Kwa Heshima Kubwa niliyopewa na huu Mtandao wa JamiiForums na kwa jinsi GENTAMYCINE ninavyoupenda huu Mtandao nimeamua hii Exclusive ianzie hapa na ukiiona ina trend Kwingineko jua imekopiwa hapa JamiiForums na imetoka Kwangu Mshindi wa Jukwaa la Michezo ( Sports ) JamiiForums kwa mwaka 2022 na najua nitaendelea Kushinda mpaka nitakapochoka Mwenyewe au pale akina
Greatest Of All Time watakaposalimu Amri Kwangu Kudadadeki.
Sasa naanza.....
Ukweli ni kwamba wala Mchezaji Fei Toto ( Feisal Salum ) hatakowi na sijui Azam FC au Simba SC.
Mchezaji Feisal Salum ( Fei Toto ) anatakiwa na Klabu Moja nchini Uturuki ( Turkey ) kwa Kiasi cha Shilingi Milioni 500 ila Viongozi wa Yanga SC waliikataa hiyo Hela.
Na hii ni mara ya Pili Viongozi wa Klabu hiyo maarufu huko nchini Uturuki ( Turkey ) kuja nchini Tanzania kumhitaji Mchezaji Feisal Salum ( Fei Toto ) ila Uongozi wa Yanga SC umewataka Walipwe ( Wamnunue ) kwa Shilingi Billioni 2 au Billioni 1.5 ila Jamaa wa Uturuki wamekomaa / walikomaa na Shilingi Milioni 500 yao.
Ni kwamba Mchezaji Feisal Salum ( Fei Toto ) angeenda katika Klabu hiyo nchini Uturuki ( Turkey ) angekuwa analipwa Mshahara wa Shilingi Milioni 90 au Milioni 80 kwa Mwezi.
Mratibu wa Jambo hili lote ni Bwana Abedi ( Abeid ) ambaye ni Msimamizi Mkuu wa Kituo cha Mafuta cha Camel Oil na hata Waturuki hawa wanamtumia kama Mtu Kati wao kwakuwa tu anajuana na Wakubwa wa Vilabu hivi Viwili vya Yanga SC na Simba SC.
Mwisho ni kwamba bahati mbaya pekee aliyonayo Mchezaji Feisal Salum ( Fei Toto ) ni kwamba achilia mbali Kutokuelewana Kwake na Uongozi wa Yanga SC ila pia Kumetokea na Janga Kubwa la Tetemeko la Ardhi huko nchini Uturuki ( Turkey ) ambalo limeathiri mno Uchumi wa Taifa hilo na huenda likaathiri pia hata Uchumi wa Vilabu vingi Vikubwa vya nchini humo hivyo kuwa Kikwazo Kwao hata katika Kumsajili Mchezaji huyo hali ambayo nina uhakika Kisaikolojia itakuwa imemuathiri sana na asipotuliza Akili au hata kupatiwa Msaada wa Kisaikolojia hali inaweza kuwa mbaya Kwake.
Haya wale mliozishutumu Klabu za Azam FC na Simba SC kuwa nyuma ya Sakata hili la Mchezaji Feisal Salum ( Fei Toto ) huku Wapuuzi Wengine hadi mkapanga Kugomea Kununua au Kutumia Bidhaa za Tajiri Mmoja mwenye Klabu yake fanyeni upesi au itisheni Press Conference muwaombe / muviombe Radhi.
Nimemaliza.
Mimi ndiyo GENTAMYCINE The King!!!