Ikulu Yaita Waandishi Wa Habari kuwaonesha Hati Ya Muungano

Ikulu Yaita Waandishi Wa Habari kuwaonesha Hati Ya Muungano

nakumbuka Pasco aliwahi kuitafuta hati ya Muungano hadi huko UN akaikosa..hii imetoka wapi?
 
Last edited by a moderator:
Hoja ya hati ya Muungano ni hoja muflisi kwa kweli.. sijui kwanini watu wasomi wameing'ang'ania hii! Hivi uhalali wa Muungano unategemea uwepo wa haki ya Muungano? Je kama cheti cha ndoa au pete ya ndoa imepotea ina maana ndoa haina uhalali? Hivi uhalali wa mkataba wowote unategemea uwepo wa nyaraka za mkataba huo hasa kama pande zote zinakubaliana kuwa mkataba ulisainiwa na ushahidi wa watu kusaini na yaliyomo mwenye hiyo hati yanajulikana?

Mkuu Mwanakijiji usijidhalilishe kiasi hiki kati ya waliokuwepo wakati huo wamekana kuiona hiyo hati sasa na wewe unatuletea hadith za kusadikika eti Unalinganisha ndoa na suala la Huu muungano umetia aibu kuleta hoja mufilisi za CCM
 
Weka picha basi, au ndo unaendeleza mashindano ya kuwahi kuanzisha uzi halafu ukitegemea wenzako waje kujazia magepu?
 
hoja ya hati ya muungano ni hoja muflisi kwa kweli.. Sijui kwanini watu wasomi wameing'ang'ania hii! Hivi uhalali wa muungano unategemea uwepo wa haki ya muungano? Je kama cheti cha ndoa au pete ya ndoa imepotea ina maana ndoa haina uhalali? Hivi uhalali wa mkataba wowote unategemea uwepo wa nyaraka za mkataba huo hasa kama pande zote zinakubaliana kuwa mkataba ulisainiwa na ushahidi wa watu kusaini na yaliyomo mwenye hiyo hati yanajulikana?

wewe kijana hebu kaa utulie hii ngoma unpoicheza sharti mabega yawe kimzambazi.
Hati ni kielelezo thibitishwa kisheria pale kunapotokea mkanganyiko wa sinto fahamu baina ya pande zinazo pingana.
Unapoongelea mfano wa ndoa lazima utambue na sheria zake,
katika taratibu za mikataba ya miungano ya mataifa mbalimbali lazima nyaraka zitunzwe ili pale zinapohitajika zitumike.
Mfano .u.s.a ile nyaraka ya muungano wao ipo na inatunzwa.
 
Hoja ya hati ya Muungano ni hoja muflisi kwa kweli.. sijui kwanini watu wasomi wameing'ang'ania hii! Hivi uhalali wa Muungano unategemea uwepo wa haki ya Muungano? Je kama cheti cha ndoa au pete ya ndoa imepotea ina maana ndoa haina uhalali? Hivi uhalali wa mkataba wowote unategemea uwepo wa nyaraka za mkataba huo hasa kama pande zote zinakubaliana kuwa mkataba ulisainiwa na ushahidi wa watu kusaini na yaliyomo mwenye hiyo hati yanajulikana?

si halali ndo maana kaulizwa swali huyo katibu mkuu kama hiyo hati iliridhiwa znz kajibu yeye kazi yake ni kuonyesha hati
 
Hiyo ni feki ingekuwapo lukuvi, kikwete, wasira, nape wasingekaa kimya ila baada ya kuitengeneza wamemtuma wasira aseme kwanza alafu wao waitoe.
Nahodha na Tume walinyimwa kwa nini?
 
Sii ipelekwe dodoma?siyo kuonyeshwa tuu bali tupewe tuone imeandikwa nini
 
Taarifa nilizozipata muda huu ni kuwa Waandishi wa habari wameitwa Ikulu na Katibu Mkuu Kiongozi lengo ni kuwaonyesha Hati Ya Muungano na kukata mzizi wa Fitina Kwa wajumbe wa bunge la Katiba. Tutawajulisha hapa hapa...
Kwenye mambo ya msingi kama haya Ikulu hukaa kimya ila ukigisa jambo binafsi la wana ccm watakuja haraka na waraka
 
Monday, April 14, 2014

Hati Halali ya Muungano hii hapa ikiwa Imesainiwa ORIGINAL na Rais Nyerere na Rais Karume,Hakuna Uchakachuaji hapa




‪#‎HABARI‬ Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue ameonesha hati ya muungano wa Tanzania, kati ya nchi ya Zanzibar na Tanganyika.

Balozi Sefue amewahakikishia Watanzania kuwa nyaraka hizi muhimu ziko salama ila hakuna haja ya kujua ziko wapi.

Balozi Sefue amesema wanaosema kuwa hati hazipo na sahihi zake ni za kughushiwa, ni waongo.
Mambo 11 waliyokubaliana viongozi, wakati Zanzibar na Tanganyika zinaungana pia yameonekana katika hati ya Muungano.



BlL3iXXIcAAc_v6.jpg:large



Hii ndio

hati halali ya Muungano iliyosainiwa na Rais nyerere na Abeid Karume,.Hati yote nitaiweka hapa Soon.


Source: Habari Kwanza
 
Mbona hata hapo kwenye hii hati ya kuchonga Tanganyika wameitaja, halafu sasahivi tunataka kuifukia shimoni.
 
Taarifa nilizozipata muda huu ni kuwa Waandishi wa habari wameitwa Ikulu na Katibu Mkuu Kiongozi lengo ni kuwaonyesha Hati Ya Muungano na kukata mzizi wa Fitina Kwa wajumbe wa bunge la Katiba. Tutawajulisha hapa hapa...

Hapo ndio Ikulu inapoonekana ni wasanii, kwa uelewa wangu hati hiyo inayoitwa ya muungano iliombwa siku nyingi na wajumbe wa katiba ili iwe reference kwa ajili ya mchakato wa huu wa katiba na hasa katika kipindi wabunge walipokuwa wanakaa kwenye kamati zao, sasa leo kuita waandishi wa habari na kuonyeshwa au kupewa hati hiyo ina mantiki gani hapa hata kama ni kweli hati hiyo ipo kwa nini basi hawakupewa hawa jamaa wanaotuwakilisha kwenye mchakato wa katiba?, waandishi wa habari kwanza walikatazwa hata kuhudhuria vikao vya hizo kamati au ndio kusema wandishi wetu wanaonyeshwa hiyo hati watatoa reference huko bungeni?.........IKULU ACHA USANII
 
Wachache ndo walisema hati haipo sasa weng wamewajibu ipo wachache hawakuamin sasa serikali imeona iweke bayana kwa w/habar maneno mengine tena yanazuka hivi tutafika kweli.serikali haikusema itawapelekea wabunge ila mjumbe Wasira ndo alitoa ahad hiyo xo tumsubiri izo siku 2 akishindwa bac tuanze kujenga hoja sasa sio sasa wandugu.
 
Back
Top Bottom