Uchaguzi 2020 Ikungi: Magufuli amuahidi Lissu kazi, amuambia aachane na Urais ambao hatashinda

Uchaguzi 2020 Ikungi: Magufuli amuahidi Lissu kazi, amuambia aachane na Urais ambao hatashinda

CCM wamefanya kampeni peke yao tangu 2015 huku wapinzani wakiishia kuandamwa na polisi pamoja na kesi mahakamani.

Lakini leo hii baada ya miaka mitano, CCM wanaiogopa CHADEMA kwa njia zifuatazo:

1. Kuzuia vyombo vya habari kurusha matangazo yanayohusiana na Kampeni za CHADEMA. Hapa simaanishi TBC tu, ni vyombo vyote kama vile tv, redio na magazeti isipokuwa blogs na online tvs.

2. Kuandaa mechi za mpira na matamasha ya wasanii ili kuwarubuni watu wasiende kwenye mikutano ya CHADEMA.

3. Kuwaengua wagombea wa upinzani bila hoja za msingi.

4. Polisi kuwapa kesi wagombea wa upinzani pamoja na kuwashikilia masaa machache kabla ya kurudisha fomu za uteuzi ili wakose sifa baada ya muda kuisha.

5. Kubadilisha matumizi ya viwanja na maeneo yaliyo wazi, mfano, huko Serengeti.

6. Raisi Magufuli kumuahidi ajira Tundu Lissu (kikazi kidogokidogo) huku akijinadi kuwa Lissu anahangaika bure hatashinda! Amejuaje hatashinda? Angekuwa anamjali, angetoa pesa za matibabu wakati alipopigwa risasi.

Screenshot_20200901-132626.png

CCM msiombe AMANI wakati hakuna HAKI. Ruhusuni vyombo vya habari viwe LIVE kwenye mikutano ya wapinzani kama mnavyokuwa LIVE kwenye mikutano yenu.

Pia wasikate matangazo maana hata ninyi mkiwa live, matangazo hayakatwi.

MWAGENI SERA ZENU, HALAFU OKTOBA TUTAFANYA UAMZI NANI TUMPE KITI.
 
Walifungia mikutano wakajipa moyo CDM imekufa ile wameruhusu wazalendo wa kweli wako palepale wameanzia pale walipoishia 2015 baada ya Dictator kuamua asikike yeye tu.
 
Kuliko udhalilishaji kwa umaskini na maisha yako bora unyanyaswe kwa mambo mengine, Mzee leo kawaambia Singida kuwa atawapa kazi ndogondogo maana hawana nguvu ya kuwa na mgombea wakuingia Ikulu.

Kwanini tumepaniki kiasi hiki? Hatukujipanga kufanya kampeni? Eleza sera zako acha wananchi wachague siyo ueleze Mambo binafsi.
Hahahah kati ya Lissu na JPm nani aliyepaniki?

Hadi leo Lissu hana hata anayoenda kufanya yeye ni kutukana na kulalamika tu kwa Magufuli hahhahaha bora asubiri hiko kikazi kidogo kuliko kujisumbua na kumaliza mafuta ya gari bure tu

Sent from my Infinix X650 using JamiiForums mobile app
 
Anahitaji akaongozwe kwa sala ya toba.

Akatubu kwanza, kisha amwombe msamaha kwa madhila yote, awaombe msamaha wote aliyodhuru maisha yao, kwa mambo aliyokwishaonywa(na Che Nkapa) kuwa ni dhami ya ukandamizaji. Ndio arudi tuongee. Amen
 
Anaanza kuomba Po,hicho kimbunga safari hii anacho.Tumechoshwa na ulaghai wa sisiem.
Tatizo la upinzani hawana watu vijijini, hawana mawakala wa kusimamia kura zao vijijin kwa hiyo upinzn wataporwa kura zao tu.
 
Kuliko udhalilishaji kwa umaskini na maisha yako bora unyanyaswe kwa mambo mengine, Mzee leo kawaambia Singida kuwa atawapa kazi ndogondogo maana hawana nguvu ya kuwa na mgombea wakuingia Ikulu.

Kwanini tumepaniki kiasi hiki? Hatukujipanga kufanya kampeni? Eleza sera zako acha wananchi wachague siyo ueleze Mambo binafsi.
Hiyo ndiyo kweli, tl hatamshinda magu
 
Hahahah kati ya Lissu na JPm nani aliyepaniki?

Hadi leo Lissu hana hata anayoenda kufanya yeye ni kutukana na kulalamika tu kwa Magufuli hahhahaha bora asubiri hiko kikazi kidogo kuliko kujisumbua na kumaliza mafuta ya gari bure tu

Sent from my Infinix X650 using JamiiForums mobile app
Tupe sample ya matusi anayotukana lissu? Babu yenu hii roho nzuri kaanza lini wkt yeye ndo aliyeshinikiza lissu asipewe hela ya matibabu?
 
Back
Top Bottom