Ila kutapeliwa kunauma wakuu

Ila kutapeliwa kunauma wakuu

Hizo si uchawi ni mind games tu...watu wanasemaga uchawi ili wasionekane wajinga coz uchawi hauna evidence...wamecheza na psychology...me ishawahi nikuta na nilifanikiwa kusanuka last minute..me Hadi gari nilipanda so ningeweza kusema nimerogwa ila ni psychology tu ikitokea hivyo unajifunza huwezi tapeliwa kizembe... sijawahi ona mtu anatapeliwa mara mbili za hivyo barabarani
Mmnh
 
Mara nyingi michongo kama hiyo ina involve watumishi wa ndani ya bank wasio waaminifu, ndio hao wanaotoa taarifa zako kwa hao waalifu walio nje ya bank , ikiwemo majina yako na kiasi cha Fedha kilicho kwenye akaunti yako, ndio maana inakuwa rahisi mtu kutapeliwa maana wahalifu tiyari Wana info zako
Mkuuu waache kutapeli wenye mabilioni wanitapeli mimi
 
Kutapeliwa huwa ni ujinga tu, na pia kinachonipa hasira zaidi ni watu kuamini kuwa ni uchawi.
 
Shukuru hata umetapeliwa hela zako safi, ukaishia kwenda kulia nyumbani kwenu.


Siku nyingine usikubali tu kuingiziwa hela kwenye akaunti yako na mtu usiyemfahamu. Ni very risky na hatari sana.

Kuna watu wanatapeliwa, na isivyo bahati njema matapeli wanatafuta njia ya kuitoa na kusafisha. Ikiwekwa tu kwenye akaunti yako, umeliwa.

Kuna hela nyingi za madili zinapigwa. Ili kuzisafisha, zinagawanywa kwenye akaunti kadhaa. Sasa baadae dili likibumba, utahenyeka mpaka ukome.

Kuna watu wanauwawa. Na matapeli wanakosa namna ya kutoa pesa isipokuwa transfer. Nani wa kumhamishia? Kanyaboya mmoja. Polisi wakifanya yao, watakukamata. Utalia na kusaga meno.

Usijaribu tena.
Kaa mbali na usiyemjua inapokuwq kwenye swala la hela.
Duuuh,🤔
 
Tatizo waliivyoniita kwa majina yangu na nikaitika tukasalimiana inaonekana ni watu familiar au wananijua mda mrefu sijui
Hizo mbinu wanazitumia sana hata kwenye simu, niliwahi pigiwa simu yule jamaa alitaja hadi jina ambalo natumia nyumbani huko mkoani, nikamuuliza mbona sijakujua ila sauti yako inafanana na ya fulani, akasema ndio yeye. Baada ya kusema vile nikawaza huyu jamaa yangu halijui lile jina la nyumbani nikakata simu.
 
Pole sana kwa kupigwa tukio, nakumbuka niliwai tapeliwa na hao jamaa mwaka 2004 nikiwa form 2 bado mdogo masikini mtoto wa watu waliniibia shenzi kabsa hawa wauni. Ilikuwa mwenge pale ilipokuwa stendi ya daladala alianza kuja mmoja akaniuliza kdgo akaja mwingine kumbe walikuwa wanajuana wale dah wakuu hawa watu wanatumia dawa usithubutu kukutana na bwana pepsi
Serious nadhani wanatumia dawa sio bure
 
Pole sana, haya mambo kama hayajawahi kukutokea au kumtokea mtu wako wa karibu, unaweza hisi ni story tu!!
Mwanangu aliwahi kutapeliwa simu katika mazingira kama hayohayo. Alikuwa akikuelezea namna alivyotapeliwa yaani haiingii akilini.

Miaka ya nyuma sana nami walitaka kunifanyia mchezo huo, nashukuru account ilikuwa inasoma frequency za fm radio😅😅
Hahahha😂😂😂
Eti frequency za FM radio
 
Hizo mbinu wanazitumia sana hata kwenye simu, niliwahi pigiwa simu yule jamaa alitaja hadi jina ambalo natumia nyumbani huko mkoani, nikamuuliza mbona sijakujua ila sauti yako inafanana na ya fulani, akasema ndio yeye. Baada ya kusema vile nikawaza huyu jamaa yangu halijui lile jina la nyumbani nikakata simu.
Wangekulamba siku hio ungelia kila sehemu
 
Back
Top Bottom