Uchaguzi 2020 Ilani ya Chama cha Mapinduzi (CCM) 2020-2025
Kukamilisha ujenzi wa mradi wa kuzalisha umeme wa Julius Nyerere
(Julius Nyerere Hydro Power Project-JNHPP) unaotarajia kuzalisha
MW 2,115

(b) Kukamilisha usambazaji umeme katika vijiji vyote na maeneo yapembezoni mwa miji (miji-vijiji - Peri Urban areas) ya Tanzania Bara

kupitia Mpango wa Umeme Vijijini pamoja na kuandaa na kutekeleza
Mpango Kabambe wa Umeme Vijijini (Rural Energy Master Plan)

(c) Kukamilisha ujenzi wa mradi wa kuzalisha umeme kwa kutumia ges
asilia wa Kinyerezi I – Extension (MW 185) na mradi wa umeme wa
maji wa Rusumo (MW 80)

(d) Kukamilisha utekelezaji wa awamu ya pili (Phase II) wa mradi wa Backbone ambao unahusisha upanuzi wa vituo vya kupoza umeme vya Iringa, Dodoma, Singida na Shinyanga vyenye uwezo wa kV
400/220/33

(e) Kukamilisha ujenzi wa miradi ya kuunganisha Gridi ya Taifa na nchi
jirani ikiwemo njia ya kusafirisha umeme kV 400 kutoka Singida -
Arush Namanga itakayounganisha nchi za Tanzania na Kenya; na
njia ya kusafirisha umeme kV 400 kutoka Iringa - Mbeya - Tunduma
itakayounganisha nchi ya Tanzania na Zambia;

(f) Kukamilisha ujenzi wa mradi wa njia ya kusafirisha umeme kV 400
kutoka Julius Nyerere HP hadi Chalinze, njia ya kusafirisha umeme
kV 400 (North East) kutoka Kinyerezi - Chalinze - Segera - Tanga, na
njia ya kusafirisha umeme kV 400 kutoka Chalinze hadi Dodoma;

(g) Kukamilisha ujenzi wa miradi ya njia ya kusafirisha umeme kV 220
kutoka Rusumo hadi Nyakanazi, njia ya kusafirisha umeme kV 220
kutoka Geita hadi Nyakanazi na njia ya kusafirisha umeme kV 220
kutoka Bulyanhulu hadi Geita

(h) Kuongeza uwezo wa uzalishaji umeme wa kutosha na wa gharama
nafuu kwa kutumia vyanzo mbalimbali ikiwemo maji, gesi asilia, makaa ya mawe na nishati jadidifu (jotoardhi, upepo, jua na
tungamotaka). Baadhi ya miradi itakayopewa kipaumbele ni pamoja
na miradi ya umeme wa maji (Ruhudji MW 358, Rumakali MW 222,
Kikonge MW 300, Kakono MW 87 na Malagarasi MW 45) na gesi asilia
(Mtwara MW 300, Somanga Fungu MW 330, Kinyerezi III MW
Plan ishabadilika, kipaombele sasa ni kurudisha tabasamu usoni, pesa mfukoni na mzunguko wa Pesa mtaani...hayo ma miradi ya mwenda zake sidhani km wanayatilia umuhimu tena, labda yale ambayo yalishaanza...
 
km 294+km 130+km 250+km 411+km 360+km 156+km 356+km 1,253+km 1,000=4,210

Kama Dar - Moro ni km 300 imechukua miaka 5 na bado haijakamilika kwa hesabu za cross multiplication km 4,210 itachukua miaka mitano tena ambayo ni 2020 to 2025?
 
Mungu fundi sana kulibeba liwe jiwe. kwa ilani hii watumishi increment na madaraja wangeendelea kuota. yani wangelimia ulimi..
Manake pamoja na uchumi kushuka corona mwamba angekomaa kutandaza mivyuma ardhini...Mungu ni mwema.
 
Mama afanye linalowezekana. Mbona bandari ya bagamoyo tuliitelekeza? maendeleo ya vitu yaendane na ya watu. unahangaika kuchimba mabwawa huku watu wanalimia meno kisa tu wewe unashiba kwa kodi za dhulma.
 
km 294+km 130+km 250+km 411+km 360+km 156+km 356+km 1,253+km 1,000=4,210

Kama Dar - Moro ni km 300 imechukua miaka 5 na bado haijakamilika kwa hesabu za cross multiplication km 4,210 itachukua miaka mitano tena ambayo ni 2020 to 2025?
Mkuu, ulikuwa unakwenda vizuri sana, na nikataka kukupa 'like' ya furaha kabisa kwa fikra pevu.

Lakini umekosea padogo tu, na siwezi kukupa nusu 'like', kwa hiyo nakupa 'like' kamili.

Kama imechukua miaka mitano toka Dar hadi Moro, km300, ina maana kila mwaka mmoja zinajengwa km 60 tu!
km300 /5 = 60 km

Kwa hiyo, kwa hizo km 4,210/60 = 70.
Itachukua miaka 70 kujenga reli hizo kama kasi ya ujenzi itakuwa sawa na hii inayotumika kwa kipande cha Dar hadi Morogoro!
 
Miaka 5 wakati tuka mwaka wa sita na bado haijaanza kutumika.
 
sio lazima hayo yaliyoahidiwa yatekelezwe. Mbona kwenye kampeni za 2015, tuliahidiwa sh milioni 50 kila kijiji lakin hatukupewa?.
 
Na kwa akili zetu watanzania tunaona tunaweza.....

Tunahitaji mipango thabiti yenye kutekelezeka ndani ya muda na sio majumuisho ya mipango.

Vip CCM tukija na mpango wa maendeleo (tofauti na ule wa serikali) wa miaka 50 na kila Raisi akapita humo tena kwa mdadavuo wa kila miaka mitano.

Lakini MKUU naona kama umedata
 
Mkuu, ulikuwa unakwenda vizuri sana, na nikataka kukupa 'like' ya furaha kabisa kwa fikra pevu.

Lakini umekosea padogo tu, na siwezi kukupa nusu 'like', kwa hiyo nakupa 'like' kamili.

Kama imechukua miaka mitano toka Dar hadi Moro, km300, ina maana kila mwaka mmoja zinajengwa km 60 tu!
km300 /5 = 60 km

Kwa hiyo, kwa hizo km 4,210/60 = 70.
Itachukua miaka 70 kujenga reli hizo kama kasi ya ujenzi itakuwa sawa na hii inayotumika kwa kipande cha Dar hadi Morogoro!
🙏✍️🤝
 
Mungu fundi sana kulibeba liwe jiwe. kwa ilani hii watumishi increment na madaraja wangeendelea kuota. yani wangelimia ulimi..
Manake pamoja na uchumi kushuka corona mwamba angekomaa kutandaza mivyuma ardhini...Mungu ni mwema.
Crap
 
km 294+km 130+km 250+km 411+km 360+km 156+km 356+km 1,253+km 1,000=4,210

Kama Dar - Moro ni km 300 imechukua miaka 5 na bado haijakamilika kwa hesabu za cross multiplication km 4,210 itachukua miaka mitano tena ambayo ni 2020 to 2025?
hahahaha ila watu tunakosea sn magufuli madarakani aliingia mwezi wa 10/2015 sizani alianza na sgr hapo hapo naona tunachanganya alivyo kaa madarakani na tareh yakuanza ujezi wa sgr. naona tupunguze siasa tutafute ukweli tujenge hoja.

kingine naona hzo ni road map plan zina faida nying tu kwa taifa hata kama hazita tekelezeka. kwamba inaonyesha taifa lina maono mapana hata muwekezaji akija anaona mazur katika fikra zetu ndani ya miaka 20 mbele. kingine akija raisi mwengine awe na muungozo pia utakao mpa mawazo ya njisi yakuendeleza hiyo miradi
 
hahahaha ila watu tunakosea sn magufuli madarakani aliingia mwezi wa 10/2015 sizani alianza na sgr hapo hapo naona tunachanganya alivyo kaa madarakani na tareh yakuanza ujezi wa sgr. naona tupunguze siasa tutafute ukweli tujenge hoja
Ujenzi wa SGR umeanza 2016 na leo ni 2021
 
kingine naona hzo ni road map plan zina faida nying tu kwa taifa hata kama hazita tekelezeka. kwamba inaonyesha taifa lina maono mapana hata muwekezaji akija anaona mazur katika fikra zetu ndani ya miaka 20 mbele. kingine akija raisi mwengine awe na muungozo pia utakao mpa mawazo ya njisi yakuendeleza hiyo miradi

Ukurasa namba 94 wa ilani ya CCM 2020/2025 kuhusu ujenzi wa Reli​

Ujenzi wa SGR umeanza 2016 na leo ni 2021
acha mkuu
20210515_074159.png
 
ilani ingekua inatekelezeka yote kuna mtu angetoka madarakani analaumiwa kwel
Ni bora ukaandaa kidogo kikamilike kuliko kuandaa kikubwa usifanikiwe kukikamilisha, unaonekana muongo
 
Asante sana Mkuu kube ni 2017 maana niliona magorofa ya pale KAMATA yanavunjwa ilikuwa 2016 kumbe yalikuwa maandalizi tu
hapo n miaka 4 ss imepita hadi mwaka huu mwezi wa 4
Ni bora ukaandaa kidogo kikamilike kuliko kuandaa kikubwa usifanikiwe kukikamilisha, unaonekana muongo
hizo ni plan tu ila katika utekelezaji kuna mambo ya budget kuna priorities kwakua nchi sio reli tu alafu kingine tunategemea mikopo ya riba nafuu mbila kua na plan yenye ushawishi haupewi mkuu.
 
Ni bora ukaandaa kidogo kikamilike kuliko kuandaa kikubwa usifanikiwe kukikamilisha, unaonekana muongo
Akili ndogo kweli wewe... aim pakubwa hata ukipata kidogo ni sawa... watu wanawaza kwenda sayari za mbali wewe unataka twende moro... hii ni nchi na sio familia yako yenye mawazo finyu. Nyie ndo siku zote mnarudisha maendeleo nyumba kwa hofu kuogopa kufeli... pambana wewe, fikiri nje ya box.
 
Back
Top Bottom