Ili taifa liwe na mwelekeo thabiti lazima kile kilicho ndani ya Katiba kiheshimiwe

Unapomaliza cku zako unatakiwa kwanza kuoga
 
Taifa lilikofikia ni kiwango cha juu kabisa cha kuamsha vurugu wakati wowote.

Katiba haiheshimiwi na watawala kisa wana bunduki zinazowalinda dhidi ya raia.

Ukweli ni kwamba umma wa watu hufikia mahali ambapo hawana uchaguzi ila na wao kutoiheshimu katiba kama watawala wao.
Ikifikia hapo ndipo unapo ona taifa likiingia katika machafuko.

Zimekuwepo nchi nyingi sana za mfano zilizofikia machafuko kwa sababu ya kiburi, kejeli, ukosefu wa busara unaosababishwa na watawala kutokuwa waadilifu wa kiapo chao cha kuilinda katiba yao.

Mfano mwingine wa karibu kabisa ni hili la polisi kumburuza na kumpa kipigo dreva wa lori hadi kifo halafu kwa ufupi na kejeli wana kuja na jibu la kwamba dereva huyo alikua na korona na hakuna aliewajibika.

Hivi ukamkuta mgonjwa kwenye viwanja vya hospitali amejipumzisha ukaanza kumburuza na kumpiga akafia mikononi mwako, jibu litakuwa raisi tu kwamba alikua mgonjwa ndio maana alilazwa?

Hata wale watakao kubalia jibu lako nao wana upungufu wa kufikiri vizuri(wavunjifu wa kanuni za haki ya kuishi)

Mungu rehemu taifa hili linaloshuka chini kwa kasi ya 5G.
 
Muheshimiwa Mungu ...muheshimiwa Raid
By Palamagamba Kabundi.
 
Umefafanua vyema.
 
Wewe una lako jambo.
Mahakama zipo, una haki ya kufungua shauri mahakamani ili majibu sahihi yapatikane,

Acha majungu.
Mahakama ipi hii inayoongozwa na Bwana Juma?
 
Mods kichwa cha habari ni taifa lililokosa mwelekeo baada ya viongozi watawala kushindwa kuilinda na kuiheshimu katiba. Nashangaa kwa nini mmerekebisha kana kwanba nimevunja sheria za JMT.
 
Mkuu wa mkoa ametia aibu,anadai eti marehemu hakutii bila shuruti.
 
Usitumie matako yako kutishia umma wa watanzania,hata Libya,Sierraleone na Uganda kulikuwa na masuala kama haya ya kutokuheshimu katiba za nchi.
Ni wewe mwenye mawazo hayo siyo umma wa watanzania! Mbona mliitisha maandamano mkazodolewa na umma wa watanzania. Usiilinganishe Tanzania na Libya, Uganda au Sierraleone, umma wa watanzania una unga mkono serikali yao (hii ya sasa) kwa zaidi ya asilimia 84.
You have failed miserable! Ulicho baki nacho ni ndoto tu! Endelea kuota.
 
Hata wewe umekuwa miongoni mwa hao wabunge wanawake usinge and Ila haya maneno,
Kuhusu usawa anajua ni haki lakini Nina uhakika hata wewe Kama una familia unajua hujaweka usawa unaoutaka hapa jukwaani,
Jambo hilo ni kubwa Ila linatatulika pale kipato kinapotosha kufanya hivyo na kubaki ziada, vinginevyo hapa duniani bado sana.
Narudia tena,hata wewe hujaweka usawa kwenye jamii yako inayokuzunguka.
 
Acha unafiki Mkuu. Kuna mvunja katiba nchi kama Mheshimiwa Rais ambae huwa unamtetea kuliko hata unavyoweza kumtetea mama yako mzazi!
Wanaanza kutafutana wenyewe kwa wenyewe. Ukiona hivyo maslahi yaliyotegemewa yameyeyuka😂
 
Wameanza kutest mitambo huko dodoma. Sauti zimeanza kusikika toka bungeni kuwa aongezewe muda!
Yameshafanyika mengi ya kipumbavu kabisa nkasema anafanya kwa nia njema nia njema bila kufuata katiba ni Uhaini tu.
Ivi raisi wa nchi anawezaje kuamuru manunuzi makubwa kama ndege bila kupata idhini ya bunge tena akaenda mbali na kuacha kabisa kutumia sheria ya manunuzi? Alikuwa na watengeneza ndege chumban ikulu akiagiza anazotaka yye. Unajua 10% ya kununua ndege moja????
 
Kaa na watu usikie manugu'uniko yao acha kukariri,huu uzi hauhusiani na Chadema wala Ccm. Watanzania wanamalamiko mengi, nyongeza ya mishahara, watun wanauliwa na vyombo vya usalama na viongozi wanajichukulia sheria mkononi; Haya yote yanahusika na Chadema? Wewe hukai na watu bali unaishi maisha ya mitandaoni.
 
Somo hapo juu sio usawa,ni katiba kuheshimiwa.
 
Ndio unaamka sasa, toka awamu hii imeingia madarakani, namba moja ndio amekuwa kinara wa kuvunja katiba, na taasisi nyingine zote zimekuwa zikifanya hivyo kwani ndio anayeamua katiba itekelezwe vipi.
 

Zile propaganda ulizokuwa unahubiri hapa ndio huyo uliyemquote amezivaa, saa hii ww umeamua kuongea ukweli mmebaki mnagongana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…