Kukamilisha ujenzi wa mradi wa kuzalisha umeme wa Julius Nyerere
(Julius Nyerere Hydro Power Project-JNHPP) unaotarajia kuzalisha
MW 2,115
(b) Kukamilisha usambazaji umeme katika vijiji vyote na maeneo yapembezoni mwa miji (miji-vijiji - Peri Urban areas) ya Tanzania Bara
kupitia Mpango wa Umeme Vijijini pamoja na kuandaa na kutekeleza
Mpango Kabambe wa Umeme Vijijini (Rural Energy Master Plan)
(c) Kukamilisha ujenzi wa mradi wa kuzalisha umeme kwa kutumia ges
asilia wa Kinyerezi I – Extension (MW 185) na mradi wa umeme wa
maji wa Rusumo (MW 80)
(d) Kukamilisha utekelezaji wa awamu ya pili (Phase II) wa mradi wa Backbone ambao unahusisha upanuzi wa vituo vya kupoza umeme vya Iringa, Dodoma, Singida na Shinyanga vyenye uwezo wa kV
400/220/33
(e) Kukamilisha ujenzi wa miradi ya kuunganisha Gridi ya Taifa na nchi
jirani ikiwemo njia ya kusafirisha umeme kV 400 kutoka Singida -
Arush Namanga itakayounganisha nchi za Tanzania na Kenya; na
njia ya kusafirisha umeme kV 400 kutoka Iringa - Mbeya - Tunduma
itakayounganisha nchi ya Tanzania na Zambia;
(f) Kukamilisha ujenzi wa mradi wa njia ya kusafirisha umeme kV 400
kutoka Julius Nyerere HP hadi Chalinze, njia ya kusafirisha umeme
kV 400 (North East) kutoka Kinyerezi - Chalinze - Segera - Tanga, na
njia ya kusafirisha umeme kV 400 kutoka Chalinze hadi Dodoma;
(g) Kukamilisha ujenzi wa miradi ya njia ya kusafirisha umeme kV 220
kutoka Rusumo hadi Nyakanazi, njia ya kusafirisha umeme kV 220
kutoka Geita hadi Nyakanazi na njia ya kusafirisha umeme kV 220
kutoka Bulyanhulu hadi Geita
(h) Kuongeza uwezo wa uzalishaji umeme wa kutosha na wa gharama
nafuu kwa kutumia vyanzo mbalimbali ikiwemo maji, gesi asilia, makaa ya mawe na nishati jadidifu (jotoardhi, upepo, jua na
tungamotaka). Baadhi ya miradi itakayopewa kipaumbele ni pamoja
na miradi ya umeme wa maji (Ruhudji MW 358, Rumakali MW 222,
Kikonge MW 300, Kakono MW 87 na Malagarasi MW 45) na gesi asilia
(Mtwara MW 300, Somanga Fungu MW 330, Kinyerezi III MW