Ikulu ya Chamwino: Nani hasa anastahili credits?
Ndio imejengwa na Samia kwa sababu yeye ndo ameikamilisha kuijenga.

Kwa hata huyo JPM si alikuta miradi iliyo anzishwa na kikwete yeye akaja kuimalizia akaita ni ya kwake?
Kama JPM amekamilisha miradi iliyoanzishwa na Kikwete, iweje miradi ya Samia iliyoanzishwa na Magufuli asitajwe wakati Kikwete katajwa na hajaanzisha huo mradi wa Ikulu? Uwe unatumia akili kwenye hija zako mkuu. Au imejaa ujii??
 
Magufuli na mapungufu yake yote lakini kwenye mambo ya miradi ya ujenzi anastahiki kila sifa. Hakuna mpuuzi yeyote aliweza kufanikisha theluthi moja ya yale aliyofanya Magufuli kwa miaka 6.

Ila hata wasipomtaja uliwmengu wote unajua nini hasa alichofanya katika kutengeneza hii nchi.
Mchango wake tunaujua hata wakifunika funika. He is one of the best things to ever happen in Tanzanian history and Africa at large.
 
Mimi nilisema tangu jana humu, hawaweze kumuweka hata kidogo.


Ila uzuri kwa dunia ilipofikia ni ngumu sana kuwadanganya watu, kila sehemu kunakorushwa hizo taarifa jina la MAGUFULI limeandikwa kwa karibia 90%.

Huwezi kuzinyonga juhudi za mtu.
 



Endeleeni na kampeni yenu kupigana na Marehemu. Lakini lakini hata Mawe yanajua kwamba ni Marehemu John Joseph Pombe Magufuli.

Alieamua kwa uthubutu mkubwa,kwa uzalendo mkubwa na kwa ujasiri wake...

Kwamba sasa Serikali inaenda Dodoma na Ikulu ianze kujengwa mara moja! Huo ndio ukweli halisi na historia haitabadilishwa kwa njama za mabazazi wachache wa kisiasa na wasakatonge wao!

Haya mengine ni unafiki jazz band ya Msoga Gang & Chawa wa Mama!
Imetoka hiyo!
Ikulu imejengwa kwa kodi zetu,tuondoleeni kelele.za huyo dhalim wenu
 
Hivi watz mtaacha lini upumbavu wa kutilia maanani vitu vidogo vidogo visivyo na faida kwenye maisha yenu na taifa kwa ujumla?

Kwani jina la Magufuri linge tajwa nchi ingeingeza bilion ngapi na baada ya kutotajwa nchi imepata hasara na billion ngapi?
Nchi kupata au kutokupata hasara kunaingiliana vipi na hoja iliyopo hapa?

Hizo hasara kila siku zinatokea nchi hii.
 
Hivi Magufuli huyu mama alimwokota wapi? Si angemteua hata Jecha kuwa mgombea mwenza wake? Inashangaza sana!
kweli magufuli alikuwa na maadui hatari[emoji116][emoji116][emoji116][emoji116]
 
Ndio imejengwa na Samia kwa sababu yeye ndo ameikamilisha kuijenga.

Kwa hata huyo JPM si alikuta miradi iliyo anzishwa na kikwete yeye akaja kuimalizia akaita ni ya kwake?
Huna lolote unalolijua wewe,hatua zote za upatikanaji wa eneo la kutosha kuijenga hiyo ikulu umefanyika chini ya JPM, msingi wa ujenzi wa hiyo ikulu umeanza chini na JPM, JPM kaenda kaanza kuitumia hiyo Ikulu tangu ikiwa bado haijakamilika kamilika.


Vurugu zote za kuhamishia ofisi za kiserikali Dodoma zimefanyika chini ya JPM, huku nyinyi haohao mkumtukana kuwa anajihangaisha na kupoteza pesa.


Hiyo ikulu kipindi jamaa anaidhinisha pesa ya ujenzi, sio nyinyi mlisema amekurupuka na kwamba hamna sababu ya kujenga ikulu nyingine?
 
Mimi nilikuwa na shukran na Kikwete, uliza wakongwe wa JF ilikuwa patachimbika hapa ukimtukana J.K kila zama na kitabu chake.

Muda wake umeisha na yeye alikuwa na mazuri na mabaya yake fine ndio siasa za africa kutesa kwa zamu.

Umeshamaliza muda wako pumzika basi Msoga waache na wenzako waendeshe nchi wanavyojua wao, walete maendeleo wanavyojua wao.

Nilipoona sio muungwana na mtu mwenye tabia za narcissistic kila saa anataka atokee kwenye media ndipo nilipoanza kumuona wa ovyo; ndugu watu wakikupigia picha nyumba aliyo mnunulia binti yake Mwanaisha na mumewe Albert Marwa nje ya London ndio utajua huyo mtu ana mihela.

Waafrica wanaelewa ndio culture yetu watu wakipata madaraka, tosheka basi; ata Lowassa’s wanawashinda Regina Lowassa ubunge viti maalum aliwaambia CDM kuna mtu ana stahili hiyo nafasi kushinda mimi mpeni; yeye yupo sawa. Sio Kikwete’s baba mtu ana self grandiose syndrome kutwa kwenye media mimi hivi mimi vile, enzi zangu sijui ilikuwa hivi, ndio nikaamua kufanya abc kila siku tumechoka story zake; mama mtu tamaa ubunge wa nini Salma Kikwete.

Funny enough ni mzazi mzuri watoto zao wote wanajitegemea wenyewe, sasa nini tena anataka zaidi ya kuacha Tanzania iende yenyewe na vyombo vyake; yeye kwa no anadhani anajua what’s best for Tanzania hapo ndipo nilipoanza kumuona huyu mzee kumbe hana maana.
jpm yupo na ataendelea kuwepo[emoji116][emoji116][emoji116][emoji116][emoji116]
 
Hivi watz mtaacha lini upumbavu wa kutilia maanani vitu vidogo vidogo visivyo na faida kwenye maisha yenu na taifa kwa ujumla?

Kwani jina la Magufuri linge tajwa nchi ingeingeza bilion ngapi na baada ya kutotajwa nchi imepata hasara na billion ngapi?
Magufuli sio jina tu kama langu na lako. Magufuli ni Maono, Ni inspiration, Ni Utayari, Uthubutu, Ujasiri, Utawala, ni Mfumo na ni Itikadi pia. Yaani ni Maisha Kamili.

Waulize watawala wako kwanini wanalikwepa hilo jina.
 
Back
Top Bottom