..hivi mnashangaa nini?
..mbona hakumshangaa wakati wana-ccm wakishangilia Tundu Lissu kupigwa risasi?
..mbona hamshagai wanaofurahia kuwa sasa Tundu Lissu ana mguu mmoja mfupi, amekuwa mlemavu?
..mbona hamkushangaa Katibu Mkuu wa CCM aliposema Tundu Lissu anadeka? Au Naibu Waziri Waitara aliposema ndani ya bunge kwamba Tundu Lissu alistahili "kutangulizwa"? Au Raisi Magufuli alipodai jimbo la Singida Mashariki lilikuwa limetelekezwa?
..hata mtoa mada
Nyani Ngabu amekuwa kinara wa kumcheka na kumbeza Tundu Lisuu, akidai kuwa anavaa " raba mtoni . "
..mtoa mada ndiye kinara wa kubeza na kuchekelea wapinzani wanapofikwa na matatizo / balaa, halafu anashangaa baadhi ya waTz kuwa na chuki na upande anajinasabisha nao.
..haya yanayotokea ni matokeo ya UKATILI na DHULUMA wanazofanyiwa viongozi na wafuasi wa vyama vya upinzani.
NB.
..sijui kama unakumbuka alichokisema Mwalimu Nyerere kuhusu Wanyarwanda waliokuwa Mwanza, waliofurahia tukio la kuanguka / kuangushwa kwa ndege iliyombeba Raisi Habyarimana.