The Giantist
JF-Expert Member
- Dec 12, 2018
- 214
- 86
Wajumbe
Nasoma hapa ukurasa wa 5 mwanzoni kabisa, kwamba CCM imezamiria kustawisha maisha ya kila Mtanzania kwa kutokomeza umaskini na kuhakikisha taifa linafikia uchumi wa kati ( Kumbe bado hatujafika au wamecopy na kupaste ya 2015 😁😁😁😁 ) kwa kuongeza ajira zaidi ya MILIONI 8 ( 1,2,3 .... 8000001+ 🙄 )
waKat.png
EMBU CCM tuelezeni kwanza kwa miaka 5 mliyopewa mmezalisha ajira ngapi ( sio viwanda uchwara ) na kupoteza ajira ngapi , halafu hii twit hapa chini inamaana tuliingizwa choo cha kike .?
Kwanza Tanzania haijajitangaza yenyewe kwamba imeingia katika uchumi wa kati, ni Benki ya Dunia ndiyo iliyoitangaza. Na Rais Dkt. Magufuli aliandika kupitia Twitter kuishukuru Benki ya Dunia kwa kuitangaza nchi yetu kuingia katika uchumi wa kati. Mpaka hapo jifunze kuandika kwa utulivu pasipo kiherehere, alimradi uwafurahishe wajinga wenzako.
Kabla hujaanza kulalamikia ajira huna budi kufanya utafiti kuweza kujiridhizisha kwamba hili ni tatizo la hapa kwetu Tanzania au na mahala pengine Duniani kote? Kilio cha ajira ni cha vijana waliopo Duniani kote na hii imesababishwa na kukua kwa kasi sana katika nyanja za sayansi na teknolojia. Na ndio maana hata kibaraka chenu Lisu analifahamu jambo hilo, na ndio maana hata kwenye kampeni yake mbagala hakusema ataleta ajira Ila ni kubadili mfumo wa elimu ambao utawawezesha vijana wasomi waweze kujiajiri. Ndio kusema alikuwa anakubaliana na tatizo la ajira kwa vijana Duniani, na Tanzania ikiwemo katika namna yake hiyo. Na ukweli huo ni mabadiliko ya kukua kwa kasi sayansi na teknolojia.
Hata hivyo serikali ya CCM imekuwa katika hatua mbalimbali za kubadili mfumo wa elimu ili kuwawezesha vijana kuweza kujiajiri lakini pia kuweka mazingira ya kuwasaidia vijana wanawake na walemavu katika kuwezesha mitaji ambayo itawafaa katika kujiajiri kwao. Pia, serikali kupitia wizara ya elimu imeweza kuboresha shule za ufundi stadi ili kuweza kumudahili vijana wengi zaidi na pia kurasimisha ujuzi wa vijana ambao hawakupata katika mfumo rasmi kwa lengo hilo la kuondoa tatizo la ajira kwa vijana kwa kuwapa nafasi vijana kuweza kujiajiri na kuwaajiri wenzao.
Na hizo ajira milioni 8 ni kwamba zitaongezeka kufikia hapo kutoka ajira milioni 3 ambazo zimepatikana mpaka sasa kupitia miradi mbalimbali ya kiserikali. Ajira hizo ni zile zisizo rasmi na zile zilizo rasmi, ambapo binafsi nimeshuhudia kijana aliyefanya kazi hizo katika mradi wa SGR, baada ya kupata fedha zake aliachana na kazi hizo na sasa amefunguka stationery yake mjini kondoa. Kwa hiyo kupitia miradi hiyo vijana wanapata fedha za mitaji ya kuendesha biashara zao, na hivyo ndivyo hitaji la serikali ya CCM kwamba kupitia miradi vijana wataajiriwa na hatimaye kuweza kupata mitaji ya kujiajiri. Mapambano dhidi ya ukosefu kwa ajira kwa vijana, serikali ya CCM imeamua kupambana nayo katika namna hizo.