Ilikuaje Jesca Magufuli aliyepata four ya 30 mwaka 2011 st Mathew akaruhusiwa kusoma Degree mwaka 2014?

Ilikuaje Jesca Magufuli aliyepata four ya 30 mwaka 2011 st Mathew akaruhusiwa kusoma Degree mwaka 2014?

Kwani s mnasema vilaza ni kina mwajuma na da waa
 
Jamani mbona mumemkomalia sana huyu mtoto? Hayo matokeo aliyonayo DDDC FFF kwa vyuo vyetu atashindwa kujiunga kozi yoyote ya diploma? Diploma za arts zote ni miaka 2 kabla ya 2017...afu 2014 ukaanza degree...utashindwa kumaliza 2017? Ukiunga masters huo mwaka utashindwa kumaliza 2019?....mbona sio mtanzania wa kwanza?.....hata babaake mbona alisoma kwa njia hii?.....ndalichako alipofuta zile diploma za UDOM ulifikiri ni kitu gani kile??.....
Nashangaa wamemkakia kooni dada wa watu ,wakati Kuna vilaza kibao
 
Samahani wewe uliyepata one upo wapi sasa hivi?? Mwenzako alipata four baadaye akaja kuwa amiri jeshi mkuu! Wewe endelea kung'ang'ania division! Nani alikudanganya kupata one unakuwa na akili???Kwa hii elimu ya Tanzania????????????


Tatizo mashindano ya darasani mnaleta mpaka mtaani halafu unakuta wale vilaza wanatusua unaanza kuona wivu, yaani unaona kama hawastahili vile kuwa na maisha mazuri!
Yaani inashangaza sn
Mpk sielewi dada wa watu wamemkomalia as if ye wa kwanza au bongo kufauku ndo issue.
Watu vipanga wako mtaani tu
 
Muacheni huyu Dada....mind your own business
 
Labda alisoma certificate kisha diploma akapata GPA kubwa akapata sifa za kusoma bachelor degree.
Yupo binti amesoma kupitia mfumo huu na Sasa ni Tutorial assistant wa chuo kikuu flani.
Bachelor degree na diploma alipata first class GPA above 4.3 kote

O-level ufaulu wa Div 4 Kama Jessica Magufuli. Alipata hivyo o-level sababu ya changamoto flani za maisha. Ila ana akili sana tena sana. Huko chuo alipata mazingira mazuri kidogo ya kujifunza na unafuu wa maisha.
 
Mtoa mada punguza upumbavu, kwani Nini kinashindikana? Kama alirudia kufanya mtihani na kupata vigezo vya kusoma five na six kwanini hasisome degree, acha kuleta madq za kipumbavu,tena ukomee.
 
Back
Top Bottom