Replica
JF-Expert Member
- Aug 28, 2017
- 1,681
- 8,887
Leo Magufuli aliweka kituo kidogo Ikungi wakati anatoka Dodoma ambapo wananchi walisimama barabarani kumsubiri akiwa anaelekea kwenye mkutano wa kampeni Singida. Pamoja na ahadi nyingine pomoni, pia amemuahidi mgombea mwenzake anaetokea Singida nafasi ndogo ya kazi kwa madai kwamba hii anayopambania hatoiweza.
"Mmoja wa wagombea nafikiri anatoka hapa (Singida) nishaurieni tu kwamba mimi mnipe kura nyingi yeye nitamtafutia kikazi kidogo dogo huko serikalini. Ni mtoto wetu tunampenda, wala hatuna tatizo na mimi ndugu zangu sina tatizo na mtu yoyote, kwani kazi lazima uwe Rais. Muachie Rais Magufuli wewe tutakupa kikazi unachoweza kufanya (Ikungi oyee)
Kwa sababu sisi wote ni wamoja, akija mwambieni kwamba Magufuli amesema atakupa kazi, kwa nini unahangaikia hii kazi ambayo hutashinda." Mwisho wa kunukuu.