Chagu wa Malunde
JF-Expert Member
- Jul 11, 2015
- 8,746
- 5,772
Ili taifa liwe na mwelekeo thabiti lazima kile kilicho ndani ya katiba kiheshimiwe. Ndio maana misingi ya utawala na hata utungaji wa sheria za nchi zetu lazima zirandane na katiba ya JMT. Kile kilichotamkwa na katiba ya JMT ndio mwanzo na mwisho juu ya mustakabali wa suala lolote.
Leo hii taifa letu linashuhudia mambo mengi tu ambayo ni kinyume na kabisa na kilichoandikwa ndani ya katiba yetu ya JMT. Mfano ibara ya 13 (1) ya katiba ya JMT imeweka wazi juu ya usawa wa kila raia mbele ya sheria za nchi nyetu. Lakini ukweli ni kuwa hili halipo hivyo. Tunashuhudia watu wengi wanafanya makosa na kwa kuwa ni viongozi au watumishi wa serikali wanalindwa na hata hawachuliwi hatua.
Ibara ya 13 (6)(b) imeweka wazi kuwa hakuna mtu ambaye atatiwa hatiani mpaka mahakama ithibishe hatia yake,lakini tumesuhudia watu wakichalazwa bakora hadharani na viongozi kama punda.
Ibara ya 23 (2) imetamka wazi kuwa kila mtanzania anayo haki ya kupata mshahara au ujira unaostahili,lakini tunashuhudia watumishi wa umma wakinug'unika kwa zaidi ya miaka mitano bila kupata nyongeza ya mishahara inayoendana na hali ya maisha.
Je, hili la wabunge waliofukuzwa Chadema na wao kukiri wazi kuwa wamefukuzwa kwa kukata rufaa lakini leo tunawaona wakitinga bungeni mbona linatia aibu!
Ibara ya 67 1(1)(b) imeweka wazi kuwa mbunge lazima awe mwanachama wa chama cha siasa aliyepitishwa na chama chake. Ibara ya 71(1) (e) imeweka wazi kuwa ukomo wa mbunge utakoma iwapo uanachama wake utakoma. Je, hawa waliofukuzwa ni wabunge?
Halina ubishi kuwa taifa letu linakwenda shagalabagala,maana katiba inakanyagwa na hii ni picha mbaya sana. Je wananchi nao wakija kuanza kutoitii katiba ya JMT nini kitafuatia? Maana tusiangalie sarafu upande mmoja kana kwamba sisi sio binadamu.