IKULU: Rais Magufuli amteua Dkt. Bashiru Ally Kakurwa kuwa Katibu Mkuu Kiongozi

I am lost ... I have decided to rest my mind for a while... May be I will understand someday
Kuna kipindi nilikuwa nafikiri Magufuli anaharibu mambo kwa ushamba tu, kwa ujinga, kwa kutojua, kwa ubishi, na kwa kutosikiliza watu.

Granted, hizo sifa nyingi kama si zote anazo.

Lakini kuna mambo mengi anafanya deliberately, kwa manipulation, Machievallian machinations, calculations etc.

Hapa naona kuna mkakati wa kukisimika chama deep kabisa kwenye civil service huko.
 
Tatizo la Bashiru ni kuacha itikadi alizokuwa anazisimamia akiwa mwalimu pale udsm na kugeuzwa mfuasi wa kuvunja Haki za binadamu kwa maslahi ya CCM.
Huoni kuwa amefanikiwa sawa na yule Benson Bana maana nayeye alikuwa mhadhiri pale mlimani lkn akijitoa sifa zilizo mfanya awe pale na mwisho wake leo hii ni balozi
 
Huyu bado ni mwalimu wa udsm

Akiacha siasa anarudi udsm, Wanamsubiri
 
Hata kama atajiuzulu Ukatibu Mkuu CCM, huu uteuzi unaonesha kwamba utumishi serikalini unaenda kupelekwa kichama chama zaidi.

Kwa hiyo siku zooote hizo hujuagi kama shughuli za kiserikali zinaendeshagwa kichama chama (Ki-CCM) zaidi?
Hilo lipo tangu enzi za Nyerere.
 
Tatizo la Bashiru ni kuacha itikadi alizokuwa anazisimamia akiwa mwalimu pale udsm na kugeuzwa mfuasi wa kuvunja Haki za binadamu kwa maslahi ya CCM.
Acha kulalama kijana,yeyote anayekuwa kinyume nanyi lazima awe adui yenu,hivi kuna mtu mwenye akili timamu anaweza kuwa na misimamo ya wafuasi wa chadema?

Kodumu chama cha mapinduzi!
 
Yale yale ya kulalamikia kila kitu!

Yeyote yule ambaye angeteuliwa na Magufuli mngemtafutia kasoro tu!

Angemteua Freeman Mbowe kuwa ndo katibu mkuu kiongozi, mngesema Mbowe kanunuliwa.

Sioni tatizo la Bashiru kuwa katibu mkuu kiongozi.

Kateuliwa kihalali na Rais aliyepo madarakani. Hata kwenye nchi zenye demokrasia zilizopevuka, viongozi wake huteua watu wa mirengo na itikadi zinazofanana na za kwao kwenye nafasi mbalimbali, zikiwemo mahakama, vyombo vya usalama, nk.

Apewe nafasi ya kufanya kazi tuone utendaji wake ukoje kabla hatujaanza kumtafutia kasoro.
 
Hongera sana mh Raisi kwakutupa mtu sahihi katika utumishi wa uma #hongera sana mh bashiru ulifanya makubwa sana ndani ya chama chetu kwakuangusha upinzani wote
 
Kwa hiyo siku zooote hizo hujuagi kama shughuli za kiserikali zinaendeshagwa kichama chama (Ki-CCM) zaidi?
Hilo lipo tangu enzi za Nyerere.
Kama ilikuwa hivyo, hakujawahi kuwapo na rais aliyefanya hilo kwa wazi kabisa kwa ngazi ya kumteua Katibu Mkuu wa Chama kuwa Katibu Mkuu Kiongozi.

Hii ndiyo mara ya kwanza mnaambiwa wazi kabisa kwamba "utumishi wa umma unaenda kuongozwa na kada wa juu kabisa wa chama sasa"
 
Mkuu,

Unalalamika kwamba mimi nalalamika sana.

Lakini wewe unanizidi kulalamika.

Unalalamika kwamba nitalalamika kuhusu vitu ambavyo sijalalamikia bado!

Kama vile umekuwa time traveler uliyeenda katika alternate universe na kuona nalalamika halafu ukarudi hapa kutoa ripoti.

Stick to the facts please.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…