Shukuru hata umetapeliwa hela zako safi, ukaishia kwenda kulia nyumbani kwenu.
Siku nyingine usikubali tu kuingiziwa hela kwenye akaunti yako na mtu usiyemfahamu. Ni very risky na hatari sana.
Kuna watu wanatapeliwa, na isivyo bahati njema matapeli wanatafuta njia ya kuitoa na kusafisha. Ikiwekwa tu kwenye akaunti yako, umeliwa.
Kuna hela nyingi za madili zinapigwa. Ili kuzisafisha, zinagawanywa kwenye akaunti kadhaa. Sasa baadae dili likibumba, utahenyeka mpaka ukome.
Kuna watu wanauwawa. Na matapeli wanakosa namna ya kutoa pesa isipokuwa transfer. Nani wa kumhamishia? Kanyaboya mmoja. Polisi wakifanya yao, watakukamata. Utalia na kusaga meno.
Usijaribu tena.
Kaa mbali na usiyemjua inapokuwq kwenye swala la hela.