Ila ndoto nyingine zinachosha, ndoto niliyoiota usiku wa kuamkia leo imenitisha.

Tafuta hela mkuu
 
Tafuta kiongozi wako kiroho akusaidie au mzazi/ mlezi, ndugu ama mtu wa karibu unaemuamini mwenye imani kali kiroho
Itabidi nifanye hivyo ya dunia ni mengi na vita ni nyingi.
Usipuuze kuna mtu hiyo Pete inampa tabu sio kawaida kuota matukio na ukakuta umetendewa hivyo hivyo
Hii pete tangu nianze kuvaa nikiwa nimelala nayo naona mabadiliko, nilianza huu utaratibu wa kulala nayo tangu mwaka jana na nikaona utulivu umeimarika sana na kuanzia hapo sijawahi kuiacha.

Mtu alieivua ndotoni ninamjua na ni mtu ambae sina muda sana tangu nifahamiane nae, ni miezi 6 tangu tufahamiane.
 
Kuna tahadhari unapewa kupitia ndoto ndo hivyo uwezo wako wa kung'amua upo chini, kuwa nae makini huyo mtu ikiwezekana muweke mbali
 
Shukrani kwa tafsiri yako mkuu, nyeto situmii na sio muumini. Maelezo yako mengine sijui kama ipo hivyo kwa sababu sina uo mpango wa kuhitaji mtoto kwa sasa na hata hayo mahusiano hayapo.

Sikusema t-shirt nyeusi ni nyepesi, hiyo tafsiri kwa kutumia nyeusi tayari ni batili.
Msinitishe zaidi wakuu.
 
Shemeji ulikuwa umelala vibaya, Ubongo ulikuwa unakupa sign ili uamke uache kuumiza sehemu ya mwili uliyoilalia vibaya..
Inawezekana ikawa hivyo shemeji ila nahisi wananiwinda, mniombee shemeji yangu.
 
Kuna tahadhari unapewa kupitia ndoto ndo hivyo uwezo wako wa kung'amua upo chini, kuwa nae makini huyo mtu ikiwezekana muweke mbali
Huyu mtu kuna maneno huwa ananitamkia kwa kilugha na huwa sielewi kilugha chake, nikimuuliza amaanisha nini huwa anaishia kucheka tena kwa nguvu sijui huwa anamaanisha nini. Ntaanza kumuepuka maana sio mara moja kumuona kwenye ndoto.
 
Mkuu bora yako,niliwahi kuota nakimbizwa balaa na watu nawajua,
Watoto mashetani,mbwa wa kuzimu ,majoka ya ajabu na mahali napajua kabisa.
Mpaka ule usiku unaisha ulikua mrefu sana.
Niliruka ukuta mrefu ndotoni nikadondoka.
Kumbe nimedondoka toka kitandani.
Ndo ikawa escape from sorbibor yangu.
Na ndoto ikaishia hapo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn moreโ€ฆ