Ili taifa liwe na mwelekeo thabiti lazima kile kilicho ndani ya Katiba kiheshimiwe

Zile propaganda ulizokuwa unahubiri hapa ndio huyo uliyemquote amezivaa, saa hii ww umeamua kuongea ukweli mmebaki mnagongana.
Unanifahamu vizuri? Unadhania mimi ni mtu wa kudeal na propaganda kama huyu mtu unaemshadidia.
 
Kulinda katiba ama kutolinda katiba kwa sasa inategemea na utashi na maono ya kiongozi aliyoko madarakani hii ni hali mbaya sana kwa mustakabali wa nchi kwa siku za mbeleni. Wananchi tuweni wanyenyekevu kwa kupiga magoti tuwaombe waheshiwa waliopo madarakani watuapatie katiba iliyobora yenye misingi thabiti ndani yake ambayo itatoa mwongozo wa namna ya kuilinda katiba.
 
🤣 🤣 🤣 🤣 🤣 🤣
Nimejikuta nacheka sana!

Yaani fisi apate ufunguo wa bucha halafu uende kumuomba huyo huyo fisi atoke nje mjenge mlango mwingine utakaomdhibiti asiingie buchani na kujilia vinono bila vizuizi?!!

Pole sana mkuu, ila hizo ni ndoto za Alinacha.
 
Kwa nini raia wengi wako kimya juu ya hili? Wanasheria wetu na watetezi wa haki za binadamu mko wapi? Wabunge wanaoelewa matakwa yanakanyagwa mko wapi?
 
Hongeraa mtoa mada,kama no uandishi na mtazamo wako isiwe tu akaunti imeingia mikono isiyo yako.
 
Sidhani kama kuna njia nzuri ya kutafuta katiba mpya kwa amani bila kulamba miguu wahusika japo si kazi rahisi kwao kukubali ila juhudi za kupiga kelele kwa amani hilo linaweza kufanikiwa. Ila tatizo linalotusumbua Watanzania tuliokuwa wengi ni ubinafsi na roho ya kwanini hapo itatuwia vigumu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…