Ikulu ya Chamwino: Nani hasa anastahili credits?
Mie ata sijui sukuma gang ni hakina nani; interest zangu ni kuona mlalahoi anapata nafuu katika maisha.

Muda wenyewe wa kuishi Tanzania wastani ni miaka 65, kuna watu toka wanazaliwa mpaka wanaaga dunia kunywa soda tu ilikuwa ni luxury katika uhai wao; now that is sad.

Wakati mijitu inagawa mali za nchi ovyo, inawakaba na mitozo watu maskini, kuiba hela zao zilitengwa kuwaletea maendeleo na kupewa viongozi wasio na maono.

Hiko ndio kinachokera yaani kula chips kuku tu mtu anapiga picha ya kuringishia. Walau Magufuli alikuwa na huruma na hawa watu na kujaribu alivyoweza kuwapa unafuu.
Kabisa kabisa !
 
Kuna nguvu kubwa sana inatumika kujaribu kumficha Late Magufuli but ukweli wanaujua wananchi waliokuwa wanateseka kabla hajaongoza nchi.

Hawa hata kama atafichwa vipi still wanaujua umuhimu wake,hatutegemei mtu kama zuhra au yeyote yule aliyeko kwenye circle ya serikali ya leo amtaje Magufuli kwa zuri maana siye anayemlipa.

NB;mimi siyo mwanasiasa ila naongea uhalisia ulivyo.
JPM kaanza kuishi kwenye hiyo ikulu hata kabla haijaisha (bado ni mapagare tu), tena alikua anakaa hata miezi kabisa kuonyesha ni kiasi gani alikuwa determined kuhakikisha alichokianzisha kinaisha, wakawa wanamcheka leo kimekamilika hahao tena wanakiona kilikuwa na maana.
 
Tatizo lenyewe mafisadi ni vilaza they just don’t know that, ni mijitu mihuni inayoishi kwenye dunia yao.

Ndio kama topic ya hii mada; unaweza kweli kuongelea Ikulu ya Chamwino bila ya kumtaja aliejenga, halafu wananchi wasiulize kulikoni.

Wana tabia ya kujiongopea na kuishi kwenye uongo wao.
You nailed it !
 
Clip imetengenezwa kipindi Mama yuko madarakani, ina vinasaba vingi vya ushawishi kutoka kwa mama.
Ni clip ambayo haina mpangilio. Bwana tambaza, mama nyerere, yule katibu mkuu kiongozi. Hata mwinyi, hajaongea vizuri. Ni clip iliyolenga tu ionekane kwamba kuna documentary ina watu hawa. Ila lengo lifike kwa mama mwenye nchi na isifie. Very bad clip ile. Naumia sababu itabaki kwenye rekodi na ikiwa na lengo la kumsifia mtu mmoja tu. Wameikata kata sana.
 
Mwalimu Nyerere,ndio mwanzilishi,na alishiriki mpaka kuchimba mitaro,kupeleka maji hapo,Chamwino,alikaa kwenye kambi hapo,karibia miezi mitatu,na hakuwa na ulinzi mkubwa .
Baada ya Mwl Nyerere nini kikaendelea kwa maraisi wengine?

Ofisi za serikali kuhamia Dodoma ilikuwa ni vision ya NYERERE, hakuna anae kataa. Ila utekelezaji wa hiyo vision umekuja kufanyika awamu ya tano.
 
Mimi nilikuwa na shukran na Kikwete, uliza wakongwe wa JF ilikuwa patachimbika hapa ukimtukana J.K kila zama na kitabu chake.

Muda wake umeisha na yeye alikuwa na mazuri na mabaya yake fine ndio siasa za africa kutesa kwa zamu.

Umeshamaliza muda wako pumzika basi Msoga waache na wenzako waendeshe nchi wanavyojua wao, walete maendeleo wanavyojua wao.

Nilipoona sio muungwana na mtu mwenye tabia za narcissistic kila saa anataka atokee kwenye media ndipo nilipoanza kumuona wa ovyo; ndugu watu wakikupigia picha nyumba aliyo mnunulia binti yake Mwanaisha na mumewe Albert Marwa nje ya London ndio utajua huyo mtu ana mihela.

Waafrica wanaelewa ndio culture yetu watu wakipata madaraka, tosheka basi; ata Lowassa’s wanawashinda Regina Lowassa ubunge viti maalum aliwaambia CDM kuna mtu ana stahili hiyo nafasi kushinda mimi mpeni; yeye yupo sawa. Sio Kikwete’s baba mtu ana self grandiose syndrome kutwa kwenye media mimi hivi mimi vile, enzi zangu sijui ilikuwa hivi, ndio nikaamua kufanya abc kila siku tumechoka story zake; mama mtu tamaa ubunge wa nini Salma Kikwete.

Funny enough ni mzazi mzuri watoto zao wote wanajitegemea wenyewe, sasa nini tena anataka zaidi ya kuacha Tanzania iende yenyewe na vyombo vyake; yeye kwa no anadhani anajua what’s best for Tanzania hapo ndipo nilipoanza kumuona huyu mzee kumbe hana maana.
Inferiority complex !!
 
Baada ya Mwl Nyerere nini kikaendelea kwa maraisi wengine?

Ofisi za serikali kuhamia Dodoma ilikuwa ni vision ya NYERERE, hakuna anae kataa. Ila utekelezaji wa hiyo vision umekuja kufanyika awamu ya tano.
Tamisemi na ofc ya PM zilishakuwepo Dom kabla ya Ngosha wenu.
Na ht wizara zilizohamia Dom wakati wa Magufuli walipewa ofc UDOM iliyojengwa enzi za JK.
So uhamiaji Dodoma haukuanza kwa Ngosha wenu
 
Hata magufuli enzi za uhai wake alipokuwa akizindua miradi mbali mbali iliyoasisiwa na watangulizi wake alikuwa akitajwa kuwa ni yeye ndiye kaijenga. Kwahiyo tuache nongwa..Tumwache Samia achape KAZI na KAZI iendelee!
 
Hakuna namna inabidi mkubali na kuvumilia maumivu. Kwa mujibu wa utamaduni wa CCM na katiba ya JMT, Rais aliyeko madarakani ndiye hupewa sifa zote kwa kazi zote za serikali. Muwe na subira huenda zamu yenu ya kusahihisha data itawadia.

Waliopita huwa hawana chao huko. Tena wanaweza kusukumiwa lawama za matatizo yote makubwa ya taifa: upigaji; ufisadi; ubaguzi; madawa ya kulevya; ushoga, inflation, you name it. Tena mtangulizi aliyedead ndio kabisa, na lake halipo! Anapuuzwa. Ndio uhalisia wa CCM huo na katiba ya JMT wanayoikumbatia sana.
 
Magufuli ni dubwana gani kama sio shetani aliyekuja kwa sura ya mtu?
Shetani hajawahi kuwepo ni upofu wenu tu na kudanganywa na hao waliowaletea utapeli wa Yesu na Muhammad.

Mchukie MAGUFULI, lakini usitafute uhalali wa kufanya hivyo kwa kutaja jina la Yesu au Muhammad, hatuyaogopi.
 
Back
Top Bottom