilivyosema huko juu.
 
β€’ Tabia ya kuwa wanyenyekevu na kuheshimiana ni jambo la kupongezwa, kwani inaweza kuchangia kujenga mazingira mazuri ya kijamii na kuimarisha udugu.

β€’ lakini kuna baadhi ya koo/familia bila kuwa na pesa, ni hali ya mateso sana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…