Ikiwa wewe ndiye Masikini zaidi kati ya ndugu zako, epuka mikusanyiko ya Kifamilia

Wapelekee moto wa kuzimu kabisa , washenzi sana
Mtu ambaye anakutreat kama mtu ukiwa na kitu halafu anakutreat kama takataka ukiwa huna kitu ,huyo hakufai , hata kama ni mzazi wako
Ni kumuonyesha ukauzu mpaka siku anaingia kaburini huko asikusahau kabisa
 
Ukiona hivyo kaa ukijua huna ndugu ,bali una ndugu jina tu
Mimi ndugu yangu ni mtu ambaye yuko tayari kupita na mimi kwenye magumu ,taabu na raha na si hawa kupe wa kujipendekeza wakati una kitu
 
Wanapata pesa bila kuwa na elimu ya utu ndo shida.
Hii ndo shida ya muafrika,weupe uwakuti wakilumbuka pesa
Na ndio wanafanikiwa sana , angalia hata asians hao wahindi ,waarabu na wachina , ni jamii za watu ambao wamefanikiwa sana kibiashara ulimwengu huu na wametapakaa kila kona ya dunia , siri ni umoja ,upendo na mshikamano kwenye hizo familia na koo zao
Na hii wanafanya mpaka kwenye biashara , akianguka mmoja wanakaa na kutafakari namna ya kuokoa jahazi .
Njoo kwa mtu mweusi sasa , ni wonder Sisi watu weusi dunia nzima miaka yote tupo hivi ,hatupigi hatua
Huwezi piga hatua kwa ubinafsi na roho mbaya za kipuuzi kama za watu weusi wengi ,never
 
Na ndio maana wengine huwa mnarogwa , kuna watu matatizo huwa wanayatafuta wenyewe. Unawafanya watu dharau kisa umepata vichenji vya kubadilisha mboga , kuna vichwa gavitakubali dharau ,watakupiga kipapai ufe kibudu
Wabongo wabadilike , acheni dharau
Dharau sio nzuri kabisa
Hata Mungu hapendi dharau ndio maana wakipiga kipapai na yeye anaacha kukulinda ili upitie cha moto na ukome ulimbukeni na ujifunze jinsi ya kuishi na watu
Kuna watu maisha yao yameharibiwa na wengine hata kupoteza maisha kwa dharau , haina haja ya kutengeneza maadui unnecessary kama hivyo , jiheshimu na heshimu watu
 
Inategemeana na familia. Familia nyingine zinasaidiaa na upendo upo so kukutana inaweza kumsaidia mtu kupata connection na dili nyingine.

Kwa familia zenye majungu ni bora ujitafute kwanza maana utajiona wewe sio kitu.
Kwa familia zenye majungu ni bora ujitafute kwanza maana utajiona wewe sio kitu
β€’ Ukiangalia kwa haraka haraka, familia zote zipo hapa, Hata kama ni tumbo moja kuinuana labda wazazi wawe bado wapo hai, tofauti na hapo, nikukomaa tu.
 
β€’ 😁😁, Mkuu una hasira sana, Sisi Africa kuja kupendana ni ndoto ambazo haziwezi kutimia milele.

β€’ Mda mwingine unajiuliza tulikosea nini, mpaka tukagubikwa na roho ya ubinafsi kiasi hiki?
 
😎😎😎
 
Hii iende sambamba na wale waliooa kwenye familia zenye watoto wengi wa kike halafu ukute wewe ndio umezidiwa kipato na wenzako. Heshima huwa haipo ukweni, wanaopewa hadhi na heshima ni wale wenye hela, hii kitu inaudhi sana ukweni
Tutafuteni hela tu maana inauma sana kuona mmealikwa ukweni wewe na wanaume wenzio waliooa hapo halafu wenzako wote wanaenda na magari yao wewe unashuka na toyo vumbi mwili mzima mpaka kwenye ulimi!
Mmekaa sebureni unamuoa shemeji yako anatumia kiatu chako kuua mende[emoji38]
Hujakaa sawa unaagizwa dukani ukabebe kreti za soda begani[emoji848]
 

wenzako wote wanaenda na magari yao wewe unashuka na toyo vumbi mwili mzima mpaka kwenye ulimi!
β€’ 😁😁😁😁. Hapo hakuna tofauti na kituko sasa,

β€’ Labda uende mtoni ukapige maji kwanza, alafu ndo uelekee kwenye tukio
 
Sidhani kama ni kweli unayoyasema hapa,ubaguzi miongoni mwa wanafamilia nisuala la kizazi cha leo,ubaguzi unatokana na mwenye nacho na asiyekuwa nacho ni mkubwa mno.Mungu tu atusaidie
 
Noted broo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…