IKULU, Dar: Rais Samia na Freeman Mbowe wakutana na kufanya mazungumzo leo Mei 9, 2022

IKULU, Dar: Rais Samia na Freeman Mbowe wakutana na kufanya mazungumzo leo Mei 9, 2022

Nikikumbuka zile agenda za baraza kuu la Chadema tarehe 11, Katiba Mpya iko pale, naamini hata kwenye akili ya Mbowe hapo kikaoni ipo pia.
Kikosi kazi kilipendekeza mchakato wa katiba uanze baada ya uchaguzi wa 2025.

Huenda mwamba naye ameridhia hilo, ndio maana kelele zake za kudai katiba zimekwisha.
 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Freeman Mbowe mara baada ya kuwasili Ikulu Jijini Dar es Salaam kwa ajili ya mazungumzo tarehe 09 Mei, 2022.

View attachment 2218354
View attachment 2218392
Huyu anawahitaji sana CHADEMA wakati huu, kuliko CHADEMA wanavyomhitaji yeye.

Je, Mkutano huu unahusiana na mikutano ya CHADEMA itakayofanyika karibuni? Sina shaka yoyote hilo ni moja ya jambo linalotia wasiwasi kwa bi mkubwa.
 
Mbona kama ametusahau ACT ?

20220412_232713.jpg
 
Kikosi kazi kilipendekeza mchakato wa katiba uanze baada ya uchaguzi wa 2025.

Huenda mwamba naye ameridhia hilo, ndio maana kelele zake za kudai katiba zimekwisha.
Huyo Mwamba atakuwa anafanya kosa la karne akikubaliana na jambo kama hilo.

Moja ya 'pozo' anayoweza kuahidiwa, ni kuwa sehemu ya serikali. Sioni tena CCM kama ilivyo sasa kuunda serikali yao wenyewe. Tanzania inaingia kwenye siasa za kiulaghai kama zile tunazoziona kwa jirani yetu wa kaskazini.

Akina Mbowe wote na takataka nyinginezo kama ACT, wote wanasombwa serikalini kuzima huu upepo unaovuma.

Hatujui hao wengine wanaosemwa kuanzishwa karibuni. Ngoja tusubiri wakijitambulisha.
 
Hiyo picha ya pili inaonyesha hapakuwa na jambo la furaha lililoongelewa kati ya hawa wawili.

Mbowe anajilazimisha sana aonekane kuwa na uso wa furaha, lakini wapi!

Hapa ndipo ilipo 'checkmate', ya kujua uwezo wa kiongozi ulivyo.

Mbowe, kapewa siku moja tu, au pungufu, ya kuyafikiria yaliyoongewa hapo kabla hajakabiriana na wajumbe wa mkutano wake.

Mambo mazito ni lazima ayapime, na kuyafanyia uamzi haraka. Atakapokutana na dhoruba ya wajumbe wake awe katika nafasi ya kushawishi juu ya maamuzi yatakayofanyika katika mkutano huo.

Bi mkubwa, akili yake ipo mbali kabisa, pengine kwa kukosa ahadi toka kwa Mwenyekiti Mbowe, kuyatimiza yale aliyoomba yatimizwe katika mkutano wa kesho.
 
Tangu atoke jela, sijasikia kongamano la katiba mpya tena. Nasikia tu vimaneno maneno kuhusu katiba mpya huku mwenye mitandao. Hivi vimaneno vya kwenye mitandao vinatosha kweli kutuletea katiba mpya?
Hujui Jambo ndio maana hufwatilii fwatilia Jambo ndio usema
 
Hata Membe leo amekuwa Ikulu ,, kabla ya Ijumaa tumepanga Zitto naye aonane na Mama !!

Mzungumzo haya Mama amemwambia Mbowe kwamba wanayafanyia kazi mapendekezo yao Lakin pia wamegusia Suala la COVID 19 Bungeni

Pia kuna mtu anakula kitengo soon
Babu Duni kashaonana na Mama tokea Tarehe 5 alienda kujitambulisha
 
Mbowe ni CCM Full stop mtanielewa 2035 !!

Nilisema Mrema ni CCM mwaka 1996 watu wakanijia juu:

Nikaandika hapa kwamba Dr SLAA ni CCM ilikuwa mwaka 2009 na kadi yake ilikuwa imelipiwa hadi 2020

Hawa wote wako Upinzani na wanaalipwa na serikali
Wa mtaani ndo utanibishia….

Britanicca
Mamkubwa shikamoo
 
Mbowe ni CCM Full stop mtanielewa 2035 !!

Nilisema Mrema ni CCM mwaka 1996 watu wakanijia juu:

Nikaandika hapa kwamba Dr SLAA ni CCM ilikuwa mwaka 2009 na kadi yake ilikuwa imelipiwa hadi 2020

Hawa wote wako Upinzani na wanaalipwa na serikali
Wa mtaani ndo utanibishia….

Britanicca
Acha uongo ina wauma kweli kweli kwasababu Zitto ni CCM ameshindwa kufanya Kazi yenu
 
Kuzaliwa bushi ukakulia mjini PhD tosha

Mbowe kutoka
---udereva BOT(kumwendesha gavana)
----UDJ wasemavo wahuni wa lumumba
----Kuonekana formsix F
--kuzaliwa Kilimanjaro /Arusha

Ndo kijana mtu wamakamo anayeshinda ndani ya ikulu ya Tz pengine kuliko wasomi wote nchini hapa na ndio kiongozi anayeipigisha kwata serikali ya ccm yooote kwasababu yakukulia mjini na kujichanganya inanikumbusha kwa Barack Obama kutoka kushinda mtaani na viatu vinabana Hadi ndani ya ikulu ya marekani na nimweusi


Mbowe salute sana
 
Back
Top Bottom