Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Tafuta hela mkuuUsiku ni mrefu ila ukilala na kuota ndoto za ajabu ajabu huufanya uwe mrefu zaidi. Kuna baadhi ya ndoto nikiota ni ngumu sana kuzikumbuka na hizi ndio hunipa hofu hasa nikiota ndoto mbaya.
Huwa ninapata hofu kwa sababu ndoto nyingi nisizozikumbuka huwa zina uwezekano mkubwa wa kutokea na zikishatokea huwa ndio nakumbuka tukio husika na kupata picha kuwa tukio husika niliona ndotoni kama lilivyo. Huwa nashangazwa sana na hii hali inawezekanaje nishindwe kuvuta kumbukumbu mda mfupi baada ya kuota lakini ukipita muda na nikaliona tukio nakumbuka kuwa niliwahi kuota kwenye ndoto ambayo sikuikumbuka?
Tukio la ndoto ya usiku wa kuamkia leo limenichosha, ni nafuu zaidi kwa sababu nalikumbuka, kwangu haina athari kama nisingekumbuka. Niliota hivi,
Kulikuwa na sherehe sijui ilikuwa ni yanini ila niliofanikiwa kuwaona
ndani ni baadhi ya maclass mate. Kwenye hiyo sherehe kiingilio kwa wanaume ni lazima uwe na kitambi tena kikubwa haswa na ukaguzi ulikuwa unaendelea kwenye lango la kuingia ukifika unavua saa, pete na shati unalikunja vizuri unaacha mlangoni unaingia tumbo wazi. Nikikumbuka hicho kitambi changu cha ndotoni nacheka sijui nilikipatia wapi mpaka kutembea ikawa shida, ni kile kitambi kikubwa kilichomwagikia pembeni na chini.
Baada ya kuingia ndani tulikaa kwa muda na hakukuwa na kinywaji chochote kile zaidi ya maongezi na niliowakuta, muda ulivyosogea likaanza zoezi la chakula, unanyanyuka kwa utaratibu kuelekea bufee zilipo na kupakuliwa chakula. Ilipofika zamu yangu nafika kwenye bufee hakuna sahani hata moja, mhudumu akaniomba nitafute sahani kwa waliomaliza nioshe ili niwekewe (muda huo vyakula kwenye bufee bado vimejaa).
Nilitembea kwa shida sana kutokana na kitambi changu kilichokuwa kinacheza kila nikipiga hatua na nilifanikiwa kupata sahani na kuiosha, ile nimerudi nafika kwenye bufee nanyoosha sahani niwekewe msosi naambiwa umeshachelewa chakula kimeisha (wazee wa sherehe ni chakula nadhani mnaelewa hii inavyokata), ile taarifa ya chakula kuisha ilinishtua hadi nikashtuka usingizini na ndoto ikaishia hapo.
Tukio lililotokea INAENDELEA COMMENT #1
Itabidi nifanye hivyo ya dunia ni mengi na vita ni nyingi.Tafuta kiongozi wako kiroho akusaidie au mzazi/ mlezi, ndugu ama mtu wa karibu unaemuamini mwenye imani kali kiroho
Hii pete tangu nianze kuvaa nikiwa nimelala nayo naona mabadiliko, nilianza huu utaratibu wa kulala nayo tangu mwaka jana na nikaona utulivu umeimarika sana na kuanzia hapo sijawahi kuiacha.Usipuuze kuna mtu hiyo Pete inampa tabu sio kawaida kuota matukio na ukakuta umetendewa hivyo hivyo
Hiyo sawa mkuu kwahiyo ni umasikini?Tafuta hela mkuu
Inatisha mkuuHatari sana
Kuna tahadhari unapewa kupitia ndoto ndo hivyo uwezo wako wa kung'amua upo chini, kuwa nae makini huyo mtu ikiwezekana muweke mbaliItabidi nifanye hivyo ya dunia ni mengi na vita ni nyingi.
Hii pete tangu nianze kuvaa nikiwa nimelala nayo naona mabadiliko, nilianza huu utaratibu wa kulala nayo tangu mwaka jana na nikaona utulivu umeimarika sana na kuanzia hapo sijawahi kuiacha.
Mtu alieivua ndotoni ninamjua na ni mtu ambae sina muda sana tangu nifahamiane nae, ni miezi 6 tangu tufahamiane.
Shukrani kwa tafsiri yako mkuu, nyeto situmii na sio muumini. Maelezo yako mengine sijui kama ipo hivyo kwa sababu sina uo mpango wa kuhitaji mtoto kwa sasa na hata hayo mahusiano hayapo.Wewe ni mpiga nyeto.
Ndoto yako ina tafsiri ifuatayo. Ama uiamini ama uamue kuipotezea.
Sherehe ya wenye vitambi, ina maana shughuli ya wanaume wenye uwezo wa kutia mimba. Na bahati nzuri kwa wakati huo, ulikuwa na uwezo mzuri mno ndiyo maana kitambi chako kilikuwa kikubwa kiasi cha kupata tabu wakati wa kutembea.
Uliponyanyuka kwenda kuchukua chakula ni kuamka kwenda kufanya shughuli maalum ya kuijaza kitambi. Ambayo, kwa tafsiri hapo juu ina maana unaanza mchakato wa kumjaza mwenza wako.
Umefika na kukuta sahani zimeisha. Maana yake wakati ukiwa na njaa na matamanio ya kupata mtoto, basi unafika na kukuta uwezo huo huna tena.
Unaelekezwa ukatafute sahani na kuiosha. Hii ina maana unaanza kutangatanga kutafuta msaada. Kuosha ina maana ya matibabu. Na baadae unafanikiwa kupona na kurudi sasa kutimiliza lengo lako.
Unafika unakuta chakula kimeisha. Hii ina maana hata baada ya kupata suluhisho, mwenza wako hayupo tena. Bali alishachukuliwa na wenzako waliokuwa kamili gado. Unafubaa kwa huzuni ya kumkosa.
Pete kiroho ina maana ya maagano. Na katika swala hili ina maana kuwa mwenza wako hakuona future njema nawe. Mwanaume asiye na uwezo wa kutenda kiume. Anavua pete yake na kukiachia. Kudhihirisha kuwa agano la ndoa baina yenu limetamatika.
Kuikuta juu ya t-shirt nyeusi.
Rangi nyeusi kiimani ina maana ya giza, huzuni, msiba, kukataliwa.
Na kwa mantiki ya ndoto yako, pete ya ndoa inawekwa kudhihirisha kuwa kwa huzuni mahusiano yenu yanatamatika.
Nini cha kufanya?
ACHA NYETO..
😂 huku ni kutaftiana banYaelekea una hamu ya kubeba mimba...maana huwezi kuota ukiwa na kitambi hivi hivi tu.
Sema tu usiogope msabato.Nikiongea utasema msabato wa dodoma
Kufanyaje?Nitakutembelea tena na Leo
Kukuvua hiyo Pete..Kufanyaje?
sema neno moja tu na roho yangu itapona 😅Hiii ndo shida ya kuishi mwenyewe mkuu,. Fanya uoe😃😃
Inawezekana ikawa hivyo shemeji ila nahisi wananiwinda, mniombee shemeji yangu.Shemeji ulikuwa umelala vibaya, Ubongo ulikuwa unakupa sign ili uamke uache kuumiza sehemu ya mwili uliyoilalia vibaya..
Shindwa na ulegee itakuunguza.Kukuvua hiyo Pete..
Unaona marue rueHiii ndo shida ya kuishi mwenyewe mkuu,. Fanya uoe😃😃
Huyu mtu kuna maneno huwa ananitamkia kwa kilugha na huwa sielewi kilugha chake, nikimuuliza amaanisha nini huwa anaishia kucheka tena kwa nguvu sijui huwa anamaanisha nini. Ntaanza kumuepuka maana sio mara moja kumuona kwenye ndoto.Kuna tahadhari unapewa kupitia ndoto ndo hivyo uwezo wako wa kung'amua upo chini, kuwa nae makini huyo mtu ikiwezekana muweke mbali
Kujia maombi chapSema tu usiogope msabato.
Wapi huko ?Kujia maombi chap