IKULU, Dar: Rais Samia na Freeman Mbowe wakutana na kufanya mazungumzo leo Mei 9, 2022

IKULU, Dar: Rais Samia na Freeman Mbowe wakutana na kufanya mazungumzo leo Mei 9, 2022

Huyu mzee muda huu wananchi wanajipambania wenyewe kuhusu bei ya petroli na mfumuko wa bei yeye kila siku anapiga piga picha tu alafu baadae uje kujiliza liza kwa wananchi.
Punguza jazba!
 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Freeman Mbowe mara baada ya kuwasili Ikulu Jijini Dar es Salaam kwa ajili ya mazungumzo tarehe 09 Mei, 2022.

View attachment 2218354
View attachment 2218392

9 May 2022
Ikulu Dar es Salaam, Tanzania

MH. FREEMAN MBOWE AFIKA IKULU TENA NA KUFANYA MAZUNGUMZO NA MH. RAIS SAMIA HASSAN

Hakika ni jambo jema kuona mwenyekiti wa CCM taifa Mh. Rais Samia Suluhu Hassan kukutana tena na mwenyekiti wa chama kikuu cha upinzani Tanzania Mh. Freeman Aikael Mbowe ikulu jijini Dar es Salaam leo tarehe 9 May 2022.

Pia Tarehe 4 Mwezi March 2022 viongozi hawa wakuu wa vyama vya siasa Tanzania walikutana ikulu jijini Dar es Salaam


 
BUNGE LA WANANCHI CHADEMA LAZUNGUMZIA KUPANDA KWA BEI YA MAFUTA NCHINI, YATOA MAPENDEKEZO KWA SERIKALI

Latoa ushauri kuhusu masuala mbalimbali yanayogusa maisha ya waTanzania kwa ujumla na kuja na ushauri wa jinsi ya changamoto hizo za kiuchumi zitatuliwe haraka wananchi wapate afuweni ya kiuchumi

  • Kupanda kwa Bei ya mafuta nchini
  • Kupanda kwa gharama za usafiri wote
  • Kupungua kwa mapato kwa serikali kwani wananchi watashindwa kufanya manunuzi yasiyo ya lazima
  • Mfumuko wa bei
  • Athari ktk maeneo mengi kiuchumi
  • Viwanda vidogo kuathirika zaidi kwani vinatumia zaidi mafuta kuendesha mitambo yake
  • Kuongezeka maradufu kwa ugumu wa maisha kwa wananchi
  • CHADEMA yatoa ushauri kwa serikali jinsi ya kukabiliana na hali hii ngumu kwa uchumi wa taifa na athari zake kwa maisha ya waTanzania ....
  • Kuondokana na uwezekano la mkwamo wa kiuchumi
  • Serikali ipunguze matumizi yasiyo ya lazima ...
  • Kutizama kwa ujumla wake mfumo mzima wa kuagiza mafuta
  • Zanzibar wameweza, Kenya wamechukua hatua kwa kutoa ruzuku n.k Kipi serikali ya Muungano inashindwa ?
Source : Mgawe TV
 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Freeman Mbowe mara baada ya kuwasili Ikulu Jijini Dar es Salaam kwa ajili ya mazungumzo tarehe 09 Mei, 2022.

View attachment 2218354
View attachment 2218392
Akiishiwa Hela tu msumbufu, anachangisha Hela za kuitisha Baraza Kuu Kila mahali
 
Mwenyekiti wa CCM A na mwenyekiti wa Ccm B wamekutana kupanga ajenda za kikao cha ccm B.
Ama kweli mwanangu kua uyaone!
 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Freeman Mbowe mara baada ya kuwasili Ikulu Jijini Dar es Salaam kwa ajili ya mazungumzo tarehe 09 Mei, 2022.

View attachment 2218354
View attachment 2218392


Mama anahitaji Chadema kusaidia hii nchi kwasasa na ndiyo maana tulisema bunge la sasa halina viongozi limejaa walalamikaji
 
Hiyo picha ya pili inaonyesha hapakuwa na jambo la furaha lililoongelewa kati ya hawa wawili.

Mbowe anajilazimisha sana aonekane kuwa na uso wa furaha, lakini wapi!

Hapa ndipo ilipo 'checkmate', ya kujua uwezo wa kiongozi ulivyo.

Mbowe, kapewa siku moja tu, au pungufu, ya kuyafikiria yaliyoongewa hapo kabla hajakabiriana na wajumbe wa mkutano wake.

Mambo mazito ni lazima ayapime, na kuyafanyia uamzi haraka. Atakapokutana na dhoruba ya wajumbe wake awe katika nafasi ya kushawishi juu ya maamuzi yatakayofanyika katika mkutano huo.

Bi mkubwa, akili yake ipo mbali kabisa, pengine kwa kukosa ahadi toka kwa Mwenyekiti Mbowe, kuyatimiza yale aliyoomba yatimizwe katika mkutano wa kesho.
Akili kubwa.
Itunzwe hii.

Sent from my SM-J610F using JamiiForums mobile app
 
Mbowe ni CCM Full stop mtanielewa 2035 !!

Nilisema Mrema ni CCM mwaka 1996 watu wakanijia juu...
Ni kawaida kabisa . Hata CCM sio Moja . Kuna CCM ya Kibepari na CCM ya Kijamaa.
Kuna CCM ya wazalendo na CCM ya wawaza magendo .
Mbowe na wengine wote ni CCM ila tofauti na CCM waliopo ni kwemba waliobaki ndani ya CCM wengi ni waoga na wawaza Kwa kupitia tumbo. Ni waoga wa aina ya Mkamia. Wakifikiria njaa inayoweza kuwakumba wanaona Bora tubanane humu humu.

Ndio maana CCM ya Nyerere sio ya CCM ya Mwinyi.
CCM ya Mwinyi sio Ile ya Mkapa.
CCM ya Mkapa sio Ile ya Kikwete.
CCM ya Kikwete sio Ile ya Magufuli.
CCM ya Magufuli sio Ile ya mama Samia.
CCM ni vyama vingi ndani ya kimoja inayotokana na woga wa kukosa maslahi yanayoshikiliwa na Mwenyekiti ambaye ni Rais Mwenye mamlaka kama ya mungu.
Ukiona mtu amejivika mabomu na kutoka nje ya CCM hata Kwa muda mfupi basi ujue huyo ni kidume. Mana lazima apate mtikisiko mkubwa na kila aina ya dhoruba kama mchawi aliyejaribu kuokoka.

Mbowe Amejaribu kuikimbia CCM mazima Sasa anapata vikwazo vingi mana anaonekana kama muasi. Katiba ya kumfanya mwenyekiti wa CCM ambaye ni Rais kuwa kama Mungu mtoa riziki kinawafanya wanachama na makada wake kuishi kama bendera inayofuata upepo.
 
COVID 19 hawaelewi wafanye nini, wahenga walisema kila mchuma janga hula na wakwao.
Hawa Covid-19 ni wabunge, ilikuwa lazima watake wasitake wenyewe. Bwana yule unafahamu wasingeweza kufanya chochote hawa Covid-19. Muulize mkamia ilibidi ajipendekeze kwa kupigia debe upresident miaka 7. Hakupenda ila alilazimika kujiokoa kwa kupinga miswada wa habari!
 
Back
Top Bottom