Uchaguzi 2020 Ikungi: Magufuli amuahidi Lissu kazi, amuambia aachane na Urais ambao hatashinda

Uchaguzi 2020 Ikungi: Magufuli amuahidi Lissu kazi, amuambia aachane na Urais ambao hatashinda

Duh!? Magufuli anaakili sana, hapo kaishamwambia mwezie anamapungufu na hawezi kabidhiwa nchi.

Kweli ukiwa na akili sentesi moja tu, inatosha kufikisha ujumbe mzito.
 
Leo Magufuli aliweka kituo kidogo Ikungi wakati anatoka Dodoma ambapo wananchi walisimama barabarani kumsubiri akiwa anaelekea kwenye mkutano wa kampeni Singida. Pamoja na ahadi nyingine pomoni, pia amemuahidi mgombea mwenzake anaetokea Singida nafasi ndogo ya kazi kwa madai kwamba hii anayopambania hatoiweza.

"Mmoja wa wagombea nafikiri anatoka hapa (Singida) nishaurieni tu kwamba mimi mnipe kura nyingi yeye nitamtafutia kikazi kidogo dogo huko serikalini. Ni mtoto wetu tunampenda, wala hatuna tatizo na mimi ndugu zangu sina tatizo na mtu yoyote, kwani kazi lazima uwe Rais. Muachie Rais Magufuli wewe tutakupa kikazi unachoweza kufanya (Ikungi oyee)

Kwa sababu sisi wote ni wamoja, akija mwambieni kwamba Magufuli amesema atakupa kazi, kwa nini unahangaikia hii kazi ambayo hutashinda." Mwisho wa kunukuu.

Huyo jamaa ni mshamba tu.

Kwa imani yake anaamini hata Nyerere (rip) hakufaa kuwa rais Ila yeye.

Akisikia baba lao anadhani hata kina Obama kwake watoto wadogo.

Kwa kweli Mkapa (rip) alitukosea sana 2015!
 
Jibu swali la Lissu....who wants to kill him? why?
 
Hiyo ni rushwa! Unamwomba mtu ajitoe kwenye uchaguzi kwa ahadi ya kumpa kazi ukishinda?! Wapi TAKUKURU?!
 
JPM Lissu ni mwanasheria na werevu mno wa mambo mengi; unapotoa shambulizi kwake jipange vilivyo; vinginevyo utajiingiza kwenye shida..

Haya sema sasa ni nani aliyempiga risasi 16 na nani aliyemyima hela za matibabu!!
 
Tumemsikia wenyewe Rais Magufuli akiwa katika kampeni zake, akiwa huko Ikungi mkoani Singida, akitamka kuwa kuna mgombea mmoja wa Urais mkoani humo ( Ingawa hakumtaja kwa jina, lakini ni dhahiri alikuwa amemlenga Tundu Lissu) akasema kuwa hawezi kushinda mbio hizo za Urais na akawaomba wananchi hao wampe salaam kuwa kura zote za Urais atazipata yeye Magufuki na akawapa ujumbe wakazi hao kuwa wamwombe Tundu Lissu ajitoe kuwania Urais na yeye Rais Magufuli atamteua katika nafasi zake nyingi za uteuzi!

Ndipo hapo ninapojiuliza iwapo Tundu Lissu tayari keshapitishwa na Tume ya uchaguzi kugombea Urais kwa tiketi ya Chadema, hivi hii kumshawishi ajitoe katika mbio hizo za Urais ili amteue katika nafasi za uteuzi, je hiyo siyo njia mojawapo ya ushawishi wa rushwa, ambayo yeye Rais Magufuli anatueleza sisi wananchi kuwa anapambana nayo kwa nguvu zote?

Jibu unalo mwananchi utakayeisoma mada hii
 
Ni kama tu ilivyotokea kwa kina Dr Mollel, M wita Waitara, na waunga juhudi wote. Hivyo lisu akiwa mwepesi kama waunga juhudi wengine tutampoteza na kisha kumuona akiwa ndani ya bustani ya mbogamboga kama Patrobas Katambi
 
Ni kama tu ilivyotokea kwa kina Dr Mollel, M wita Waitara, na waunga juhudi wote. Hivyo lisu akiwa mwepesi kama waunga juhudi wengine tutampoteza na kisha kumuona akiwa ndani ya bustani ya mbogamboga kama Patrobas Katambi
Lakini kwa kumiminiwa risasi zote zile 16, sidhani kama atalainika kwa hivyo vishawishi!
 
Tumemsikia wenyewe Rais Magufuli akiwa katika kampeni zake, akiwa huko Ikungi mkoani Singida, akisema kuwa kuna mgombea mmoja wa Urais mkoani humo ( Ingawa hakumtaja kwa jina, lakini ni dhahiri alikuwa amemlenga Tundu Lissu) akasema kuwa hawezi kushinda mbio hizo za Urais na akawaomba wananchi hao wampe yeye kura zote za Urais na akawapa ujumbe wakazi hao kuwa wamwombe Tundu Lissu ajitoe kuwania Urais na yeye Rais Magufuli atamteua katika nafasi zake nyingi za uteuzi.

Ndipo hapo ninapojiuliza iwapo Tundu Lissu tayari keshapitishwa na Tume ya uchaguzi kugombea Urais kwa Urais kwa tiketi ya Chadema, hivi hii kumshawishi ajitoe katika mbio hizo za Urais ili amteue katika nafasi za uteuzi, je hiyo siyo njia mojawapo ya ushawishi wa rushwa, ambayo yeye Rais Magufuli anatueleza sisi wananchi kuwa anapambana nayo kwa nguvu zote?
Sasa kweli hatakama hukusoma atadarasa lakwanzaaa unamuona lisu anafaaa kitengo nyeti cha uraisi kweliii.
Mtu amejawa na jazba zilizopindukia, kuomba kurakwenyewe anatumia kama tumchague kwa razma, hajawahi shuka chini iliaombe kura atasikumojaaa.

Nivyema akaaachana na kugombea ,maaana uraisi wenyewe hapatiiii. Kwahiyo hata kumpa nafasi yoyote serikaliini Mimi siungi hojaaaa.
 
Angeanza kumkumbuka lijuakali,karanga kwanza,hizo ni ahadi sawa na kumtongoza binti,karanga wa monduli aliambiwa aunge juhudi atalipiwa madeni yake akaunga kwa mkopo ikala kwake,mbatia alihadiwa kupewa majimbo ajitoe ukawa hata udiwani apati safari hii yeye na le profesele watabakia kuwa wapenzi watazamaji
 
Lakini kwa kumiminiwa risasi zote zile 16, sidhani kama atalainika kwa hivyo vishawishi!
Hakuna yeyeto aliyewahi umizwa akaunga juhudi check waunga juhudi wote hakuna hata mmoja aliyewahi umizwa
 
Ni kama tu ilivyotokea kwa kina Dr Mollel, M wita Waitara, na waunga juhudi wote. Hivyo lisu akiwa mwepesi kama waunga juhudi wengine tutampoteza na kisha kumuona akiwa ndani ya bustani ya mbogamboga kama Patrobas Katambi
Ninavyo amini no kuwa haki Kwanza mengine yanafuata,hats anaeonekana changamoto Leo huenda wangekuwa wanakutana meza moja na kusingekuwa na Hali tunayo Iona leo.
 
Back
Top Bottom